TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Friday, 29 November 2013

IN DAR TODAY,ALLIANCE AUTOS LAUNCHES NEW VOLKSWAGEN (TOUAREG)




DSC_0170
The Charge d’ Affaires from the Embassy of the Federal Republic of Germany, Hans Koeppel speaks to invited guests and reporters (not in picture) during the official handing over ceremony of the New Model Volkswagen Touareg held at Umoja House premises in Dar.(All photos by Zainul Mzige).

.Germany Embassy in Dar has chosen TOUAREG has it’s official car

By Damas Makangale, MOblog
THE Embassy of the Federal Republic of Germany has launch the new model of the Volkswagen TOUAREG sport utility vehicles as part of the Embassy’s mobility fleet. It has been established.

Speaking to invited dignitaries during the official handover ceremony at Umoja House in Dar es Salaam, the Charge d’ Affaires from the Embassy of the Federal Republic of Germany, Hans Koeppel said that Volkswagen is one of the largest automobile company in the world, in Tanzania and underlined that German products are known worldwide for high class technology and innovative engineering.

UZINDUZI WA ‘KIOTA’ KIPYA CHA CLUB TIFFANY KUPAMBWA NA ASIA IDOROUS


Na Mwandishi Wetu
WADAU mbali mbali wa burudani  na mitindo nchini ususani wa jijini Dar es Salaam,  wanatarajia kushuhudia shoo kali ya onesho la mavazi kwenye uzinduzi wa  ‘kiota’ kipya cha burudani cha Club Tiffany.

Uzinduzi huo unatarajia kufanyika Usiku wa Ijumaa Novemba 29,  ndani ya  hoteli ya  kisasa ya Tiffany Diamond , iliyopo katikati ya jiji la Dar e Salaam Mitaa ya Morogoro na Indira Gandi huku kiingilio kiasi cha sh. 10,000.

Akizungumzia  kupamba shoo hiyo, Asia Idorous, alisema tayari warembo wake wamejifua vya kutosha kuonesha mavazi mavazi mapya nay a kisasa ndani ya Club hiyo.

“Mamodols wamejipanga kuonesha shoo ya pekee na ya aina yake kwenye uzinduzi huo, hivyo wadau wa burudani na mitindo watafurahia shoo hiyo naomba wajitokeze kwa wingi” Alisema Asia Idorous. Na kuongeza kuwa,  mbali na shoo hiyo, pia kutakuwa na utambulisho wa Tanzania Top Model, watakaoongozwa na mshindi wa Mr. Dar 2013.

Ukumbi huo wa kisasa upo ndani ya hoteli hiyo ya Tiffany Diamond,  kwenye ghorofa ya 10, ambapo umejengwa kwa mtindo wa kisasa na kuwa ukumbi wa kipee kwa Tanzania.

Wednesday, 27 November 2013

WAANDAA TAMASHA JIJINI ARUSHA,TAKUKURU KWA KUSHIRIKIANA WADAU WA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA



DSC_0043
Afisa Mtendaji Mkuu wa Megamark Ltd. Chedi Ngulu (kulia) akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Bodi ya ushauri wa Umoja wa Afrika ya kupambana na Rushwa yaani African Union Advisory Board on Corruption (AUABC) na Tamasha la wasanii lenye lengo la kufikisha ujumbe juu ya Madhara ya Rushwa kwenye Jamii, Kati kati ni Emmanuel Atenga toka (AUABC) na Stephane Ndilimbaye toka AUABC.

