TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Wednesday, 20 November 2013

DAR-MCHINA ATIWA MBARONI KWA KUKUTWA NA MKONO WA MTU.

Mkono wa mtu uliopatikana kandokando ya Kiwanda cha kutengeneza mifuko ya Viroba na Plastiki, Mababi jijini Dar.

Dada wa kijana anayedaiwa kuwa mwenye mkono huo, Rehema Rashidi akihojiwa na mwandishi wa ITV, Sam Mahela.
Mmiliki wa kiwanda hicho, Lee Sliim, akiwa ndani ya gari la Polisi kuelekea kituoni kwa mahojiano zaidi.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakiendelea kushangaa juu ya tukio hilo.
Bw. Lee Sliim akiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
DUNIA  inaimba sandakarawe! Mwenye kupata sasa anapata na mwenye kukosa hana chake tena! Mwekezaji mmoja wa kiwanda cha Urafiki Plastic Co. Ltd kinachokihusisha na utengenezaji wa mifuko ya viroba na palstiki ambaye ni raia wa China, Lee Slim amekamatwa kwa tuhuma za kuonekana kwa mkono wa mtu karibu na kiwanda chake, tukio hili limetokea mchana huu maeneo ya Mabibo, jijini Dar es salaam. Mkono huiop unadaiwa kuwa ni wa mfanyakazi wa kiwanda hicho, kijana Jumanne Rashid. ( HABARI/PICHA: BRIGHTON MASALU/GPL )

No comments:

Post a Comment