Kamishna Mkuu wa Ustawi wa Jamii nchini, Danford Makala (wa pili kulia), akiwa ameongozana na viongozi wa Jukwaa la Tiba Asilia Tanzania wakati akielekea kutembelea mabanda katika maonesho hayo.
Mganga Mtafiti wa Tiba Asilia na Magonjwa Sugu na Ukimwi Tanzania, Ahmad Darusi (kulia), akimuelekeza jinsi dawa zake zinavyofanya kazi, Kamishna Mkuu wa Ustawi wa Jamii nchini, Danford Makala (kushoto), wakati akitembelea mabanda ya maonesho ya Jukwaa la Tiba Asilia Tanzania yaliyofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Waganga Watafiti wa Tiba Asilia Tanzania (Umawati), Dk. Salehe Mohamed na Mwenyekiti wa Chama cha Utabibu wa Dawa Asili Tanzania (ATME), Simba Simba.
Mkurugenzi wa Huduma ya Uponyaji, Wilfred Mwazini akimpa zawadi Kamishna Mkuu wa Ustawi wa Jamii nchini, Danford Makala wakati wa maonesho hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mchicha Natural Food Products, Rose Mkoma (kulia), akiwahudumia wateja waliotembelea banda lake kwenye maonesho hayo.
Dk. Richard Kayombo (kushoto), kutoka Rich Herbbs Medicines akimuelekeza jambo Edina Tesha baada ya kutembelea banda lake.
Tabibu Elias Samweli kutoka Baangoi Herbalist Clinic akiwa na bidhaa zake kwenye maonesho hayo.
Mganga Mtafiti wa Tiba Asilia na Magonjwa Sugu na Ukimwi Tanzania, Ahmad Darusi (kushoto), akiwa na watabibu wenzange kwenye maonesho hayo.
Mkurugenzi wa Utafiti na Utawala, Dk.Crispo Musyangi
akiwa mbele ya bidhaa zake katika maonesho hayo.
Tabibu akiandaa dawa zake kwenye maonesho hayo
No comments:
Post a Comment