Na.Mwandishi wetu
TAASISI YA KUPAMBANA NA KUZUIA RUSHWA (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Bodi ya Ushauri wa Umoja wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Rushwa (AUABC) na Megamark Ltd wameandaa tamasha kubwa litakalowashirikisha wasanii mbali mbali toka Tanzania, Kenya na Uganda katika kuadhimisha miaka 10 tangu bodi hiyo ya Afrika katika maswala ya Rushwa kuanzishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Takukuru jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Megamark ltd, Chedi Ngulu amesema kuwa lengo la tamasha hilo ni kufikisha ujumbe kwa umma juu ya kupambana na Rushwa na kuelezea madhara ya Rushwa kwenye jamii na nchi kwa ujumla.
DSC_0063
DSC_0075
Bw. Emmanuel Atenga (wa pili kushoto) kutoka na Bodi ya Ushauri wa Umoja wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Rushwa (AUABC) akizungumza na waandishi wa habari juu ya Tamasha hilo litakalofanyika tarehe 7 mwezi ujao katika viwanja vya General Tyre Arusha. Kulia ni mmoja wa wasanii wataoimba kwenye Tamasha hilo Fid Q na wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Megamark Ltd. Chedi Ngulu na kushoto ni Stephane Ndilimbaye kutoka AUABC.
“Muziki upo katika asili ya waafrika na umekuwa ukitumika kuburudisha lakini zaidi kufikisha ujumbe wenye kujenga na kurekebisha jamii (Hadhira) iwe ni nyimbo, kughani ambayo tunatambua kwa njia ya Rap na ngoma za asili, lakini tumechagua muziki kama njia rahisi ya kufikisha ujumbe hasa kwa vijana kuhusu madhara ya Rushwa,” amesema Ngulu.
Amesema kuwa katika tamasha hilo nyimbo mbalimbali zitaimbwa katika kuelezea matatizo ya Rushwa kwenye jamii na hasa kuelimisha vijana umuhimu wa kukataa Rushwa kwa sababu vijana ndio nguvu kazi ya taifa na asilimia 75 ya watu nchini ni vijana.
“kwa mantiki hii, tumeandaa onyesho lenye anuani isemayo “Rushwa sio” ikimaanisha rushwa haina manufaa na ni yenye kutakiwa kupigwa vita kwa gharama yoyote ile,”
DSC_0095
Msanii Fid Q akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha hilo.
“Onyesho hili litafanyika Arusha tarehe 7 mwezi wa kumi na mbili katika viwanja vya General Tyre kuanzia saa saba na nusu mpaka saa kumi na mbili jioni na litahusisha wasanii wenye kukubalika na jamii,” alisisitiza

Kwa upande wake, Emmanuel Atenga toka Kitengo cha Mawasiliano (AUABC) amesema Board hiyo ya Umoja wa Afrika ya kupambana na rushwa imepata mafanikio kwa kuanzisha vitengo vya ufatiliaji kwa wanachama wa Umoja wa Afrika wenye lengo la kusaidiana katika mapambano dhidi ya Rushwa.

Amesema mapambano dhidi ya rushwa Afrika yanahitaji nguvu ya pamoja kwa ksuhirikisha jamii wakiwemo wasanii katika kuhamasisha mapambano ya kukataa Rushwa kwenye ngazi zote ndani ya nchi na bara zima la Afrika.
DSC_0036
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe akiuliza swali wakati wa mkutano huo.
DSC_0039
Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.
DSC_0059

Tuesday, 26 November 2013

TUSKER PROJECT FAME WATANZANIA WAOMBWA KUMPIGIA KURA HISIA



Mshiriki pekee aliyebaki katika mashindano ya kusaka vipaji Afrika Mashariki kutoka Tanzania Elisha Maghiya(Hisia) akiwa katika jukwaa la Tusker Project Fame msimu wa sita nchini Kenya.
 Mshiriki wa Tusker Project Fame msimu wa sita kutoka Tanzania Hisia(katikati) akiwa na washiriki wenzake katika gari la kifahari wakifurahia jambo kulia kwake ni Amosi kutoka Kenyana Kojjo kutoka Uganda na kushoto kwake ni Nyambura kutoka Kenya na Daisy kutoka Uganda.
  Hisia kutoka Tanzania(kulia) na Kojjo kutoka Uganda wakiwa katika picha ya pamoja

WARSHA YA FURSA JIJINI DAR LEO,RAIS KIKWETE AWAASA VIJANA KUJITUMA KUFANYA KAZI


 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Wadau mbali mbali walioshiriki kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.Mh. Rais ameupongeza uongozi wa Kampuni ya Clouds Media Group kwa ubunifu wao wa Kampeni ya Fusra inayowakutanisha na kuwahamasisha vijana mbali mbali nchini kujituma na kufanya kazi ili kutokomeza swala zima la ukosefu wa ajira,Pia Rais Kikwete ameahidi kuwasaidia waendeshaji wa Warsha hiyo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi,Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,ili aweze kuzungumza na Wadau mbali mbali walioshiriki kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi,Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,ili aweze kuzungumza na Wadau mbali mbali walioshiriki kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa,Ahmed Lussasi akizunguma katika Warsha ya Fursa namba alivyo

