TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Thursday, 20 November 2014

WAKULIMA WA SHAYIRI MONDULI WAELEZEA MAFANIKIO YA UFADHILI WA TBL


Pichani ni baadhi ya nyumba za Mkulima wa Shayiri, Barrick Kivuyo zikionekana baada ya kuwa amezifanyia ukarabati ikiwa ni pamoja na kuweka umeme wa jua (Solar)
 Mkulima wa Shayiri akionesha moja ya Ghala lake (Stoo) kwa ajili ya kuhifadhia zana mbalimbali za kilimo ikiwamo utunzaji wa pembejeo, ambapo jengo hilo amelijenga kutokana na fedha za Shayiri.
Baadhi ya Wanawake wanaojishughulisha na kilimo cha Shayiri wakiwa katika picha ya pamoja na Ofisa wa  Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha anayesimamia wakulima katika eneo hilo la Monduli Juu, wilayani Monduli mkoani Arusha.
Mkulima wa Shayiri wilayani Monduli Meporoo Losulu akionesha Trekta zake mbili ambazo amezinunua kutokana na kilimo cha Shayiri, pichani nyingine akizungumza kuelezea mafanikio yake. 

TIMU YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO YAKAGUA MADARAJA LUHEKEI MKOANI RUVUMA

SONY DSC
Meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoani Ruvuma, Mhandisi Abraham Kissimbo akizungumza na timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofika ofisini kwake. SONY DSC
Kiongozi wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (mwenye koti jekundu) pamoja na timu yake wakijinea Daraja la Luhekei C lenye urefu wa mita 60. SONY DSC
Kiongozi wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (mwenye koti jekundu) pamoja na timu yake wakijinea Daraja la Luhekei C lenye urefu wa mita 60. SONY DSC
Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja na  mwenyeji wao Mhandisi Lusage Mulenzi katika kibao cha ufunguzi rasmi wa Darala la Luhekei C. Daraja hili lina urefu wa mita 60, lilifunguliwa rasmi tarehe 18 Julai, 2014 na Mheshimiwa Rais, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
PICHA ZOTE NA SAIDI MKABAKULI

MISS HONDURAS, DADA YAKE WAKUTWA WAMEUAWA


 
Miss Honduras, Maria Jose Alvarado (kulia) akiwa na dada yake Sofia Trinidad enzi za uhai wao.


Miss Honduras, Maria Jose Alvarado aliyekuwa anatarajia kushiriki Miss World jijini London.GPL(P.T)


Mpenzi wa Sofia, Plutarco Antonio Ruiz akiwa mikononi mwa polisi.
MISS Honduras, Maria Jose Alvarado, 19, na dada yake Sofia Trinidad, 23, wamekutwa wamekufa baada ya kupotea tangu Alhamisi iliyopita.
Warembo hao walipotea Alhamis iliyopita ya Novemba 13, mwaka huu mara baada ya kutoka kwenye sherehe ya bethidei katika Mkoa wa Santa Barbara.
Maria Jose Alvarado ni miongoni mwa warembo waliokuwa wanatarajiwa kushiriki mashindano ya Miss World jijini London.
Watu wanne akiwemo mpenzi wa Sofia aitwaye Plutarco Antonio Ruiz wanashikiliwa na polisi kusaidia uchunguzi.
Miili ya wawilihao imekutwa katika Kijiji cha Cablotales village, karibu na Mto Aguagua imeelezwa.

