TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Showing posts with label Maisha. Show all posts
Showing posts with label Maisha. Show all posts

Monday, 10 November 2014

UMUHIMU WA KUTOKA ‘OUT’ NA UMPENDAYE

NI Jumatatu nyingine tunapokutana katika uwanja wetu huu mzuri, tukijuzana na kuelimishana kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo mapenzi. Mada yetu ya leo ni kama inavyojieleza hapo juu.
Je, mara ya mwisho kwa wewe na mpenzi wako kutoka ‘out’ ilikuwa ni lini? Una desturi ya kutoka na umpendaye, mkaenda mahali tulivu ambapo mtapata muda wa kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu maisha na mapenzi? Kama jibu lako ni hapana, unaishi kwenye mapenzi yaliyokosa uhai. Maisha yanaenda kasi sana, wanandoa wengi au watu ambao wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi, wanajikuta wakikosa kabisa nafasi ya kuwa pamoja kutokana na kila mmoja kuweka kipaumbele katika kazi, biashara au shughuli nyingine za utafutaji pesa au malezi ya watoto.
Matokeo yake, watu wengi wanaishi kwa mazoea tu lakini katika uhalisia, mapenzi yanakuwa yamepungua sana au hayapo kabisa.
KUTOANA OUT HUFUFUA MAPENZIWatafiti wa mapenzi wanaeleza kwamba hakuna kazi ngumu kama kuishi pamoja wewe na mpenzi wako, iwe ni kwenye ndoa au uhusiano wa kawaida wa kimapenzi kwani ni rahisi sana watu kuchokana. Hata kama unampenda vipi, lazima kuna muda utamchoka au utachoshwa na mazingira ambayo mmekuwa mkiishi siku zote.
Unapofikia hatua hii, kitu pekee kinachoweza ku-refresh akili na hisia zako, ni wewe na umpendaye kutoka pamoja na kwenda sehemu tofauti kama ufukweni, hotelini au sehemu yoyote tulivu ambayo mtakaa pamoja, mtakunywa au kula na kufurahi. Kitendo hiki kinatajwa kuwa siri kuu ya kufufua mapenzi na kuondoa ile hali ya kuchokana.
Haijalishi umeishi kwa muda gani na mpenzi wako, hata kama mna miaka kibao, lazima muendelee kutoana out mara kwa mara. Hata kama tayari mmeshazaa watoto na wamekuwa wakubwa, suala la out halikwepeki kama mnataka kuishi kwa amani na upendo. Wengi wanaamini kwamba mpenzi mpya pekee ndiye anayetakiwa kutolewa ‘out’, jambo ambalo siyo sahihi.
Mkirudi, kila mmoja atashangaa kwamba mapenzi yake kwa mwenzake, yatazidi maradufu, kama kulikuwa na migogoro ya hapa na pale, itaisha na mtaendelea kuishi kwa amani na furaha.
SIYO LAZIMA UWE TAJIRI KUTOKA OUTWengi tunasumbuliwa na kasumba kwamba ili kumtoa mpenzi wako out, ni lazima waleti yako iwe imejaa, lazima mkatumie fedha nyingi au lazima umpeleke sehemu ya gharama. La hasha, siyo lazima kabisa.
Kwa mfano, inakugharimu nini wewe na mpenzi wako kutoka na kwenda ufukweni, mkaagiza soda, maji au vinywaji mnavyovipenda, mkakaa kwenye mchanga wa bahari na kupunga upepo mwanana?
Hata kama hakuna ufukwe hapo mnapoishi, mnaweza kutoka na kwenda sehemu yoyote tulivu, iwe ni kwenye uwanja wa mpira muda ambao hakuna watu, sehemu za milimani au mahali popote ambapo mtakuwa wawili tu, inatosha kabisa. Unaweza kununua matunda, vinywaji au vitafunwa mnavyovipenda, mkaenda navyo mpaka sehemu mliyoichagua, siyo lazima uwe na fedha nyingi.
MAMBO YA KUZINGATIA MKIWA OUT
Ili mtoko wako na umpendaye ukamilike, kuchagua sehemu ya kwenda ni jambo la kwanza lakini kubwa zaidi, lazima ujue kwamba mkiwa ‘out’, unapaswa kufanya nini ili mpenzi wako afurahi na kufufua upya hisia za mapenzi ndani ya moyo wake.
Ukishindwa kujua nini cha kufanya na kipi hutakiwi kabisa kufanya mkiwa out, badala ya kufufua mapenzi, unaweza kujikuta unaongeza ufa hivyo ni lazima kila mmoja ajue anatakiwa kufanya nini anapokuwa out.
Tukutane wiki ijayo ili kujuzana nini unatakiwa kufanya na kipi hutakiwi kabisa kufanya mnapotoka out na umpendaye. Vitabu vya ufundi katika mapenzi vinapatikana kwa wakazi wa Dar. Piga namba za hapo juu kwa maelezo.

