TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Thursday, 20 November 2014

MISS HONDURAS, DADA YAKE WAKUTWA WAMEUAWA


 
Miss Honduras, Maria Jose Alvarado (kulia) akiwa na dada yake Sofia Trinidad enzi za uhai wao.


Miss Honduras, Maria Jose Alvarado aliyekuwa anatarajia kushiriki Miss World jijini London.GPL(P.T)


Mpenzi wa Sofia, Plutarco Antonio Ruiz akiwa mikononi mwa polisi.
MISS Honduras, Maria Jose Alvarado, 19, na dada yake Sofia Trinidad, 23, wamekutwa wamekufa baada ya kupotea tangu Alhamisi iliyopita.
Warembo hao walipotea Alhamis iliyopita ya Novemba 13, mwaka huu mara baada ya kutoka kwenye sherehe ya bethidei katika Mkoa wa Santa Barbara.
Maria Jose Alvarado ni miongoni mwa warembo waliokuwa wanatarajiwa kushiriki mashindano ya Miss World jijini London.
Watu wanne akiwemo mpenzi wa Sofia aitwaye Plutarco Antonio Ruiz wanashikiliwa na polisi kusaidia uchunguzi.
Miili ya wawilihao imekutwa katika Kijiji cha Cablotales village, karibu na Mto Aguagua imeelezwa.

No comments:

Post a Comment