the Diabetes Pandemic Addressing

Addressing the Diabetes Pandemic

     Over a century ago, Dr. Elliot P. Joslin, believed that the key to managing diabetes lay with patient involvement, education, and empowerment. Even before the discovery of insulin in 1922, Dr. Joslin foresaw the astounding epidemic of diabetes and the fact that if patients controlled their diabetes well, they could live longer, more meaningful lives. We’ve seen the number of patients with type 2 diabetes (which accounts for more than 90% of the cases of diabetes) rapidly increase in both developed and developing countries.  This epidemic is caused to a large extent by obesity and physical inactivity., In the United States alone, 25.8 million children and adults—8.3% of the population—currently have diabetes and another 79 million have pre-diabetes (CDC, 2011).  More than 360 million people worldwide have diabetes and this number is expected to exceed 550 million by 2030.  And what’s more another 418 million people will have impaired glucose intolerance (also commonly referred to as pre-diabetes). In addition to the adverse physical and emotional effects associated with this chronic disease, its economic costs are staggering.  In 2012 in the USA the costs attributed to diabetes were $ 245 billion—by 2030 the global economic burden is expected to reach $490 billion.

Monday, 25 November 2013

Ajifumua kwa risasi kama shinikizo ili mke aliyemtaliki amrudie


MFANYABIASHARA maarufu mjini Tabora, Hakimu Hamdun, mkazi wa Kata ya Kanyenye anashikiliwa Polisi akituhumiwa kujaribu kujiua kwa kujipiga risasi kutokana na wivu wa mapenzi.
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Kamishna Msaidizi, Peter Ouma, alisema jana kuwa Hamdun alijaribu kujiua kwa risasi wiki iliyopita saa kumi na mbili jioni nyumbani kwake eneo la Kanyenye mjini hapa. 
Alisema kuwa Hamdun ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa Kitete kwa matibabu, alijipiga risasi baada ya mkewe aliyempa talaka mbili, kumtaka afuate utaratibu wa ndoa ili warudiane.
Inadaiwa Hamdun alimpa talaka mbili mkewe huyo, Joha binti Sudi, lakini baadaye alibadilisha mawazo na kumtaka warudiane huku akimtishia kumuua kama asipokubali.
Kwa mujibu wa madai ya Kamanda Ouma, wanandoa hao waliotalikiana walikuwa wanaishi nyumba tofauti na Hamdun aliamua kumfuata mkewe alipokuwa akiishi akiwa na gari lake na kumtaka warudiane. Hata hivyo, alidai mkewe huyo alikataa kurudiana kienyeji na kumtaka Hamdun kama kweli anampenda, afuate utaratibu wa Dini ya Kiislamu ndipo watimize azma yao hiyo ya kurudiana.
Utaratibu Utaratibu huo kwa mujibu wa dini ya Kiislamu, talaka moja na mbili zinaitwa talaka rejea, ambapo mume aliyotoa talaka hizo, anapaswa kumpa chumba mkewe pale pale nyumbani wanakoishi na chakula kwa miezi mitatu (eda). Ndani ya hiyo miezi mitatu, ikiwa watataka kurudiana, mume huyo ataruhusiwa kwenda katika chumba cha mkewe na kumtaja kwa jina lake na kutamka nimeamua kukurejea. Kwa taratibu za imani ya Kiislamu, mke hatakiwi kukataa na hilo linapofanyika halihitaji shahidi wala shehe. Ikiwa mke atapewa talaka tatu, atakaa eda akila na kuhudumiwa kila kitu mpaka miezi mitatu iishe, ambapo mwanamke atasafiri kurudi kwao. Kama mume atataka kumrejea, mke huyo atapaswa kuolewa kwanza, aachike ndipo utaratibu wa kufunga naye ndoa uanze. 
Badala ya kufuata utaratibu, inadaiwa Hamdun alienda kwenye gari lake na kuchukua bunduki aina ya Shot gun na kwenda nyumbani kwake ambapo alifunga milango, akajipiga risasi katika ubavu wa kushoto.
Kwa mujibu wa Kamada Ouma, mtuhumiwa huyo hali yake inaendelea vizuri lakini amepoteza sifa ya kumiliki bunduki na hivyo hatapewa tena. 
Aidha, Hamdun atakapomaliza matibabu atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yake ikiwemo ya kutishia kuua na jaribio la kutaka kujiua. --- 
HabariLeo


MKE ACHINJWA KISA WIVU WA MAPENZI


Gervas Kadaga akiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya baada ya kujeruhiwa na kisu tumboni baada ya kumuua kwa kumchoma kisu mkewe

MWANAMKE mkazi  wa kijiji cha Mahango kata ya Madibila wilayani Mbarali mkoani Mbeya aliyefahamika kwa jina la Jitihada  Mamga(20) ameuawa kwa kuchomwa kisu na mumewe aliyefahamika kwa jina Gervas Kadaga(25) ambaye pia ni mkazi wa kijijini hapo.

