Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Rasilimaliwatu Lusius Mwenda kutoka Wizara ya Nishati na Madini akifunga awamu ya kwanza ya mafunzo ya jinsi ya kuandaa mapendekezo ya miradi, sera pamoja na utekelezaji wake yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Bagamoyo. Mafunzo hayo yalishirikisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi (TDGC)
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungaji wa mafunzo hayo iliyokuwa inatolewa na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Rasilimaliwatu Lusius Mwenda (hayupo pichani)
Afisa Rasilimali watu kutoka Idara ya Utawala Judith Ntyangiri akipokea cheti cha ushiriki mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo
Mwishoni mwa wiki Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Lusius Mwenda, alifunga awamu ya kwanza ya mafunzo ya jinsi ya kuandaa mapendekezo ya miradi, sera pamoja na utekelezaji wake yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Bagamoyo.
Mafunzo hayo yalishirikisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi (TDGC). Pamoja na kufunga mafunzo hayo, alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa washiriki na kuwataka kuboresha tathmini ya mapendekezo ya miradi ( project proposals)
Ninawasilisha kwenu habari pamoja na picha za matukio ambazo zimeambatishwa pamoja na email hii. Pia captions zimeambatishwa
No comments:
Post a Comment