Thursday, 30 October 2014

HII NI KWA WANAWAKE NA WASICHANA WANAOPITIA CHANGAMOTO MBALI MBALI ZA KIMAISHA.


umekuwepo na hali ya kuchaguliana nini cha kufanya kwenye maisha.Hali ambayo hupelekea wengine kupata msongo wa mawazo kisa kuona hawakubaliki katika jamii fulani.Au kuona kuwa hathaminiki kisa ana utaratibu flani wa kimaisha tofauti na wengine.

Kumcheka mtu kwa sababu ya muonekano fulani bila kujali kuwa huo muonekano umekuja baada ya kupitia changamoto fulani katika maisha.Wakati mwingine wanawake ndio hao hao hukaa na kunyoosha vidole kumcheka mwanamke mwenzao.Wasichana wanamkejeli na kumdhihaki msichana mwenzao kisa muonekao or style flani ya maisha.Nimetumia mfano wa wanawake kwa sababu ndio wanaongoza kwa tabia hiyo dhidi ya wanawake wenzao.



Picha hizi ni kazi ya mwanadada Carol Rosseti wa Brazil.Amechora na kutengeneza picha hizi kuwatia moyo na kuiasa jamii kuacha maneno ya dharau na kejeli kwa wanawake.

 


b







Je wewe upo wapi?

MAISHA NI MAPAMBANO,KILA SIKU NI MAPAMBANO.

Kila siku za maisha yetu tunapitia mapambano mbali mbali na changamoto mbali mbali.
Likiisha hili unahisi utakaa kwa raha lakini baadae litakuja lingine.Changamoto kwenye kazi kawaida huwa tunaita matatizo mie natumia neno changamoto.Kama sio kwenye kazi basi kwenye,biashara,nyumbani,kwenye mahusiano yako,kwa majirani,marafiki,watoto,pesa,jamiii yaani likiisha hili baada ya muda linakuja hili.

Usitarajie utakaa kwa starehe mwenyewe ndio maana kila jambo lina kinyume chake.Raha karaha,tabasamu kinyume chake huzuni,kicheko kinyume chake kilio n.k

Napenda ni kwambie vyovyote iwavyo lazima maisha yaendelee.Maisha hayatakiwi kusimama.Tatizo linapojitokeza usipaparike ukatapatapa TULIA.Tuliza akili tafakari na uweze kuona vyema namna utakavyojitoa kwenye tatizo husika.Ukipaparika utashindwa kuona vyema na badala ya kutatua tatizo ukaongeza tatizo.

Pia kubwa angalia CHANZO cha tatizo husika ni nini ili usolve ukijua unasolve nini?tatizo la aina gani
Kwa sababu ya wahaka na roho kuwa juu na maumivu ya tatizo husika unakuta unakuwa na huzuni,hasira,uchungu, ambao unaweza kuzidisha na kuzalisha tatizo jipya hata ukija kutaka kutatua tatizo chanzo hukioni kwa sababu tayari umejijazia matatizo.

Hakuna hali ya kudumu kuwa na imani,kuwa mvumilivu na mwenye subira.Usikae chini ukasema yaani jamani kila siku mimi tu mimi tu matatizo yananiandama kila mtu ana mapambano yake na anapambana nayo kivyake.Usikae chini ukajihurumia simama.

Wakati mwingine matatizo na changamoto ukiyatazama vizuri yanaweza kuwa fursa.Sio yote inategemea ni tatizo gani.

Litambue tatizo,usipaparike stay calm,acha mawazo na akili yako yawe chanya ili uweze kuona vyema na kutafakari vyema.Kuwa kwenye control sio tatizo ndio likucontrol wewe.

*Haya ni mawazo yangu kama mdau unaweza kujazilizia mtazamo wako pindi tunapopitia changamoto mbali mbali za kimaisha tufanyeje?*

*wewe hufanyaje nyakazi za matatizo na changamoto?*

*Hapo siongelei Msiba au kifo.

