Na Andrew Chale
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Aisha Bilal, anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye onesho la Usiku wa Khanga za Kale 2013 ‘5th Extra Vaa Khanga Party’ ndani ya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Novemba 8.
Akizungunza jana, mwandaaji wa onyesho hilo, Asia Idarous, alisema usiku huo Mama Asha Bilal atakuwa mgeni rasmi sambamba na watu mbalimbali maalufu wa ndani na nje ya Tanzania ambo pia watashuhudia muziki wa bendi ya Mashauzi Classic na DJ Mkongwe nchini DJ John Dilinga .
“Wadau wa mitindo watapata burudani na kufurahia mitindo ya khanga itakayoonyeshwa kwenye shoo hiyo, hii si ya kukosa kwa mwaka huu,” alisema Asia Idarous.
Alisema usiku huo vazi la khanga ndilo litakuwa maalumu kwa wadau watakaohudhuria sambamba na kupinga matumizi ya dawa za kulevya.
Onyesho la Usiku wa Khanga za Kale 2013 ambalo mwaka huu limeandaliwa kwa ushirikiano wa Asia Idarous na Fabak Fashions, linatarajiwa kuwa na shangwe mbalimbali ikiwamo kushirikisha watu maarufu na nyota mbalimbali. Wakiwemo Shilole, Snura, Ben Kinyaiya, Kibonde na wengineo.
Kiingilio katika onyesho hilo ni sh 30,000 na viti maalumu itakuwa ni sh 50,000 ambako tiketi zimeanza kuuzwa Fabak Fashions Mikocheni na Gift Shop Serena Hotel.
Aidha, alisema kati ya pesa zitakazo patikana pia zitaenda kusaidia kituo maalum cha kupambana na waathirika wa dawa za kulevya.
Usiku wa Khanga za Kale umedhaminiwa na Redd’s, CXC, Clouds FM, Vayle Spring, Magic FM, Eye View, Amina Design, Kabile, Vijimambo blog,Voice of America, Origin Unite, Channel Ten, DTV, Times FM, Michuzi Media Group, Event Light na Miss Tanzania,New Africa tv.com na wengine wengi.
No comments:
Post a Comment