TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Showing posts with label Burudani. Show all posts
Showing posts with label Burudani. Show all posts

Monday, 27 October 2014

MSANII LULU AITAMBULISHA FILAMU YAKE MPYA IITWAYO MAPENZI YA MUNGU LEO.FILAMU YAINGIA SOKONI LEO

 Msanii wa Sanaa ya Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Alipokuwa akiitambulisha filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU ambayo amewashirikisha Flora Mtegoha au Mama Kanumba na Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Linah Sanga.
 Msanii Wa Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiitambulisha filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU leo mbele ya wanahabari (hawapo pichani).,Kulia ni Mmoja kati wa wasanii walioshiriki katika filamu hiyo ajulikanae kama Flora Mtegoha almaarufu kama Mama Kanumba
Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Ltd, Evance Stephen akiongea na wanahabari leo katika Ofisi za Proin Promotions Ltd zilizopo Mikocheni mtaa wa Ursino wakati wa Utambulisho wa Filamu mpya ya Lulu Iitwayo MAPENZI YA MUNGU.

Msanii Elizabeth Michael aka Lulu leo ametambulisha Filamu yake Mpya ambayo imeingia sokoni leo iitwayo MAPENZI YA MUNGU, huku akiwa amemshirikisha Msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga na Mama Kanumba.

Wakati akiilezea filamu hiyo leo mbele ya wanahabari Lulu amesema Kuwa Ni Filamu inayofundisha na Kutoa somo kwa mtu yoyote yule ambae yupo hapa duniani kwa kuendelea kuonyesha kuwa MUNGU YUPO. Akiongezea kuwa…”Sisi kama binadamu tumekuwa tukifanya mambo mengi sana hapa Duniani na kupelekea kumsahau Mungu na pengine kuendelea kufikiria kuwa yote tuyafanyayo ni kwa uwezo wetu kumbe Sio uwezo wetu na Ni Mapenzi ya Mungu tu ndio yanayofanya sisi kufikia hapa tulipo leo”

Filamu ya MAPENZI YA MUNGU imekuwa gumzo kabla ya kutoka kutokana na watanzania wengi kuwa na shauku ya Kutaka kumuona Lulu tena mara baada ya Kuonekana  katika Filamu Zake Mbili zilizotangulia za FOOLISH AGE na FAMILY CURSE. Sasa Lulu kuonekana tena katika kiwango cha Juu katika Filamu hii Mpya ambayo imeingia Sokoni Leo.

Filamu ya MAPENZI YA MUNGU ni filamu inayosambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd.

Friday, 21 February 2014

PATA NAKALA YAKO PIGA NO.0784670746


Kutana na producer chipkizi Hilda Ngaja, kwenye movie iitwayo ( He Hurts me ) ambayo iko sokoni tayari. Pata nakala yako bila kukosa, pia unaweza letewa ulipo kwa kupiga no 0784670746 au wasiliana nasi kupitia ukurasa  wetu wa  facebook www.nkema.blogspot.com.

post by

Nkema

Thursday, 5 December 2013

YAMKUTA WEMA

Stori: Imelda Mtema na Richard Bukos
KICHEKO! Ile kesi ya kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni Meneja wa Hoteli ya Mediteranian iliyopo Kawe Beach, Dar, Godlucky Kayombo iliyokuwa ikimkabili Wema Isaac Sepetu imetolewa hukumu yake kama ilivyokuwa ile ya shosti’ake, Kajala Masanja.
Wema Sepetu akitinga Mahakama ya Mwanzo ya Kawe, Dar.
Habari kutoka kwa chanzo makini cha gazeti hili kilieleza kuwa Wema alihukumiwa kifungo cha miezi mitatu au faini ya shilingi laki moja kwa maana ya elfu hamsini kwa kila kosa baada ya kukutwa na hatia ya kutenda makosa hayo mawili ya kupiga na…

Sunday, 1 December 2013

EMMANUEL MSUYA ALAMBA MILIONI 50 ZA EBSS


Kinyanganyiro cha kumtafuta Super Star wa Bongo kupitia Epiq Bongo Star Search 2013 kimekamilika alfajiri hii kwenye ukumbi wa Escape 1.
Mashindano haya ambayo kidogo yalichelewa kuanza yalipambwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Barnaba,Makomando,Young Killer,water chilambo,Shaa,Kimbunga na Snura. 
Katika round ya mwisho,Emmanuel Msuya ameibuka kidedea na kuwa Mshindi wa Epiq Bongo Star Search 2013,akiwa ni mshiriki anaetokea Jijini Mwanza na kumpokea taji water chilambo ambae alikua mshindi wa mwaka jana
Zawadi kwa mshindi wa mwaka huu ni Milion hamsini[50]ambayo kakabidhiwa jukwaani.

Katika mashindano haya ambayo yalikua na jumla ya washiriki watano ambao ni Amina Chibaba,Elizabeth Mwakijambile,Emmanuel Msuya,Maina Thadei na Melisa John,ambao walipita kwa round tatu kisha majaji kuwapunguza watatu na kisha kubakia Emanuel Msuya na Elizabeth Mwakijambile katika Round ya 4 na ya mwisho. 

MSHINDI WA MISS TANZANIA USA PAGEANT NI JOY KALEMERA


 Mlimbwende Joy Kalemera akipungia mashabiki baada ya kushinda mashindano ya Miss Tanzania USA Pageant yaliyofanyika usiku wa Jumamosi Novemba 30, 2013 kwenye ukumbi wa Hollywood Ballroom uliopo Silver Spring , Maryland na Mhe. Balozi Liberata Mulamula ndiye aliyekua mgeni rasmi. Joy Kalemera alipohojiwa na Vijimambo alikua na haya ya kusema.
 Mshindi wa Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalamera akipewa maua na aliyekua Miss District of Columbia baada ya kutangazwa mshindi kwenye Miss Tanzania USA Pageant ambapo mashindano haya ya kumtafuta Miss Tanzania USA Pageant ndiyo ya kwanza kufanyika kwenye ardhi ya Marekani. 
 Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera akiwa mwenye furaha baada ya kutangazwa mshinidi wa Miss Tanzania USA Pageant.
 Balozi wa Tnzania nchini Marekani na Mexico akimvisha taji Joy Kalemera baada ya kutangazwa mshindi wa Miss Tanzania Pageant
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa mwenye furaha baada ya shindano hili kufana sana na kuandika historia iliyobeba ukurasa mpya wa kutangaza Tanzania kwenye mashindano haya ya Miss Afrika USA Pageant ambayo Tanzania ilikua na mshiriki wa kwanza mwaka huu ambae ushiriki wake haukupitia ngazi hii.
Joy Kalemera akipongezwa na washiriki wenzake waliokua nae kwenye kinyang'anyiro hiki kilichoanzia miezi miwili iliyopita.
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa kwanza katika historia ya Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera kulia ni Mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Tanzania USA Pageant Ma Winny Casey.
 Joy Kalemera katika picha ya pamoja na majaji pamoja na mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA Pageant, Lady Kate (kulia)
 Kutoka kushoto ni Faith Kashaa kutoka Alabama ambaye ndiye mshindi wa tatu, Doreen Rumaya kutoka Pennsylvania mshindi wa pili, Joy Kalemera kutoka New Jersey Miss Tanzania USA Pageant, Julia Nyerere mshindi wa Tano na Namala Elias mshindi wa nne wakiwa kwenye picha ya pamoja
 Miss Tanzania USA Pageant katika picha ya pamoja na washiriki wenzake.

Saturday, 9 November 2013

USIKU WA KHANGA ZA KALE WAFANYIKA NA MAMA ASHA BILAL ASHEREHESHA JIJINI DAR .


 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti Miss Tanzania 2012,Brigitte Alfred, kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha sherehe za Usiku wa Khanga, zilizofanyika jana usiku Novemba 8, 2013 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mratibu wa Hafla hiyo,Asia Idarus.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti mwakilishi wa Micuzi Media Group, Othman Michuzi, kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha sherehe za Usiku wa Khanga, zilizofanyika jana usiku katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mratibu wa Hafla hiyo,Asia Idarus. 
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti Mkurigenzi wa Gazeti la Jambo Leo,Benny Kisaka, kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha sherehe za Usiku wa Khanga, zilizofanyika jana usiku katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mratibu wa Hafla hiyo,Asia Idarus. 

Tuesday, 29 October 2013

HATIMAYE JAMII PRODUCTION YAZINDULIWA RASMI


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara alipokuwa akisisitiza jambo wakati wa mahojiano mafupi aliyofanya na Jamii Production kabla ya KUZINDUA RASMI shughuli za kutayarisha na kusambaza matangazo ya Radio na Video.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiwa na waanzilishi wa Jamii Production, Mubelwa Bandio (kulia) na Abou Shatry (kushoto)

Naam....
Kwa baraka za Mhe. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt
Fenella Mukangara, JAMII RASMI IMEZINDULIWA RASMI Oktoba 26, 2013, alipotutembelea kuangalia utendaji wetu na kuizindua rasmi hapa ofisini
kwetu Washington DC.
Hii ilikuwa ni ZAIDI YA TUKIO.
Ilikuwa ni BARAKA KWETU na tunamshukuru kila aliyewezesha hili.
NA SASA.....
Kazi ya kutekeleza yale yaliyousiwa na Mhe Waziri, yaliyo yaliyo msingi
wa kituo chetu, yale yaliyo MAHITAJI ya walaji (hadhira yetu) NA WAJIBU
WA FANI YETU ndio imeanza.
Na......
Hakuna litajalokuwa na maana kama hatutajua namna ambavyo utendaji wetu unaathiri maisha yako kwa namna CHANYA na HASI
Wewe (msikilizaji, mtazamaji na msomaji wetu) ni mdau mkubwa wa kufanikisha hili. Tuzidi kushirikiana TWAWAPENDA
Msimamizi wa vipindi na mpigapicha mkuu wa Jamii Production Abou Shatry akisisitiza jambo kabla ya kuwasili kwa mgeni rasmi
Mtayarishaji na Mtangazaji wa kipindi cha FAMILIA Georgina Lema akiwa "kitini"

Mmoja wa wawezeshaji wakuu wa Jamii Production Bwn Isidory Lyamuya wa Prestige Health Services akijaribu vitendea kazi vya kituo.
Mhe. Waziri Mukangara akipokea maelezo ya utendaji wa kituo. Kushoto ni Afisa Ubalozi Mindi Kasiga

 Mhe. Waziri akisikiliza RISALA ya Jamii Production
 Mhe. Waziri Mukangara akijibu risala ya Jamii Production
Bwn Isidory Lyamuya akipata akipata picha ya pamoja na Mhe. Waziri kwa msaada anaotoa kufanikisha kazi za Jamii Production
Bwn Isidory Lyamuya akipata mkono wa pongezi toka kwa Mhe. Waziri kwa msaada anaotoa kufanikisha kazi za Jamii Production
Abou Shatry akipongezwa na Mhe Waziri Mukangara
 "Mwanamama" Georgina Lema wa kipindi cha FAMILIA akipata kumbukumbu na Mhe. Waziri
  Mkurugenzi wa Mambo Jambo Radio Bwn Julius Makiri ambaye aliungana nasi katika uzinduzi huu rasmi akipata kumbukumbu na Mhe. Waziri
 Mhe. Waziri Dkt Fenella Mukangara na Afisa Habari katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mindi Kasiga pamoja na wanaJAMII
 
Hakuna ZAWADI kubwa sawa na kilichofanyika. Na zawadi pekee tuliyonayo ni UPENDO. Ambao hauonyesheki wala haupimiki.

Lakini....tunapenda POPOTE UWAPO, UKUMBUKE SIKU YA LEO.
Na hivyo..twaomba KIKOMBE hiki kiwe kumbukumbu ya tukio hili kubwa kwetu
Abou Shatry akiwa mahala anapopatawala zaidi...

Monday, 28 October 2013

FILAMU YA "FIGO" KUTOKA PROIN PROMOTIONS KUINGIA SOKONI MUDA WOWOTE KUANZIA SASA

 

 
Kampuni ya utengenezaji,uuzaji na usambazaji wa filamu za kitanzania ya Proin Promotions Limited inatarajia kuingiza movie yake nyingine sokoni mapema wiki hii. Filamu ya "FIGO" ni filamu ya kitanzania ambayo imechezwa na waigizaji wakongwe katika tasnia ya filamu nchini na Ni filamu ambayo inasimimua,kufundisha na kuelemisha, Filamu ya Figo ni moja kati ya filamu ya Kitanzania ambayo imechezwa kwa ustadi wa hali ya juu na kutengenezwa kwa hali ya juu na kampuni Mahiri ya Utengenezaji na Uuzaji wa Filamu Tanzania ya Proin Promotions Limited 

Proin Promotions ni moja ya kampuni kubwa ya utengenezaji,uuzaji na usambazaji wa filamu Tanzania ambayo tayari ishaingiza Sokoni Filamu Mbili ambazo zinafanya Vizuri kama vile Foolish Age, Long Time na sasa inakuletea Filamu ya FIGO ambayo imechezwa na Jennifer Kyaka ambaye anafahamika kama Odama, Irene Uwoya, Rachel Haule, Stanley Msungu na wengineo wengi.

Filamu ya "FIGO" inatarajia kuingia sokoni muda wowote kuanzia sasa ambapo itapatikana katika maduka yote ya Uuzaji wa filamu na Kwa mawakala Wao Nchini Nzima, Vilevile Unaweza kununua filamu hiyo ya figo kupitia Ukurasa wa facebook wa Proin Promotions Limited Kupitia https://www.facebook.com/proinpromotions na kupitia pia tovuti yao ya http://www.proinpromotions.com

Tuesday, 22 October 2013

SINGER/ ACTRESS BABY MADAHA AZINDUA RASMI PERFUME NA MIFUKO YENYE NEMBO NA PICHA YAKE (PHOTOS)

Baby Madaha ambaye ni actress wa Swahiliwood na pia muimbaji wa bongofleva ambaye hivi karibuni alisainishwa mkataba nchini Kenya na kampuni ya Candy n Candy Records amepiga hatua zaidi kwa kuzindua perfume na mifuko yenye nembo na jina lake ambyo imeanza kuuzwa rasmi nchini Kenya ambako ana mashabiki wengi. Baby Madaha ambaye kwasasa anatamba na nyimbo za Squeeze It na Summer Holiday alisema kuwa perfume na mifuko hiyo itaingia Tanzania pia muda si mrefu. Hongera sana Baby Madaha kwa kutanua wigo wako wa kujiongezea kipato. Angalia baadhi ya picha wakenya wakiwa na bidhaa hizo za Madaha


Monday, 21 October 2013

WARIDI :TUNAIGA SANA UZUNGU KATIKA FILAMU ZETU MPAKA AIBU

Muigizaji wa siku nyingi Anna Costantine maarufu kama Waridi ambaye alitamba sana mwishoni mwa miaka ya tisini amesema kuwa maadili ya kitanzania na kiafrika yameshuka sana katika filamu zetu mpaka ni aibu kutokana na kuiga sana uzungu ambao hata wazungu wenyewe hawafanyi hasa kwa waigizaji wa kike. Akizungumza na Mwananchi Waridi alisema "maadili yameshuka, hatuendani na maadili ya mwafrika, wanaiga sana umagharibi, tunaiga mpaka inakuwa aibu, hata wazungu hawafanyi hivyo"

Waridi ambaye alitamba enzi hizo na kina Monalisa, JB, Bishanga na Aisha alipoulizwa kuwa anategemea kurudi lini katika filamu alisema "mwanzoni mwa mwaka ujao nitarejea, nimejipanga vilivyo, ni lazima nifanye vizuri, nina kipaji, nimesomea kazi hii(chuo cha sanaa Bagamoyo), pia nina karama ya uigizaji, nitarudi kwa kasi, nitatingisha kama awali"

                                                            
 
Waridi
 

Saturday, 19 October 2013

SIKILIZA CLOSER TO ME REMIX - VANESA MDEE FT MAX

 

Vannesa Mdee akishirikiana na Max katika ngoma hii ya Closer to Me remix kitu kilichotengenezwa na Herm B. Isikilize hapo Chini au Ipakue(Download)

Thursday, 17 October 2013

ROCK CITY MARATHON 2013, ZAIDI YA WANARIADHA 2000 KUSHIRIKI


 

ZAIDI ya wanariadha 2000 wanatarajia kushiriki mbio za mwaka huu, za awamu ya tano za Rock City, zitakazofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza mwezi Oktoba tarehe 27, kamati ya maandilizi imesema.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa kamati ya maandilizi ya mbio za Rock City mwaka huu, Bw. Mathew Kasonta alisema mwenendo wa usajili unaonyesha matumaini makubwa na kuongeza kuwa inatarajiwa kushika kasi zaidi katika wiki hii ya mwisho ambapo washiriki wanategemewa kuongezeka kufikia 2000 kwa mwaka huu.  