Na Dina Marios.

NI WAJIBU WAKO KAMA MZAZI KUMJENGEA MTOTO WAKO KUJIAMINI.

Huwa nasoma sana website inaitwa woman of christ nilikutana na huu ujumbe nikapenda kushare nanyi.Hasa wazazi itawafaa katika malezi.

Mzazi ni wajibu wako kuwapenda watoto wako wote, kuwafundisha njia ipasayo, kuwatia moyo wanapopitia magumu, na kuhakikisha unakuwa mstari wa mbele kuwajengea self esteem imara. Mzazi hupaswi kuwa critic wa mtoto wako, hiyo sio kazi yako. Muongoze katika kweli, mfundishe, muadhibu pale anapokosea na chunga sana usimuadhibu ili kumuaibisha bali kumsaidia. Adhabu ya kumsaidia mtoto unampa kwa kujali utu wake na sio mbele ya kadamnasi na kumuaibisha.
Watoto hawalingani, usifanye kosa la kuwalinganisha watoto, iwe ni watoto wako wote au kumlinganisha wako na wa jirani. Tambua kila mwanadamu ameumbwa tofauti, jitahidi kumfahamu mwanao na kumsaidia kuwa bora kwa jinsi Mungu alivyomuumba ukiangalia zaidi strengths zake kuliko mapungufu. Kosa ambalo wazazi wengi wanafanya ni kuwabagua watoto kulingana na uwezo wao kwa yale ambayo yanaonekana mema katika jamii mfano kumpenda zaidi mtoto anayejituma kuwahi kuamka na kumbeza yule anayependa kulala tena mbele za wengine. Ndio, kila mtoto lazima afuate utaratibu lakini usitumie kigezo hiki kupimia upendo, badala ya kumsaidia utakuwa unampoteza kabisa.

Mtoto anayeona anabaguliwa nyumbani atajenga kiburi na ataanza kuwachukia wenzie wanaopendwa zaidi na itampelekea kutafuta upendo nje kwa watu wasiofaa na kujikuta katika matatizo makubwa. Chunga sana maneno unayomwambia mtoto wako, maneno yanaumiza kwa muda mrefu, yanaua kujiamini na yanaumba. Mtamkie maneno ya baraka, tumaini na hata pale unapomuonya maneno yako yasiwe ya kumdhalilisha mfano hujui kitu kabisa, sijui wewe ni mtoto wa aina gani, hufai kabisa n.k. Maneno ya aina hiyo hayafai kabisa maana hayajengi bali yanamuondolea kujiamini na kumfanya ajione hana thamani

Wednesday, 18 December 2013

RICH MAVOKO ALIZWA NA STORY YA MAMA SHARO MILIONEA.

Na Shakoor Jongo

STORI kuhusu maisha ya mama mzazi wa staa wa komedi Bongo, marehemu Husein Mkiety ‘Sharo Milionea’, baada ya kifo cha mwanaye huyo imemliza Rich Mavoko ambaye alikwenda kumtembelea nyumbani kwake kijijini Lusanga, Muheza mkoani Tanga.
Rich Mavoko akifuta machozi alipomtembelea Mama Sharo Milionea.
Akiteta machache na Risasi Vibes, Mavoko alisema, yeye kama msanii aliguswa kwenda kumsalimia mama Sharo kwa kuwa wote ni wasanii na aliona mama huyo anahitaji faraja kutoka kwa watu waliokuwa karibu na mwanaye.
“Mama alifurahi sana kuniona. Tulizungumza mengi lakini niliguswa sana na matatizo aliyonayo mama yetu. Mama anasema, mali nyingi za marehemu mwanaye, amekuwa akizisikia tu lakini hajapewa.
Mavoko na Mama Sharo wakiwa katika kaburi la Marehemu Sharo Milionea.
“Kiukweli mama Sharo anatia huruma sana kwani faraja imepotea, mali za mwanaye hazioni, amebaki akitia huruma.
Unajua marehemu alikuwa akimsadia sana mama yake, ndiyo lilikuwa tegemeo lake kubwa. Ameondoka na kumuacha akiwa hana la kufanya, mbaya zaidi hata mali zake ambazo zingepaswa kumsaidia kipindi hiki, wajanja wamezidhulumu.
“Dunia haina usawa kabisa. Kiukweli inatia huruma sana. Nawasihi wasanii wenzangu na wadau wa sanaa, inatakiwa tukumbuke wenzetu waliotangulia tena kwa kuwaenzi kwa kila njia.
Marehemu Sharo Milionea enzi za uhai wake.
Kuna vitu vinauma sana amenieleza tangu kifo cha mwanaye haki zake nyingi hajui zilipo. Tuungane wasanii tuwasaidie wazazi wa wasanii wanaotangulia mbele za haki,” alisema Mavoko.RICH

