TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Tuesday 17 December 2013

RUSHWA BARANI AFRIKA,WAZIRI MKUCHIKA AFUNGUKA

george-mkuchika-akiWAZIRI wa nchi ofisi ya rais anayeshughulikian utawala bora George Mkuchika amezitaka nchi za Afrika  kujenga umoja na kupeana uzoefu katika vita vya kupambana na rushwa huku  nchi hizo z ikitakiwa kujenga sera za uwazi kwenye sekta nzima ya rasilimali ili waweze kunufaika nazo ikiwa ni pamoja na kupaza sauti moja kuomba kurejeshwa kwa fedha zilizoko nje ya bara la afrika. Mkuchika alitoa kauli hiyo jana  alipokuwa akifunga na kusherehekea maadhimisho ya siku ya umoja wa mataifa ya mapambano dhidi ya rushwa yaliyofanyika jini hapa.

Alisema kuwa umoja una  nguvu katika kupambana na rushwa hivyo ili kuhakikisha kuwa swala hilo linatokomezwam nchi za afrika zinapaswa kutekelza kwa vitendo mkataba wa umoja wa afrika dhidi ya rushwa kwa kila nchi kujiunga moja kwa moja kwa kutoa uzoefu juu ya mapambano dhidi ya rushwa ambayo yameonekana kurudisha nyuma maendeleo ya bara la Afrka. Alieleza kuwa pamoja na chi za Ulaya kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa lakini nchi hizo zimekuwa zikikumbatia Uhamishaji wa fedha kutoka bara la afrika na kukaa kimya kilawanapotakiwa urejeshwaji wa fedha zilizopo kwenye mataifa hayo.

Aidha alifafanua kuwa nchi 30  zimesaini mkataba wa umoja wa mataifa wa mapambano dhidi ya rushwa kati ya nchi 44 zinazotakiwa kusain mkataba huo hivyo kuzitaka nchi zilizobaki kujiunga na umoja huo ili kuliletea maendeleo bara la afrika na kuwa na sauti moja ya mapambano dhidi ya rushwa huku akizitaka nchi za bara la afrika kutambua kuwa mapambano si ya rushwa si ya mtu moja bali ya watu wote.
Nae mkurugenzi wa takukuru nchini Drt Edward Hosea alisema kuwa bara la afrika bado lina safari ndefu katika mapambano ya vita vya rushwa kwani kati ya nchi za afrika 34 kati ya 44 ndizo amabzo zimesaini mkataba wa mapambano ya rushwa huku akidai kuwa mikataba mingi inaingia kwenye rasilimali za nchi za bara la afrka haina uwazi na sheria zinazotumika  hazimnufaishi mwananchi wa kawaida dhidi yamapambano ya rushwa.

No comments:

Post a Comment