TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Sunday, 14 June 2015

INSPIRATIONAL…STRESS LESS

stress-less

Unafanya nini pale ambapo huwa umechukia,hauko kwenye mood au uko disappointed?kuna njia chanya tofauti taofuti ambazo unaweza kufanya ili kurudi kwenye hal yako ya kawaida kwa mfano kuna kufanya mazoezi,kusoma novel,kusikiliza muziki,kucheza(dancing),kuongea na mtu unayemuamini kuhusu tatizo ulilonalo,kutembea kwenye fukwe kwa watu wanaoishi karibu na fukwe na nyingine nyingi.
Kwa upande wangu kabla ya kujua nini nifanye nilikua ni mtu rahisi sana kuchukia ambapo hasira hizo zilikua zinazidisha matatizo zaidi badala ya kunisaidia,hali hiyo binafsi nikawa siifurahii sana basi nikawa najaribu kutafuta msaada kwa kuongea,kusoma articles tofauti tafauti ya jinsi ya kukabiliana na hasira na hata kuongea na mtu ninaye muamini kuhusu shida niliyonayo,kwa kiasi kikubwa vimenisaidia sana.
Lakini nikagundua kitu kingine ambacho kinanisaidia ambacho sijawahi kufikiria kwamba kinaweza kunisaidia,napenda sana kusoma misemo(quotes) nikagundua kwamba kwa kusoma misemo tofauti tofauti najisikia vizuri ni kama nimemwambia mtu what I feel na pale ndipo Napata ushauri,pia naona kama tatizo si la kwangu tu bali la wengi.

No comments:

Post a Comment