TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Tuesday, 8 October 2013

BAADA YA KUIBA TAIRI YA BAJAJ KIBAKA AONJA JOTO YA JIWE


Kibaka akiwa ndani ya Bajaj akifanya mawasiliano na simu baada ya kupokea kipigo.
Mwenye Bajaj akimvuta kwa hasiri ili amtoe nje.
Madereva wa Bajaj wakimtazama kibaka huyo.
Bajaj iliyoibiwa tairi.
Kibaka  akipelekwa kituo cha polisi.
 
KIBAKA mmoja aliyejulikana kwa jina la Chura jana alioja joto ya jiwe kwa kushushiwa kipigo na madereva wa Bajaj baada ya kuiba tairi ya Bajaj maeneo ya Bamaga jijini Dar es Salaam.

 
Baada ya kupewa  kipigo  kikali alikimbilia kwenye Bajaj na kukaa ndani yake ambapo alivutwa lakini haikuwezekana kutolewa kutokana na jinsi alivyokuwa amejishikilia kwa nguvu  ndipo watu walipoamua kumpeleka katika kituo cha polisi Mabatini. Tairi hilo lililoibiwa halikupatikana.Habari/picha:Na Gladness Mallya

No comments:

Post a Comment