WATOTO 130000 WANAISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI

unnamed

Wajumbe kutoka asasi za umma na za binafsi za ndani na nje ya nchi zinazoshughulikia mambo ya Ukimwi waliohudhuria kongamano la nne la kitaifa linalohusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kwa watoto wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa kongamano hilo. Hadi sasa watoto wenye maambukizi ya VVU 130000 wameweza kufikiwa kati ya hao 39317 wamepewa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
unnamed1
Baadhi ya wajumbe kutoka asasi za umma na za binafsi za ndani na nje ya nchi zinazoshughulikia mambo ya Ukimwi wakimsikiliza Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Pindi Chana (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la nne la kitaifa linalohusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kwa watoto. Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Taasisi ya Elizabeth Glaser Pediatric Aids (EGPAF).
……………………………………………………………………………..
 TAKWIMU zinaonesha kwamba watoto 130000 wana maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU) kati ya hao 39317 wamefikiwa na kupatiwa huduma ya dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Pindi Chana wakati akifungua kongamano la nne la kitaifa la VVU na UKIMWI kwa watoto linalofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere uliopo jijini Dar-es-salaam.
Dkt . Chana alisema asilimia 39 ya watoto walio katika hatari ya kupata maambukii ya UKIMWI hupimwa vipimo vya kubaini maambukizi ya VVU ndani ya miezi miwili baada ya kuzaliwa hivyo basi kuna umuhimu kwa watoto hawa kupata huduma za tiba mapema.
Akizungumzia maambukizo ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto waziri huyo alisema Tanzania imepiga hatua katika kuzuia maambukizo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto lengo likiwa ni kutokomeza kabisa maambukizi mapya kwa watoto wachanga.
“Mama wajawazito na wale wanaonyoyesha wanapatiwa huduma ya dawa za kupunguza makali ya VVU mara tu wanapogundulika kuwa na maambukizo, kupitia mpango mpya unaojulikana kama ‘uwezekano namba 2 au (Option B+)”, alisema Dkt.Chana
Alisema kufikia mwezi Juni mwaka huu jumla ya akina mama 940900 kati ya 1050043 hii ni sawa na asilimia 89.6% ya waliohudhuria kliniki walipimwa UKIMWI kati ya hao 47856 takribani asilimia 5 walikutwa na maambukizi ya VVU.
Kwa upande wa watoto 20569 walipima kipimo cha DBS kati ya hao 2063 hii ni sawa na asilimia 10 walikutwa na maambukizo ya VVU.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mbando, alisema ingawa nchi imepiga hatua katika mapambano ya kudhibiti UKIMWI hali halisi inaonyesha kuwa bado kuna maambukizo yanatokea sio tu kwa watu wazima bali na kwa watoto pia.
“Ni jukumu letu kuendelea kuweka mikakati ya dhati na kuisimamia ili kuhakikisha lengo la kutokomeza maambukizo ya VVU tunalifikia kwani mwaka 1986 maambukizi yalikuwa juu kwa asailimia 18 lakini hivi sasa yameshuka na kufikia asilimia 5.3”, alisema Dkt. Mbando
Kwa upande wake Mkurugenzi wa ufundi kutoka Taasisi ya Elizabeth Glaser Pediatric Aids (EGPAF) ambao ni waandaaji wa kongamano hilo Chrispin Kimario alisema ni muhimu kwa wazazi na jamii kushirikiana kwa pamoja na kulibeba jukumu la kuhakikisha kila mama mjamzito anapata huduma ya vipimo husika na matibabu kwa wakati.
Kimario alisema, “Watoto wameachwa nyuma, ni vyema tukumbuke kuwa mtoto hawawezi kujipeleka wenyewe hospitali kupima afya zao, hivyo ni jukumu letu wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuhakikisha watoto hawa wanapata huduma wanazostahili”.
Kauli mbiu ya kongamano hilo la siku mbili ambalo limehudhuriwa na wadau wa afya kutoka asasi za umma na binafsi za ndani na nje ya nchi ni ongeza kasi: Rahisisha upatikanaji wa utumiaji wa huduma za VVU na Ukimwi, pata matokeo chanya ya afya za mama na watoto wanaoishi na VVU.