Thursday, 12 December 2013

AJALI MBAYA YATOKEA BASI LA BURUDANI LIKITOKEA KOROGWE KUELEKEA JIJINI DAR,WATU ZAIDI YA 12 WAHOFIWA KUFARIKI NA MAJERUHI ZAIDI YA 50.

Basi la Burudani baada ya ajali leo Wilaya ya Handeni, Tanga.
Basi la Burudani leo limepata ajali kijiji cha Taula Wilaya ya Handeni, Imeripotiwa mpaka sasa watu zaidi ya 12 wamefariki na majeruhi zaidi ya 55. Watu 4 wamepelekwa MOI na KCMC. Tuwaombee majeruhi.
Hospitali ya wilaya ya Korogwe.
Majeruhi wakipatiwa matibabu.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo ( kushoto) akiangalia mmoja wa majeruhi akipatiwa matibabu.
Manesi wakiendelea na matibabu kwa majeruhi.
Mmoja wa majeruhi akiwa amelazwa kwenye benchi.
Wananchi wakiwa eneo la Hospitali.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA MKUU WA WILAYA YA KOROGWE, MRISHO GAMBO.

Thursday, 5 December 2013

Mjue Rose Ndauka

Rose Ndauka
Anafahamika zaidi kama Rose Ndauka ni mmoja warembo wenye mvuto wa pekee ndani ya tasnia ya bongo movies kwa vipaji vyake vingi sana. Licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuigiza pia rose ni mwandishi na mwongozaji wa Filamu. Akiwa ameshaigiza kwenye zaidi ya Filamu kumi na saba (17) na kupata tuzo mbalimbali ikiwemo ya best actress in mini ziff 2011; Rose Pia ni mfanyabishara na anamiliki kampuni yake binafsi iitwayo Ndauka Entertainment inayojihusha na mambo ya Filamu na burudani. Rose Hupenda kusikiliza muziki, kuogelea, na  kusoma vitabu akiwa yupo nyumbani

Early life

Historia ya Rose inaanza tarehe saba (7) mwezi wa kumi (10) mwaka 1989. Huu ni mwaka tarehe na siku alipozaliwa. Alizaliwa hapa hapa Tanzania na kupata elimu yake katika shule ya sekondari zanaki- Dar es salaam alipomaliza mnamo mwaka 2008. Toka alipokuwa mdogo sana Rose alipenda kuigiza. Na kipaji chake Kiligunduliwa na mama yake mzazi kabla ya yeye mwenyewe kuamua kujiingiza rasmi kwenye tasnia ya Filamu nchini.

Career

Rose alionekana kwa mara ya kwanza kwenye Filamu ya “SWAHIBA” aliyoigiza kama “Aisha” mnamo mwaka 2007. Filamu hii ilipigiwa kura kama Filamu bora ya mwaka na kituo cha redio cha clouds FM. Baada ya Filamu hiyo Rose aliweza kupata nafasi ya kuigiza katika Filamu mbalimbali zikiwemo Mahabuba na na Solemba na nyota yake ilionekana sana pale alipoigiza Filamu ya Deception na marehemu Steven Kanumba kama mmoja wa waigizaji wakuu pamoja na Lost Adam aliyoigiza na mkali mwingine wa bongo movies Jacob steven “JB”
Mwaka 2010 Rose Ndauka alifungua kampuni yake mwenyewe ya “Ndauka Entertainment”  na pia alipata nafasi ya kuigiza kwenye Filamu inayohusu mauaji ya halaiki ya Rwanda iliyopewa jina la “RWANDA BAADA YA VITA” ama (URWANDA NYUMA U’GENOCIDE)  kwa kirwanda.
Mwaka huo huo chin ya kampuni yake Rose alitoa filamu mbili za “BAD GIRL” na “THE DIARY” ambazo zilifanya vizuri sana sokoni.
Mashabiki wake wanapenda kuita “Rosie” na mara nyingi amekuwa akipata “attention” kubwa kwenye vyombo vya habari na magazeti kutokana na mvuto wake na umbo lake zuri.