Tukio hilo limetokea juzi Novemba 21 majira ya saa 1:00 jioni baada ya kutokea ugomvi baina ya wapenzi hao ambapo marehemu alikutwa na majeraha tisa ya kisu katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Bw. Diwani Athumani alisema kuwa marehemu alifia nyumbani kwake ambapo mtuhumiwa ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya naye amejeruhiwa kwa kuchomwa na kisu tumboni.

Hata hivyo Kamanda Athumani alisema kuwa hadi sasa hakijafahamika chanzo halisi cha ugomvi huo ambapo Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo huku mtuhumiwa akiwa amewekwa chini ya ulinzi wa polisi katika hospitali ya rufaa ya Mbeya alikolazwa.

Tukio la aina hiyo ni  la pili kwa kipindi kisichozidi wiki mbili ambapo Novemba 12 mke na mwanawe wa kiume waliotambulika kwa majina ya Husulina Kornel(42)  na mwanaye Kondo Alphonce Chikondo(19) wakazi wa kijiji cha Iseche kata ya Mwambani tarafa ya Kwimba wilayani Chunya walishirikiana  kumuua mumewe aliyefahamika kwa jina la Sylvester Chikondo(55).

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda Athumani ni kwamba mwanamke huyo Husulina Kornel aliyedaiwa kushirikiana na mwanaye kumuua mumewe  mumewe alikamatwa Novemba 20 huko Mwambani Chunya.

Kamanda Athumani alisema kuwa katika mahojiano ya Jeshi la Polisi na mwanamke huyo alidai kuwa alifanya mauaji hayo peke yake bila kumhusisha mwanaye ambaye anaendelea kutafutwa na Jeshi la Polisi.

Aidha alisema kuwa asilimia kubwa ya matukio ya mauaji ya aina hiyo yanatokana na migogoro ya ndoa na wivu wa kimapenzi na kwamba ni vyema wanandoa wakatatua migogoro yao ya ndani kwa njia ya mazungumzo ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea.

Akizungumza katika hospitali ya rufaa alikolazwa mama mkubwa wa Gervas aliyejitambulisha kwa jina la Martha Lugenge alisema kuwa vijana hawa walikutana Madibila kila mmoja akiwa katika shughuli zake ndipo walipoamua kuishi pamoja.

Alisema yeye alipewa taarifa za tukio hilo siku inayofuata na kwamba alipofika alikuta ndugu wa marehemu wameuchukua mwili wa mtoto wao kwa ajili ya taratibu za mazishi na kwamba hajui chanzo cha ugomvi uliosababisha wapigane visu.

Mama huyo alisema kuwa vijana hao hawajawahi kupata mtoto na kwamba hawajaanza kuishi pamoja muda mrefu;  ''Wote  ni watoto, kwani wameanza kuishi muda mrefu? wamekutana kila mmoja akiwa katika kazi zake, ndipo walipoanza kuishi kama mke na mume,''alisema.

Kijana Grevas Kadaga anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma kisu akiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya alikolazwa kwa ajili ya matibabu
Mama mkubwa wa Gervas Martha Lugenge akimjulia hali mwanaye katika hospitali ya Rufaa Mbeya

Gervas Kadaga akiwa katika wodi namba Moja Hospitali ya Rufaa Mbeya

Friday, 22 November 2013

USIKU WA KUAMKIA LEO P-SQUARE WATUA BONGO TAYARI KWA KUTIKISA SHOW JUMAMOSI HII LEADERS CLUB


 Wanamuziki wanaotajwa kuwa na mvuto zaidi barani Afrika, P Square, wamewasili usiku huu katika uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere  kwa ajili ya onesho lao linalotarajiwa kufanyika Jumamosi hii katika viwanja va Leaders Club maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Pichani juu ni Petter(wa pili kutoka kushoto na Paul). Kulia ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ndio wadhamini wakuu wa onesho lao ambalo limeratibiwa na East africa Radio na TV
 Hapa wakifanya mahojiano na kituo cha East Africa TV ambao ndio wenyeji wao
Mahojiano na picha za hapa na pale zikiendelea...
Vijana wakielekea kupumzika tayari kwa kazi