Wednesday, 19 November 2014

KONGAMANO LA NNE LA TAIFA LA WATOTO NA VVU NA UKIMWI KUFANYIKA NOVEMBA 19-20-2014 KATIKA UKUMBI WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE


 Mwakilishi kutoka Kitengo cha Taifa cha Kudhibiti Ukimwi (NACP), Dk. Anath Rwebembera.
 Makamu wa Rais wa EGPAF, Anja Giphart (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi wa EGPAF Tanzania, Dk. Chrispine Kimaro na Mwakilishi kutoka Kitengo cha Taifa cha Kudhibiti Ukimwi (NACP), Dk. Anath Rwebembera.
 Mwakilishi kutoka Kitengo cha Taifa cha Kudhibiti Ukimwi (NACP), Dk. Anath Rwebembera (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Kongamano la nne la Taifa la Watoto na VVU na Ukimwi litakalofanyika leo Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Kutoka kushoto ni Mratibu wa  Mawasiliano  wa Shirika la Huduma za Watoto la Elizabeth Glaser Pediatric Foundation (EGPAF), Tanzania, Mercy Nyanda na Makamu wa Rais wa EGPAF, Anja Giphart.
 Mkurugenzi wa Ufundi wa EGPAF Tanzania, Dk. Chrispine Kimaro (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
  Mratibu wa Mawasiliano wa Shirika la Huduma za Watoto la Elizabeth Glaser Pediatric Foundation (EGPAF), Tanzania, Mercy Nyanda (kushoto), akitambulisha meza kuu kwa wanahabari.
 Mratibu wa Mawasiliano wa Shirika la Huduma za Watoto la Elizabeth Glaser Pediatric Foundation (EGPAF), Tanzania, Mercy Nyanda.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

Dotto Mwaibale

ASILIMIA 26 ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanaohitaji matibabu ya dawa za kurefusha maisha (ARV's) baada ya kuathirika na virusi vya Ukimwi hawapati huduma hiyo.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirika la Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation (EGPF), Chrispine Kimario alitoa kauli hiyo Dar es Salaam leo wakati akitoa taarifa ya Kongamano la Nne la Watoto na Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Alisema kongamano hilo lina kaulimbiu inayosema 'Kuongeza Kasi Kuimarisha Upatikanaji wa Huduma Vipimo Matunzo na Tiba ya VVU ili Kuboresha Maisha ya Mtoto', ambapoasilimia 7.6 ya watoto walioathirika na virusi hivyo ndiyo wanaopata matibabu. 

"Hapa nchini watoto wengi wamekuwa wakiugua ugonjwa wa Ukimwi kutoka kwa mama pindi tu wanapozaliwa na hiyo ndiyo inasababisha ongezeko la watoto wenye virusi," alisema.
Alisema kongamano litasaidia watu kupanga mipango mkakati wa kupambana na tatizo hilo.

Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Aneth Lubembere alisema uzingatiaji mkuu utakuwa katika malengo mapya yaliyotangazwa ya agenda ya dunia mwaka 2015.

"Agenda hizo ni asilimia 90 ya watu waliopimwa, asilimia 90 ya watu wanaoishi na VVU na walio katika matibabu na asilimia 90 ya watu wanaoendelea kwenye huduma na matunzo na tiba ya kupunguza kabisa virusi," alisema. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