Friday, 8 November 2013

MKE AUWAWA KIKATILI NA MWILI KUFICHWA STOO


 Ni kifo cha kusikikisha cha mwanamke huyo pichaniHamida Urembo na muhusika wa mauaji hayo ni mumewe wa ndoa waliyeishi kwa miaka mitatu.Hamida alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu na mwaka watatu na alikuwa anatarajia kugraduate mwezi huu chuoni hapo.
Hamida na mumewe yahaya walibahatika kupata mtoto wa kike mwenye miaka mitatu sasa.Kwa mujibu wa dada wa Hamida ndoa yao ilikuwa ya misuko suko sana.Mume alikuwa sio mwaminifu mara nyingi alikuwa akizini nje.Ukiacha hilo alikuwa akimpiga sana mkewe mpaka kumzimisha.
Matatizo ambayo ndugu walikuwa wakiyajua na walishasuluhisha mara nyingi na Hamida kurudi kwa mume kuendelea na maisha.Hii ya mwisho ndio ilikuwa kubwa zaidi.Mume alikuwa akimtongoza housegirl hapo nyumbani na alipokuwa kesho housegirl akamfahamisha mama.
Akamueleza jinsi gani muwewe amekuwa akimsumbua kumtaka kimapenzi.Hamida akamwambia anataka tu uthibitisho kama ni kweli.Siku ya siku Yahaya akamlazimisha Hamida kwenda kwao na Hamida akakubali akijua kuna jambo.Akasindikizana na mumewe mpaka kituoni mume akijua mkewe hayupo kumbe mke aligeuzia njiani akarudi nyumbani akajificha chini ya uvungu chumbani kwa housegirl wake.Baadae mume akawasilia na housegirl kuwa anarudi nyumbani,aliporudi akaendelea kuomba mambo tena akavua nguo kabisa akabaki na boxer.Wakati huo yupo chumbani kwao na mkewe.Housegirl akamwambia wahamie chumbani kwako hapo sio salama.Basi wakahamia chumbani na akawa ndio anamuinamisha dada ili amfanye Hamida akatoka chini ya uvungu ili kumuokoa dada na kumuonyesha mumewe kuwa alikuwepo na amejua usaliti wake.Na alipokuwa chini ya uvungu alikuwa akirekodi kila kitu kwenye simu na alipotoka na picha akapiga.
Yahaya mume wa Hamida pichani
 
