IMG_2521
Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakiwa kwenye mazungumzo ya awali na Mkuu wa Shule ya Arusha (Madam Kitigwa) baada ya kuwasili katika shule hiyo kwa lengo la kukutana na Kilabu cha Umoja wa Mataifa shuleni hapo na kuzungumza na Wanafunzi kuhusiana na agenda mbalimbali za Umoja huo.  Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kikishirikiana na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA) wapo katika ziara ya kuzitembelea shule zenye na zisizo na Vilabu vya Umoja huo kwa lengo la kufikisha habari na kazi za Umoja wa Mataifa.
IMG_2563
Afisa Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi-wananchama wa klabu ya Umoja wa Mataifa katika Shule ya Msingi Arusha Medium ambapo amewasisitiza juu ya umuhimu wa kuzifahamu agenda mbalimbali za Umoja Mataifa na nafasi yao katika kuleta maendeleo chanya kwa jamii.
IMG_2602
Mwenyekiti Taifa wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa Tanzania Bara na Visiwani (UNCTN) Bw. Rahim Rajab Nasser akizungumza na vijana wa shule ya msingi Arusha Medium juu ya umuhimu wa vilabu hivyo na umuhimu wa ushiriki wao kuanzia shule za msingi mpaka Sekondari na Vyuoni.
IMG_2629
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama (katikati) akisisitiza jambo kwa vijana wa shule ya msingi Arusha Medium. Kulia ni Mkutubi wa Maktaba ya kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Harriet Macha na  kushoto Mwenyekiti Taifa wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa Tanzania Bara na Visiwani (UNCTN) Bw. Rahim Rajab Nasser.

IMG_2650
Kobe mwenye umri sawa na shule ya Msingi Arusha Medium iliyojengwa mwaka 1930 akiwa hai mpaka na kuwa kivutio kwa wageni mbalimbali wanaofika shuleni hapo ikiwemo Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN).
IMG_2754
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha kuhusiana na umuhimu wa agenda za malengo ya Milenia  (MDG’s) yanayotarajia kufikia tamati 2015 ambapo wao kama vijana wameshauriwa kutilia mkazo utekelezaji wa malengo hayo ikiwemo Usawa wa kijinsia na fursa sawa kwa Wanawake, Upatikanaji wa Huduma bora za uzazi na kupambana na Ukimwi, Malaria na magonjwa mengine.
IMG_2748
Pichani juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha waliobahatika kushiriki mkutano huo ulioendeshwa na Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN).
IMG_2782
IMG_2860
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama akisalimiana na Mkuu wa Shule ya USA Academy Bw. Elibariki Malisa mara baada ya kuwasili shuleni hapo. Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kikishirikiana na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA) wapo katika ziara ya kuzitembelea shule zenye na zisizo na Vilabu vya Umoja huo kwa lengo la kufikisha habari na kazi za Umoja wa Mataifa.
IMG_2868
Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakiwa na mwenyeji wa msafara wao MC Kalinga wa Arusha wakielekea kukutana na wanafunzi wa USA Academy.
IMG_2874
Mlezi wa Klabu ya Umoja wa Mataifa katika shule ya USA Academy jijini Arusha Bw. Emmanuel Bayo akitambulisha msafara Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN).
IMG_2930
Mkutubi wa Maktaba ya Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Harriet Macha akitoa ufafanuzi juu ya umuhimu wa kuyasoma na kuyatunza machapisho mbalimbali yenye habari za Umoja wa Mataifa kwa Wanafunzi wa USA Academy mara baada ya kutembelea sule hiyo.
IMG_2939
Mjumbe wa Kamati kuu ya Utendaji katika Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) Bw. Haji Musa H akizungumza na wanafunzi wa shule ya  USA Academy waliojitokeza kuupokea ugeni huo ambapo aliwahimiza umuhimu wa kuendelea kushiriki shughuli mbalimbali za Umoja Mataifa na Asasi hiyo kwa ujumla.
IMG_2959
Baadhi ya wanafunzi ambao pia ni wanachama wa klabu cha Umoja wa Mataifa shuleni hapo wakifurahi na kusikiliza mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa juu ya kazi na agenda mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
IMG_2996
Msafara wa Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wanachama wa UN Club USA Academy jijini Arusha kwenye bustani iliyotengenezwa na klabu hiyo shuleni hapo.
IMG_3138
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Katiti mkoani Arusha ambao wameanzisha na kuendesha kilabu hicho shuleni hapo kujiunga kwa wingi zaidi kwani kutawawezesha kujifunza shughuli  za Umoja wa Mataifa duniani, kuhusishwa na mashirika mengine ya kimataifa, kushiriki katika mafunzo mbalimbali, warsha na mikutano ndani na nje ya nchi kama vile National Model UN, the Eastern Africa Model UN, the Africa Regional Model UN na mengineyo, ikiwemo kupata nafasi ya kuisaidia jamii zao kupitia program mbalimbali za kujitolea zitolewazo na YUNA kupitia UNCTN.
IMG_3052
Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakishuhudia moja katika vipaji vingi vya wanafunzi wa klabu ya Umoja wa Mataifa katika shule ya sekondari Katiti.
IMG_3080
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Katiti wakishuhudia vipaji vya Sarakasi na michezo kutoka kwa wanafunzi wenzao wa klabu ya UN.
IMG_3194
Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) pamoja na Mlezi wa UN Klabu na Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Katiti wakiwa kwenye picha ya pamoja mbele ya mti wa kumbukumbu wa klabu hiyo shuleni hapo.
IMG_3258
Msafara wa Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakisalimiana na Mkuu wa Shule ya Sekondari Ilboru ya jijini Arusha Bw. J. Shulla mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
IMG_3262
 Mkuu wa Shule ya Sekondari Ilboru ya jijini Arusha Bw. J. Shulla akizungumza na ugeni huo.
IMG_3269
Mlezi wa Klabu ya UN shule ya Sekondari Ilboru Mwl. Rashid Killasa akitoa utangulizi wa ripoti ya maendeleo ya Klabu hiyo mbele ya wanafunzi na ugeni kutoka Umoja wa Mataifa.
IMG_3275
Mwenyekiti wa Klabu ya Umoja wa Mataifa Ilboru Sekondari Bw. Kamana Msumi akisisitiza kwa wananchama wape juu ya umuhimu wa kuyashika yale yaliyoletwa na msafara huo shuleni hapo.
IMG_3313
Mjumbe wa Kamati kuu ya Utendaji katika Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) Bw. Haji Musa H akizunngumza na wanachama wa klabu ya UN shuleni hapo juu ya faida mbalimbali zipatikanazo ndani ya Asasi hiyo zenye manufaa kwa maisha yao baada ya shule.