MAONYESHO YA JUKWAA LA TIBA ASILIA TANZANIA YAFANYIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA DAR ES SALAAM


 Kamishna Mkuu wa Ustawi wa Jamii nchini, Danford Makala (wa pili kulia), akiwa ameongozana na viongozi wa Jukwaa la Tiba Asilia Tanzania wakati akielekea kutembelea mabanda katika maonesho hayo.
 Mganga Mtafiti wa Tiba Asilia na Magonjwa Sugu na Ukimwi Tanzania, Ahmad Darusi (kulia), akimuelekeza jinsi dawa zake zinavyofanya kazi, Kamishna Mkuu wa Ustawi wa Jamii nchini, Danford Makala (kushoto), wakati akitembelea mabanda ya maonesho ya Jukwaa la Tiba Asilia Tanzania yaliyofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Waganga Watafiti wa Tiba Asilia Tanzania (Umawati), Dk. Salehe Mohamed na Mwenyekiti wa Chama cha Utabibu wa Dawa Asili Tanzania (ATME), Simba Simba.
 Mkurugenzi wa Huduma ya Uponyaji, Wilfred Mwazini akimpa zawadi Kamishna Mkuu wa Ustawi wa Jamii nchini, Danford Makala wakati wa maonesho hayo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mchicha Natural Food  Products, Rose Mkoma (kulia), akiwahudumia wateja waliotembelea banda lake kwenye maonesho hayo.
 Dk. Richard Kayombo (kushoto), kutoka Rich Herbbs Medicines akimuelekeza jambo Edina Tesha baada ya kutembelea banda lake.
 Tabibu Elias Samweli kutoka Baangoi Herbalist Clinic akiwa na bidhaa zake kwenye maonesho hayo.
  Mganga Mtafiti wa Tiba Asilia na Magonjwa Sugu na Ukimwi Tanzania, Ahmad Darusi (kushoto), akiwa na watabibu wenzange kwenye maonesho hayo.
 Mkurugenzi wa Utafiti na Utawala, Dk.Crispo Musyangi 
akiwa mbele ya bidhaa zake katika maonesho hayo.
Tabibu akiandaa dawa zake kwenye maonesho hayo

Monday, 17 November 2014

TAMASHA LA KUONYESHA VIPAJI BAINA YA WANAFUNZI WA SHULE ZA ST MARY’S INTERNATIONAL ZA DAR ES SALAAM LAFANA

001
Mkurugenzi wa Shule za St Mary’s, mama Getrude Lwakatare akizungumza na wanafunzi wa Shule za St Mary’s International za Dar es Salaam wakati akizundua tamasha la kuonyesha vipaji vya wanafunzi wa Shule za St Mary’s International za Dar es Salaam lililofanyika Novemba 15, 2014 jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa. 
002
Mwalimu wa Shule ya St Mary’s International, Eric Sendi akiwaasa wanafunzi waandelee kuonyesha vipaji vyao.mm
003Mkurugenzi wa Shule za St Mary’s, mama Getrude Lwakatare (kushoto), akikabidhiwa baadhi ya Peni na Meneja Masoko wa Kampuni ya SILAFRICA, Salman Pathan kama mchango wake kwaajiliya shule za St Mary’s International.
006
Wanafunzi kutoka shule za St Mary’s International za Dar es Salaam wakiwa kwenye tamasha hilo.
 007
Wanafunzi kutoka shule za St Mary’s International za Dar es Salaam wakitoa burudani wakati wa tamasha la kuonyesha vipaji.
Tamasha Hilo lililoshirikisha Shule za Mbagala, Tabata na Mbezi Junior lililenga kuonyesha vipaji vya wanafunzi katika sanaa ya kucheza, kuimba na sarakasi.
Akizungumza wakati wa kuzindua tamasha Hilo,Mkurugenzi wa Shule za St Mary’s, Mheshimiwa Mama Getrude Lwakatare, Alisema ukuzaji wa vipaji Ni sehemu muhimu ya Shule za St Mary’s International.
‘Leo Ni Siku muhimu kwetu sisi kama St Mary’s Kwani pamoja na elimu bora tunayoitoa, Lakini pia tunasisitiza umuhimu wa vipaji Kwa wanafunzi wetu ‘ Alisema Mheshimiwa Mama Lwakatare.
Tamasha Hilo Ambalo limeandaliwa Kwa kushirikiana na Tanzania House of Talent, limedhaminiwa na Simtank ambao wametoa peni pamoja na tenki moja.