Hamida alitoka hapo akashitaki kwao na kwao wakamwambia aende kwa mjomba wa mumewe kumueleza matatizo ya mtoto wao.Alipofika kwa mjomba akaambiwa wanaume ndivyo walivyo avumilie tu arudi kwa mumewe.
Hamida akarudii kwao akiwa hana hana raha lakini uamuzi aliouchukua ni kuachana na mumewe kwani alikuwa kashachoka.
Wakawa wakivutana sana mume akimsihi arudi nyumbani walikokuwa wakiishi Mbagala ila Hamida hakuridhia.
Story ya Hamida ni ndefu sana hapa naipeleka huku nikiruka ruka.
Hamida alishaenda mpaka Bakwata ili mumewe aamriwe kutoa talaka.
Mwisho wa Hamida kuonekana nyumbani ni siku ambayo yeye na ndugu zake walikuwa waende kijijini kwao kwenye viwanja walivyopewa na babu yao.Ila siku hiyo Hamida alitoa udhuru kuwa haendi na akamtaarifu mama yake kuwa Yahaya kamuita akachukue vitu vyake vilivyobakia.Mama akamkatalia kwenda akamwambia kuna kaka zake wakubwa aache wataenda kuvifata kwani huyo mume ni mshenzi anaweza kumfanyia kitu kibaya.Hamida akamwambia mama anataka kwenda mwenyewe kwani kuna vyeti vyake muhimu akavichukue.
Basi mama akamuacha aende kishingo upande lakini mama akamwambia basi nenda hata na mdogo wako.Akaenda na mdogo wake lakini kufika kule mume akamkatalia mdogo mtu kuingia ndani.
Wakabishana sana kwa nini asiingie mdogo mtu kuepusha shari akaenda kukaa kwa jirani asubiri kuitwa.Akakaa na muda kupita kukawa kimya akajua wale wameelewana ndio maana hakuna makelele hivyo akaendelea kusubiri.
Akakaa weee mpaka jioni giza lilipoanza kuingia kidogo Yahaya akampigia simu kwa kutumia simu ya Hamida akimwambia aondoke tu arudi nyumbani wao wameshaondoka na vyombo wamebeba.
Mdogo mtu akaondoka kurudi nyumbani kwao Tabata akijua mke na mume wameelewana kumbe dada yake ameshakufa ndani.
Mdogo mtu akafika nyumbani saa mbili usiku na kumwambia mama jinsi Hamida alivyomuudhi kamuacha yeye kwa jirani na akaondoka na mumewe Yahaya.Mama machale yakamcheza akanyanyua simu akampigia Yahaya kumuuliza mwane yupo wapi.Yahaya akamjibu kuwa ameachana nae kitambo mama akamwambia sio kweli mwanangu hawezi kuchelewa kurudi nyumbani na hana kawaida hiyo.Yahaya akamjibu atarudi tu Hamida mtu mzima.
Mamam tayari alishajua kuna jambo akampigia simu baba Hamida aliyekuwa Arusha kumtaarifu kilichotokea.Baba Hamida akampigia Yahaya lakini hakupokea simu.Wasiwasi ukazidi kutanda na ndugu kupeana taarifa zaidi.Asubuhi kulipokucha wakaenda Mbagala kwa Yahaya lakini wakatoa taarifa polisi.Polisi wakawaondoa wasiwasi kwamba hao wanajuana wenyewe labda wameamua kukumbushiana.
Ndugu hawakuridhika wakaenda kwa mjumbe awaruhusu wavunje nyumba waingie ndani pengine kamfungia ndani maana ilikuwa kawaida yake kufanya hivyo kumfungia Hamida ndani.Basi mjumbe akaruhusu mlango uvunjwe walipoingia ndani palikuwa patupu hawakuona kitu wala dalili za mauaji.Kuna chumba ambacho ni stoo hicho walishindwa kufungua na mjumbe akawaambia hiyo ni stoo wanawekaga mavitu yamejazana humo basi wakakiacha wakaondoka.
Hawakuishia hapo bado waliendelea kumsaka Hamida bila mafanikio.
Hamida alipotea toka jumapili iliyopita,jumanne juzi kila mtu wakapanga kila mtu akamtafute popote pale anapoona anaweza kumpata.Mama akaenda kwenye maombi kanisani wakati muislam,dada akaenda blue pearl kazini kwa Yahaya na huku majirani Mbagala wakaanza kuona inzi na harufu kali ikitoka nyumbani kwa Yahaya.Ikabidi mjumbe apige simu kwa mama Hamida kumueleza kinachoendelea polisi wakaitwa,nyumba ikavunjwa ili kutafuta harufu inatokea wapi.Wakavunja kile chumba cha stoo na kukuta mwili wa Hamida umeshaanza kuharibika.Kanyongwa na kamba ya katani na kitenge kafungwa puani na mdomoni.Mwili wake ukawekwa kwenye mfuko akajaziwa mito na manguo nguo na tendegu la kitanda kawekewa shingoni.
Ndugu,polisi wakachukuwa mwili kwa ajili ya msiba na mazishi wakati huo Yahaya alishakimbia siku nyingi hajulikani alipo.
Hamida alizikwa jana kule kwa babu yake Mzenga uzaramuni walipokuwa waende  kwenye mashamba waliyopewa.Msiba upo nyumbani kwao Tabata.Na ameacha mtoto wa kike wa miaka mitatu anaitwa Tayana.
Habari hii tumeianza kusikiliza leo inaendelea tena kesho katika heka heka za leo ndani ya leo tena ya clouds fm.

Monday, 21 October 2013

BABA AUZA NYUMBA MTOTO AKIWEMO NDANI NA KUTOKOMEA :HUU NI UKATILI MKUBWA

 

“ Nilikuwa nimelala  ndani ambapo nilipoamka asubuhi nilikuta mlango umefungwa kwa nje hata hivyo nilivumilia hadi njaa ilipoanza kuniuma baada ya siku tano nikaanza kupiga kelele ndipomajirani walipokuja kunifungulia na kuniambia nyumba imeuzwa” alisema mtoto Erasto Emmanuel.  

