TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Wednesday, 20 November 2013

MAONYESHO YA BIASHARA AFRIKA JIJINI DAR YAFUNGWA LEO NA WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara , Dr Abdallah Kigoda wakati alipofunga maadhimisho ya siku ya Viwanda Afrika kwenye uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Novemba 20, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Bw. Gerge Buchafu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO) baada ya kufunga maadhimisho ya siku ya viwanda Afrika kwenye uwanja wa Maonyesho wa Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Novemba 20, 2013. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dr. Abdallah Kigoda.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu viatu kutoka kwa Elizabeth George (kulia)wakati alipotembelea banda la Woiso Original Products katika maonyesho yaliyoambatana na maadhimisho a siku ya Viwanda Afrika yaliyofaungwa na Waziri Mkuu Novemba 20, 2013 kwenye uwanja wa maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam . Kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashar, Dr. Abdallah Kigoda na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Agness Tegete (kulia) wakati alipotembelea banda la Pani Lihengu Company katika maonyesho yaliyoambatana na maadhimisho a siku ya Viwanda Afrika yaliyofaungwa na Waziri Mkuu Novemba 20, 2013 kwenye uwanja wa maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam . Kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashar, Dr. Abdallah Kigoda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments:

Post a Comment