TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Saturday, 12 October 2013

HIDAYA NJAIDI AOMBA MSAADA WA KUTIBIWA MKONO WAKE NJE YA NCHI.

 
  Hidaya Njaidi
 
Muigizaji wa filamu Swahiliwood anayeuvaa uhusika wa mama katika filamu nyingi, Hidaya Njaidi aliyepata ajali mwanzoni mwa mwaka huu na kuumia vibaya mkono anaomba msaada wa matibabu kwani mkono wake umesagika kwa ndani na anahitaji kupatiwa matibabu zaidi nje ya nchi.
Akizungumza na Globalpublishers hivi karibuni, Hidaya alisema kuwa kwa sasa mkono wake unamuuma sana na anachosubiri ni kujua kiasi cha pesa anachotakiwa kutoa na hospitali atakayokwenda kutibiwa kati ya India au Afrika Kusini.
“Wiki ijayo ndiyo nitajua baada ya kurudi Muhimbili lakini ukweli ni kwamba mkono unanisumbua. Hata hivyo, sina pesa za kutosha hivyo naomba watu wanisaidie,” alisema Hidaya ambaye ameng'ara sana na filamu nyingi.

 Get well soon Hidaya...... 
    
 

No comments:

Post a Comment