Groli Emmanuel (9) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Hatwelo alisema siku akiwa anaondoka aliagwa na baba yake ambaye alimwachia shilingi 3000 lakini hakumwambia kama nyumba imeuzwa.
Hii ndiyo nyumba iliyouzwa mtoto akiwa ndani
Mwandishi wa Mbeya yetu  akizungumza na mwenyekiti wa kijiji cha Hatwelo Ibrahim Mponzi katikati akiwa  na barozi juu ya uuzwaji nyumba hiyo

Mwanaharakati wa haki za Binadamu, Yasin Yuta, alisema majirani waligundua baada ya kusikia kelele za mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Erasto Emmanuel (11) aliyekuwa amefungiwa ndani na kukaa kwa siku tano.


 
VITENDO vya ukatili dhidi ya watoto vimeendelea kushika kasi katika baadhi ya maeneo hususani vijijini, licha ya Serikali na asasi mbali mbali kulipigia kelele ambapo hivi karibuni Baba mmoja aliamua kuuza nyumba ikiwa na watoto ndani na kutokomea kusikojulikana na kuwaacha wasijue la kufanya.
 
Mkasa huo wa ajabu ulitokea katika kijiji cha Hatwelo, Kata ya Ijombe Mbeya Vijijini ambapo Mkazi huyo aliyefahamika kwa jina la Emmanuel Yuta alipouza nyumba yake na kutokomea yeye na mkewe na kuwaacha watoto wawili wenye umri kati ya miaka 9 na 11 wakikosa mahala pa kuishi.
 
Akizungumzia sakata hilo kijijini hapo, Mwanaharakati wa haki za Binadamu, Yasin Yuta, alisema majirani waligundua baada ya kusikia kelele za mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Erasto Emmanuel (11) aliyekuwa amefungiwa ndani na kukaa kwa siku tano.
 
Alisema baada ya kumfungulia mtoto huyo ndipo ilipobainika kuwa nyumba hiyo ilikuwa imeshauzwa huku mtoto akiwa ndani na ndipo mnunuzi alipofunga na kufuli bila kujua kama kuna mtoto ndani huku watoto wengine wakiwa kwa ndugu zao ambao pia hawakuelezwa kama nyumba imeuzwa.
 
Nyumba hiyo iliuzwa kwa Dati Nsagaje kwa gharama ya shilingi 750,000/= ikiwa ni nyumba mbili pamoja na kiwanja ambapo mnunuzi huyo alilipa kianzio cha shilingi laki nne biashara iliyofanyika tangu April 26 mwaka huu  na kiasi kilichobaki wakiwa wameahidiana kulipana Mwezi Mei 15, Mwaka huu.
 
Wahanga wa tukio hilo ambao ni watoto walisema hawakuwa na taarifa zozote za kuuzwa kwa nyumba wanayokaa ambapo walisikia kuwa baba yao ameenda Sumbawanga kumfuata  mke wake ambaye inasemekana aliolewa na mwanaume mwingine.
 
“ Nilikuwa nimelala  ndani ambapo nilipoamka asubuhi nilikuta mlango umefungwa kwa nje hata hivyo nilivumilia hadi njaa ilipoanza kuniuma baada ya siku tano nikaanza kupiga kelele ndipomajirani walipokuja kunifungulia na kuniambia nyumba imeuzwa” alisema mtoto Erasto Emmanuel.  
 
Mtoto mwingine aliyetelekezwa ambaye siku ya tukio alikuwa ameenda kulala kwa bibi yake Groli Emmanuel (9) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Hatwelo alisema siku akiwa anaondoka aliagwa na baba yake ambaye alimwachia shilingi 3000 lakini hakumwambia kama nyumba imeuzwa.
Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida na kuonesha kukosa uwajibikaji kwa baadhi ya viongozi wa Serikali ya Kijiji ambao walishiriki moja kwa moja zoezi hilo huku wakiwa wamesaini kama mashahidi na kugonga mhuri wa Serikali ya Kijiji walipoulizwa kuhusiana na sakata hilo hawakuwa na majibu ya kuridhisha.
 
Mwenyekiti wa Kijiji cha Hatwelo, Ibrahimu Mponzi, alisema kitendo alichokifanya muuzaji ni cha kawaida kwa sababu ameuza mali yake mwenyewe na kwamba wao kama majirani na serikali ya kijiji hawawezi kuhoji atakako waacha watoto kwa sababu ni mipangilio ya maisha ya kila mtu.
 