Wednesday, 20 November 2013

Taarifa ya Polisi kwa umma kuhusu matumizi ya silaha zinazomilikiwa kihalali

Picture

Interpol wamtia nguvuni mwenye ghala la vipusa vya ndovu, Polisi Zanzibar

Na Mohammed Mhina, Jeshi la Polisi

Makachero wa Polisi Zanzibar kwa kushirikiana na Makachero wa Interpol, wamemkamata mfanyabiashara wa mjini hapa kwa tuhuma za usafirishaji wa meno ya tembo yaliyokamatwa wiki iliyopita kwenye kontena.

Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alimtaja mfanyabiashara huyo kuwa ni Mohammed Haji Haji Udole (41), mkazi wa Mbuzini mjini hapa.

Alisema mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwa ni mmoja kati ya watu walioshiriki katika kuyapokea, kuyahifadhi na kuyaandaa 
meno hayo kwa ajili ya kusafirishwa.

Kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo kunaifanya idadi ya watuhumiwa waliokwisha kamatwa kufikia sita baada ya wengine watano wakiwamo watumishi wawili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na mmoja wa Mamlaka ya Bandari Zanzibar, kumatwa siku ya pili ya tukio hilo.

Mtuhumiwa Udole, anamiliki ghala kubwa la kuhifadhia mizigo katika eneo la Mbuzini mjini hapa.

Tayari mtuhumiwa Udole naye ameshasafirishwa kwenda Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam kuunganishwa na watuhumiwa wengine watano waliokamatwa.

Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ambao wanaendelewa kuhojiwa na makachero wa Polisi Makao Makuu jijini Dar es Salaam ni Mohammed Suleiman Mussa (45) na Juma Ali Makame (34), ambao ni mawakala wa mizigo kutoka Kampuni ya Island Sea Food ya Zanzibar.

Wengine ni Omari Hamad Ali (50) na Mohammed Hija (48), ambao ni maofisa wa TRA tawi la Zanzibar na Haidar Ahmad Abdallah (54), mfanyakazi wa Bandari ya Zanzibar.

Meno hayo ambayo yalikamatwa Jumatano iliyopita Novemba kwenye Bandari ya Zanzibar, ni vipande 2,023 vyenye uzito wa kilo 2,915 yaliyotokana na kuuawa kwa tembo 305 wenye thamani ya Dola za Marekani 4,775,000 (sawa na Sh. bilioni 7.4).

Vipande hivyo vya meno vilikuwa kwenye magunia 98 yaliyochanganywa na viumbe vya Bahari na kuwekwa kwenye konteina la futi 40 yakiwa tayari kusafirishwa kwa meli ya MV Kota Henning kwenda Ufilipino. --- via blogu ya ZanziNews

MJINI WARSAW, POLAND! RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AHUTUBIA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MABADILIKO YA TABIA NCHI WA COP19/CMP9 MWAKA HUU


















Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano waKimataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nchi wa COP19/CMP9 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Poland, mjini Warsaw. Rais Kikwete alikuwa anazungumza kwa niaba ya viongozi wa Umoja wa Afrika (AU) katika nafasi yake akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi (CAHOSCC).

Rais Kikwete amekuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo tokea Januari, mwaka huu, 2013, wakati alipochaguliwa na viongozi wenzake kushika nafasi hiyo kufuatia kifo cha aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mheshimiwa Meles Zenawi, Septemba, mwaka jana. Picha na Ikulu

DAR-MCHINA ATIWA MBARONI KWA KUKUTWA NA MKONO WA MTU.

Mkono wa mtu uliopatikana kandokando ya Kiwanda cha kutengeneza mifuko ya Viroba na Plastiki, Mababi jijini Dar.

