Mwakilishi kutoka Kitengo cha Taifa cha Kudhibiti Ukimwi (NACP), Dk. Anath Rwebembera.
Makamu wa Rais wa EGPAF, Anja Giphart (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi wa EGPAF Tanzania, Dk. Chrispine Kimaro na Mwakilishi kutoka Kitengo cha Taifa cha Kudhibiti Ukimwi (NACP), Dk. Anath Rwebembera.
Mwakilishi kutoka Kitengo cha Taifa cha Kudhibiti Ukimwi (NACP), Dk. Anath Rwebembera (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Kongamano la nne la Taifa la Watoto na VVU na Ukimwi litakalofanyika leo Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Kutoka kushoto ni Mratibu wa Mawasiliano wa Shirika la Huduma za Watoto la Elizabeth Glaser Pediatric Foundation (EGPAF), Tanzania, Mercy Nyanda na Makamu wa Rais wa EGPAF, Anja Giphart.
Mkurugenzi wa Ufundi wa EGPAF Tanzania, Dk. Chrispine Kimaro (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Mratibu wa Mawasiliano wa Shirika la Huduma za Watoto la Elizabeth Glaser Pediatric Foundation (EGPAF), Tanzania, Mercy Nyanda (kushoto), akitambulisha meza kuu kwa wanahabari.
Mratibu wa Mawasiliano wa Shirika la Huduma za Watoto la Elizabeth Glaser Pediatric Foundation (EGPAF), Tanzania, Mercy Nyanda.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Dotto Mwaibale
ASILIMIA 26 ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanaohitaji matibabu ya dawa za kurefusha maisha (ARV's) baada ya kuathirika na virusi vya Ukimwi hawapati huduma hiyo.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirika la Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation (EGPF), Chrispine Kimario alitoa kauli hiyo Dar es Salaam leo wakati akitoa taarifa ya Kongamano la Nne la Watoto na Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Alisema kongamano hilo lina kaulimbiu inayosema 'Kuongeza Kasi Kuimarisha Upatikanaji wa Huduma Vipimo Matunzo na Tiba ya VVU ili Kuboresha Maisha ya Mtoto', ambapoasilimia 7.6 ya watoto walioathirika na virusi hivyo ndiyo wanaopata matibabu.
"Hapa nchini watoto wengi wamekuwa wakiugua ugonjwa wa Ukimwi kutoka kwa mama pindi tu wanapozaliwa na hiyo ndiyo inasababisha ongezeko la watoto wenye virusi," alisema.
Alisema kongamano litasaidia watu kupanga mipango mkakati wa kupambana na tatizo hilo.
Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Aneth Lubembere alisema uzingatiaji mkuu utakuwa katika malengo mapya yaliyotangazwa ya agenda ya dunia mwaka 2015.
"Agenda hizo ni asilimia 90 ya watu waliopimwa, asilimia 90 ya watu wanaoishi na VVU na walio katika matibabu na asilimia 90 ya watu wanaoendelea kwenye huduma na matunzo na tiba ya kupunguza kabisa virusi," alisema. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)