Mbali na mwenyekiti wa Kijiji kuwa shahidi wa upande wa mnunuaji akiwa sambamba na watu wengine wanne akiwepo Mkewe ambaye pia ni Balozi wa nyumba kumi pia waliosaini wengine ni ndugu wa mnunuaji ili hali muuzaji akiwa hana shahidi hata mmoja.
NA Mbeya yetu

Monday, 14 October 2013

KUMBUKUMBU YA MAISHA YA MWL NYERERE; ANGALIA HAPA

 

nyerere
 
Tukiwa tunakumbuka na kusherekea maisha ya Baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere, unaweza kuangalia hii documentary inayohusu maisha ya mwalimu kuanzia alipozaliwa hadi alipoanza harakati za siasa. Siku kama ya leo natumaini mtu wangu wa nguvu haya yatakuwa material mazuri kwa ajili yako, enjoy.



Use Facebook to Comment on this Post

Saturday, 12 October 2013

One woman's startlingly frank admission about becoming a parent 'I love my son, but being a mother bores me'

     Last week I was flicking through old photographs of myself and came across one in which I looked young, happy and carefree.
I had no frown lines, no bags beneath my eyes but, more importantly, there was a tangible feeling of freedom that emanated from that photo, a feeling that said: I’m free and anything is possible.
I then looked at myself in the mirror to compare the photo to my current reflection and shuddered. But I then realised when that photo had been taken. ‘B.A.’ Before Alex.
Just the three of us: Julie with her husband Cornel and their little boy Alex
Just the three of us: Julie with her husband Cornel and their little boy Alex

I LOVE THIS: KIM KARDASHIAN STEP OUT IN CURVES REVEALING GRAY DRESS.

 


Kim Kardashian stepped out to the family store on Oct. 11 in a gray dress that showed she's still up tight. Remember she did a pre-birth workout before the arrival of North West. I guess it really worked! 

MTOTO ANYONGWA NA HOUSE GIRL NA MAITI YAKE KUTUPWA KWENYE DIMBWI LA MAJI MACHAFU HUKO KIBAHA

 


NI ukatili uliopitiliza! Hausigeli aliyejulikana kwa jina moja la Ester (14) yupo matatani kwa madai ya kumuua mtoto Arafat Allan (3) kwa kumnyonga shingo na kumpiga na kitu kizito kichwani kisha kuutumbukiza mwili wake kwenye dimbwi la maji machafu, Risasi Jumamosi limekamata tukio zima.

Tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita Mailimoja, Kibaha mkoani Pwani ambako marehemu alikuwa akiishi na wazazi wake.
Akizungumza kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo, ZakiaPeter ambaye amelazwa katika Zahanati ya Kellen kutokana na mshtuko wa kifo cha mwanaye, alisema siku ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa na siku mbili tangu aanze kazi aling’ang’ania kutumwa sokoni saa mbili asubuhi ambapo alimkubalia na kumuagiza mboga.
 

 

AONDOKA NA MTOTO

Bila mwanamke huyo kujua, msichana huyo alimpitia Arafat kwa jirani alikokuwa akicheza na wenzake na kuondoka naye kwa madai anamsindikiza.
Nilipoona muda unasonga mbele bila hausigeli kurudi na mtoto nilianza kuwatafuta,” alisema mama wa marehemu.
Akasema aliwatafuta kwa muda mrefu bila mafanikio mwishowe yeye na majirani zake wakaenda kutoa taarifa polisi na kufunguliwa jalada la kesi KB/RB/1154/2013 TAARIFA.
HABARI ZASAMBAA MAITI YA MTOTO KUONEKANA KWENYE DIMBWI LA MAJI
Mama wa marehemu aliendelea kusema kuwa zoezi la kumsaka msichana huyo na mtoto wake liliendelea mpaka Jumanne iliyopita ambapo habari zilisambaa kwamba kuna maiti ya mtoto wa kiume  imekutwa ikielea kwenye dimbwi la maji machafu linalotumika kumwagilia bustani za mboga maeneo hayo.
Niliondoka na ndugu wengine hadi kwenye dimbwi hilo! Nilipata mshtuko mkubwa kukuta maiti ya mtoto anayeelea ni ya mwanangu Arafat,” alisema huku machozi yakimtoka.
 
MADAKTARI WAANIKA RIPOTI YA UCHUNGUZI
Baada ya hapo, mwili huo ulipelekwa katika Hospitali Teule ya Tumbi, Kibaha ambapo madaktari waliufanyia uchunguzi na kubaini kuwa marehemu alinyongwa shingo na kupigwa na kitu kizito kichwani hali iliyomsababishia mauti.