Dada wa kijana anayedaiwa kuwa mwenye mkono huo, Rehema Rashidi akihojiwa na mwandishi wa ITV, Sam Mahela.
Mmiliki wa kiwanda hicho, Lee Sliim, akiwa ndani ya gari la Polisi kuelekea kituoni kwa mahojiano zaidi.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakiendelea kushangaa juu ya tukio hilo.
Bw. Lee Sliim akiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
DUNIA  inaimba sandakarawe! Mwenye kupata sasa anapata na mwenye kukosa hana chake tena! Mwekezaji mmoja wa kiwanda cha Urafiki Plastic Co. Ltd kinachokihusisha na utengenezaji wa mifuko ya viroba na palstiki ambaye ni raia wa China, Lee Slim amekamatwa kwa tuhuma za kuonekana kwa mkono wa mtu karibu na kiwanda chake, tukio hili limetokea mchana huu maeneo ya Mabibo, jijini Dar es salaam. Mkono huiop unadaiwa kuwa ni wa mfanyakazi wa kiwanda hicho, kijana Jumanne Rashid. ( HABARI/PICHA: BRIGHTON MASALU/GPL )

KAMPUNI YA APPLE YAILIPWA DOLA BILIONI MOJA KAMA FIDIA NA SAMSUNG

After a year of scorched-earth litigation, a jury decided Friday Samsung ripped off the innovative technology Apple uses to create its revolutionary iPhone and iPad.

On 29th August, more than 30 trucks filled with 5-cent coins arrived at Apple’s headquarters in California. Initially, the security company that protects the facility said the trucks were in the wrong place, but minutes later, Tim Cook (Apple CEO) received a call from Samsung CEO explaining that they will pay $1 billion dollars for the fine recently ruled against the South Korean company in this way.



The funny part is that the signed document does not specify a single payment method, so Samsung is entitled to send the creators of the iPhone their billion dollars in the way they deem best.



This dirty but genius geek troll play is a new headache to Apple executives as they will need to put in long hours counting all that money, to check if it is all there and to try to deposit it crossing fingers to hope a bank will accept all the coins.
Lee Kun-hee, Chairman of Samsung Electronics, told the media that his company is not going to be intimidated by a group of “geeks with style” and that if they want to play dirty, they also know how to do it.



You can use your coins to buy refreshments at the little machine for life or melt the coins to make computers, that’s not my problem, I already paid them and fulfilled the law.A total of 20 billion coins, delivery hope to finish this week, Samsung said Let’s see how Apple will respond to this.

MAONYESHO YA BIASHARA AFRIKA JIJINI DAR YAFUNGWA LEO NA WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara , Dr Abdallah Kigoda wakati alipofunga maadhimisho ya siku ya Viwanda Afrika kwenye uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Novemba 20, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Bw. Gerge Buchafu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO) baada ya kufunga maadhimisho ya siku ya viwanda Afrika kwenye uwanja wa Maonyesho wa Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Novemba 20, 2013. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dr. Abdallah Kigoda.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu viatu kutoka kwa Elizabeth George (kulia)wakati alipotembelea banda la Woiso Original Products katika maonyesho yaliyoambatana na maadhimisho a siku ya Viwanda Afrika yaliyofaungwa na Waziri Mkuu Novemba 20, 2013 kwenye uwanja wa maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam . Kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashar, Dr. Abdallah Kigoda na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Agness Tegete (kulia) wakati alipotembelea banda la Pani Lihengu Company katika maonyesho yaliyoambatana na maadhimisho a siku ya Viwanda Afrika yaliyofaungwa na Waziri Mkuu Novemba 20, 2013 kwenye uwanja wa maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam . Kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashar, Dr. Abdallah Kigoda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Tuesday, 19 November 2013

DKT SENGONDO MVUNGI AZIKWA MKOANI KILIMANJARO TAZAMA PICHA


Askofu Damian Dallu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita akiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba marehemu Dkt. Sengondo Mvungi katika makaburi ya familia kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18, 2013.
Mke wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba marehemu Dkt. Sengondo Mvungi, Bi. Anna Mvungi akiweka shada la maua katika kaburi la mume wake wakati wa mazishi kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18, 2013.
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi wakati wa mazishi kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro JUmatatu, Novemba 18, 2013.
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi likishushwa kaburini wakati wa mazishi yaliyofanyika kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro JUmatatu, Novemba 18, 2013.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, mkewe Mama Tunu, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba na viongozi wengine wakifuatilia ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi. Mazishi hayo yalifanyika kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro JUmatatu, Novemba 18, 2013.
Familia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi ikifuatilia ibada ya mazishi iliyofanyika katika kijijini cha Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18, 2013.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha Josephat Lobullu (kulia) na Askofu wa Jimbo la Same Rogath Kimaryo wakiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi. Ibada hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chanjale wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro na kuhudhuriwa pia na Askofu Damian Dallu (katikati) wa Jimbo la Geita JUmatatu, Novemba 18, 2013.Picha Kwa Hisani Ya Sufiani Mafoto Blog