NISHATI NA MADINI WATAKIWA KUBORESHA TATHMINI YA MAPENDEKEZO YA MIRADI

Picha Na 1
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Rasilimaliwatu  Lusius Mwenda kutoka  Wizara  ya Nishati na Madini akifunga awamu ya kwanza ya mafunzo ya jinsi  ya kuandaa mapendekezo ya miradi, sera pamoja na utekelezaji wake yaliyofanyika mwishoni mwa wiki  mjini Bagamoyo. Mafunzo hayo yalishirikisha wataalamu kutoka Wizara  ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)  na Kampuni ya Uendelezaji  wa Jotoardhi (TDGC)
Picha Na 2
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini hotuba  ya ufungaji wa mafunzo hayo iliyokuwa inatolewa na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Rasilimaliwatu  Lusius Mwenda (hayupo pichani)
Picha Na 3
Afisa Rasilimali watu kutoka Idara ya Utawala Judith Ntyangiri akipokea  cheti cha   ushiriki mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo
Mwishoni mwa wiki Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Lusius Mwenda, alifunga  awamu ya kwanza ya mafunzo ya jinsi  ya kuandaa mapendekezo ya miradi, sera pamoja na utekelezaji wake yaliyofanyika mwishoni mwa wiki  mjini Bagamoyo.
 Mafunzo hayo yalishirikisha wataalamu kutoka Wizara  ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)  na Kampuni ya Uendelezaji  wa Jotoardhi (TDGC). Pamoja  na kufunga mafunzo hayo, alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa washiriki na kuwataka kuboresha tathmini ya mapendekezo ya miradi ( project proposals)
Ninawasilisha kwenu habari pamoja na picha za matukio ambazo zimeambatishwa pamoja na email hii.  Pia captions zimeambatishwa

JAJI MKUU AMJULIA HALI RAIS KIKWETE MAREKANI

1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe
Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba
16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins
jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika
hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. Kushoto ni mke wa
Rais Mama Salma Kikwete. Jaji Mkuu yuko Marekani kwa ziara ya kikazi
ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria
mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi
jijini Washington na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na
marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia  wa ujenzi wa maendeleo
ya mahakama
2: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake
waliopomtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika
hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore,
Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo
alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.  Jaji Mkuu na ujumbe wake wako
Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na
ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya
Sheria ya Ushahidi jijini Washington  na pia kukutana na taasisi
mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia
wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. Wengine kutoka kushoto ni Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula, Jaji wa Mahakama ya
rufani Mhe Ibrahim Juma, Msajili wa Mahakama Kuu Mhe Ignass Kitusi,
daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi na Mtendaji Mkuu wa Mahakama
Mhe Hussein Katanga.3Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu Mhe Mohamed
Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16,
2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini
Baltimore, Maryland.  Jaji Mkuu yuko  Marekani kwa ziara ya kikazi
ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria
mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi na
pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo
katika ili  kupata wabia  wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama.5

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Afisa wa Ubalozi wa
Tanzania nchini Marekani  Dkt. Sweetbert Mkama ambaye alimsindikiza
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman kwenda kumjulia hali
jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 20146Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Meja Jenerali Adolph
Mutta ambaye alimsindikiza Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande
Othman kwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili
Novemba 16, 20147Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Mtendaji Mkuu wa
Mahakama Mhe Hussein Katanga. ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara wa
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia
hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 20148Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Msajili wa Mahakama Kuu
ya Tanzania Mhe Ignass Kitusi  ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara
wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda
kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 20149Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Balozi wa Tanzania
nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula aliyesindikiza   msafara wa Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali
jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 201410Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Jaji wa Mahakama Ya
Rufani Tanzania Mhe Ibrahim Juma  ambaye ni mmoja wa wajumbe wa
msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman
walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili
Novemba 16, 2014
11Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Jaji Mkuu wa Mahakama ya
Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali
Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya
Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada
kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.  Jaji
Mkuu na ujumbe wake wako  Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja
na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa
kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington  na
pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo
katika ili  kupata wabia  wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama.