Mkurugenzi wa Shule za St Mary’s, mama Getrude Lwakatare akizungumza na wanafunzi wa Shule za St Mary’s International za Dar es Salaam wakati akizundua tamasha la kuonyesha vipaji vya wanafunzi wa Shule za St Mary’s International za Dar es Salaam lililofanyika Novemba 15, 2014 jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
Mwalimu wa Shule ya St Mary’s International, Eric Sendi akiwaasa wanafunzi waandelee kuonyesha vipaji vyao.mm
Mkurugenzi wa Shule za St Mary’s, mama Getrude Lwakatare (kushoto), akikabidhiwa baadhi ya Peni na Meneja Masoko wa Kampuni ya SILAFRICA, Salman Pathan kama mchango wake kwaajiliya shule za St Mary’s International.
Wanafunzi kutoka shule za St Mary’s International za Dar es Salaam wakiwa kwenye tamasha hilo.
Wanafunzi kutoka shule za St Mary’s International za Dar es Salaam wakitoa burudani wakati wa tamasha la kuonyesha vipaji.
Tamasha Hilo lililoshirikisha Shule za Mbagala, Tabata na Mbezi Junior lililenga kuonyesha vipaji vya wanafunzi katika sanaa ya kucheza, kuimba na sarakasi.
Akizungumza wakati wa kuzindua tamasha Hilo,Mkurugenzi wa Shule za St Mary’s, Mheshimiwa Mama Getrude Lwakatare, Alisema ukuzaji wa vipaji Ni sehemu muhimu ya Shule za St Mary’s International.
‘Leo Ni Siku muhimu kwetu sisi kama St Mary’s Kwani pamoja na elimu bora tunayoitoa, Lakini pia tunasisitiza umuhimu wa vipaji Kwa wanafunzi wetu ‘ Alisema Mheshimiwa Mama Lwakatare.
Tamasha Hilo Ambalo limeandaliwa Kwa kushirikiana na Tanzania House of Talent, limedhaminiwa na Simtank ambao wametoa peni pamoja na tenki moja.
No comments:
Post a Comment