Mwenyekiti wa Tanzania Business
Entrepreneurs for Women, Haika Lawere akizungumza na Waandishi wa
Habari wakati wa Kongamano hilo lililofanyika Hoteli ya Mbezi Guarden
Dar es Salaam.
Wadau wa kongamano hilo wakiwa
wamejipanga kisawasawa. Kutoka Kulia ni Getrude Kilyabusebu, Haika
Lawere, Hilda Mgaja na Julieth Mjale.
Mwezeshaji wa Kongamano hilo, James Mwang'amba
akitoa mada.
Muwezeshaji wa kongamano hilo, Chriss
Rupia (kulia), akitoa maelezo juu ya namna ya kuanzisha Kampuni na hatua
mbalimbali ambazo mtu anatakiwa azifuata wakati wa kufungua kampuni
hasa binafsi.
Mwenyekiti wa Tanzania Business
Entrepreneurs for Women Haika Lawere (wa kwanza kulia) pamoja na wadau
wengine wakiangalia bidhaa mbalimbali wakati wa kongamano hilo.
Mmoja wa majaji akiangalia bidhaa
mbalimbali zilizopangwa kwenye meza zilizotokana na ubunifu wa wanawake
waliohudhuria kongamano hilo.
Baadhi ya wajasiriamali na wadau mbalimbali wakiwa katika Kongamano hilo.
Mmoja wa waratibu wa kongamano hilo
Getrude Kilyabusebu (Kulia) akiweka sawa kumbukumbu ya wadau waliofika
katika kongamano hilo.
Bidhaa mbalimbali zikioneshwa. |
Maonyesho ya bidhaa mbalimbali yakiendelea. |
Baadhi ya wajasiriamali wakionesha kazi zao.
Wadau mbalimbali wakitizama bidhaa mbalimbali katika Kongamano hilo. Na Dotto Mwaibale
WAJASIRIAMALI wanawake nchini wametakiwa kuwa na moyo wa uthubutu ili kupiga hatua ya maisha na kiuchumi badala ya kuwa waoga.
Mwito huo umetolewa na Mratibu wa Kongamano la Jumuia ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania, Julieti Mjale wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kongamano hilo lililofanyika Hoteli ya Mbezi Garden Dar es Salaam jana.
"Uthubutu katika jambo lolote ni muhimu kwani unamfanya muhusika kupiga hatua ya maendeleo" alisema Mjale
Alisema wajasiriamali waliowengi wamekuwa na mipango mizuri ya kubuni biashara fulani lakini wanakuwa na hofu ya kupoteza fedha zao na hiyo inatokana na kushindwa kuthubutu au kuchukua maamuzi magumu ya kuanza kufanya biashara waliyoikusudia.
Akijitolea mfano yeye alisema alithubutu kwa kuanza kufanya biashara za chini lakini leo hii ana nyumba za kupangisha na kufikia hatua ya kufanya biashara za kwenda nje ya nchi na kuandaa makongamana ya namna hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya biashara.
Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Haika Lawere alisema lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wajasiriamali wanawake ili kupeana uzoefu wa biashara na kujua changamoto walizonazo na kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kupanua wigo wa shughuli zao na kutafuta masoko mapya ya bidhaa zao.
Katibu wa Jumuia hiyo, Hilda Ngaja, alisema changamoto kubwa waliyonayo wajasiriamali wanawake ni kutokuwa na uelewa mkubwa wa kufanyabiashara zao na kujikuta wakirudi nyuma kimaendeleo na ndio maana wamekuwa wakitumia fursa za semina na makongamano kwa ajili ya kuelimishana.
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba-0712-727062)
No comments:
Post a Comment