“Tunayo faraja kubwa kuona usajili unaendelea vizuri. Watu wengi wameshajitokeza kujisajili na kuchukua fomu wenyewe, na wengine wameshalipia fomu zao kupitia Airtel Money. Japokuwa usajili unaendelea, kwa mpaka jana, takwimu niliyo nayo inaonyesha kuwa wale waliochukua fomu zao wamefikia washiriki 531, wakati wengi waliotumia Airtel Money kulipia watachukua fomu zao wakati wowote kupitia vituo vifuatavyo; 

Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam, Maduka ya Airtel Dodoma, Arusha, Mwanza, Zanzibar na Mbeya,” alisema. Mratibu wa mbio hizo alisema usajili bado unaendelea na fomu zinapatikana katika ofisi za kampuni ya Capital Plus International jijini Dar es Salaam, viwanja vya Nyamagana mkoani Mwanza na ofisi zote za michezo za wilaya mkoani Mwanza.

Kasonta alibainisha kuwa wanariadha kutoka nje wameonyesha nia yao ya kushiriki kwa kutuma maombi yao kupitia Chama cha Riadha Tanzania (RT) – ambacho kitahakikisha washiriki wote wa kutoka nje wanafuata taratibu zote za kisheria kabla ya kushiriki.

“Tumeshapata simu kutoka kwa washiriki kutoka nchi kama Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC), pamoja na washiriki ambao ni raia wa Australia, India, Canada na Amerika, wanaotaka kushiriki mbio hizi. Sababu tunafanyakazi kwa ukaribu na RT, tumeamua kuwa RT watahakikisha washiriki kutoka nje wanafuata taratibu zote kabla ya kushiriki ili kuifanya Rock City Marathon ifikie viwango vilivyowekwa kimataifa,” alisema Kasonta. Mbali na washiriki ambao tayari wamechukua fomu zao, Kasonta alisema makampuni mbali mbali, wafanyabiara, taasisi na watu maarufu wamethibitisha kuleta timu zao ili kushiriki mbio za kilometa 5 ambazo ni maalum kwa wafanyakazi.

Mratibu alisema kupitia udhamini wa NSSF, Africa Barrick Gold (ABG), Precision Air, Airtel kupitia Airtel Money, Bank M, PPF, Nyanza Bottling Ltd, New Mwanza Hotel, Sahara Communications, Continental Decoders na Umoja Switch, kamati imeboresha zawadi zitakazoshindaniwa na kualika kikundi cha Sanaa cha Bujora kitakachokuwepo kunogesha tukio hilo.

“Rock City Marathon ambayo kwa miaka mitano sasa imekuwa ikiandaliwa na kampuni ya Capital Plus International Ltd, kwa miaka mingi imekuwa ikibeba kauli mbiu ya “Tukuze utalii wa ndani kupitia michezo.” Kwa kutambua hilo, katika mbio za mwaka huu, tutaburudishwa na kikundi cha Sanaa cha Bujora ambacho kimeonyesha kuwa kikundi bora zaidi kwa kuonyesha utamaduni wa kitanzania kupitia dansi,” alisema.

Mbio za mwaka huu zinavipengele vitano ambavyo ni kilometa 21 kwa wanaume na wanawake, kilometa 5 kwa wafanyakazi kutoka katika makampuni, kilometa 3 kwa watu wenye ulemavu wa ngozi, kilometa 3 kwa wazee kuanzia miaka 55 na zaidi na kilometa 2 kwa watoto kuanzia umri wa 7 mpaka 10.

LULU;SIPO TAYARI KUOLEWA KWASASA


Star mkubwa Swahiliwood Elizabeth Michael(Lulu) amesema kuwa hayupo tayari kuolewa kwasasa kwa kuwa muda bado na ukifika atafanya hivyo. Akizungumza katika show ya Mkasi inayorushwa East Africa Tv Lulu alisema "sitaki kuolewa kwasasa, muda wa kuolewa haujafika, ukifika nitafanya hivyo lakini kwasasa sipo tayari kuolewa"