TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Friday 4 October 2013

TAZAMA YANAYOFANYIKA DAR ES SALAAM JE MIKOA MINGINE YANAFANYIKA?

Mkoa unatambua mchango mkubwa wa wanawake katika kuendeleza familia na kukuza pato la kaya. Katika kuendelea kufanikisha suala hili, Mkoa umesisitiza uanzishwaji wa vikundi na utoaji wa Elimu kwa Wajasiriamali.

Vikundi vya kiuchumi vya wanawake 5,730 na wanaume 2,455 vimeanzishwa. Shughuli ambazo vikundi hivi vinafanya ni uuzaji wa vyakula, ususi, ufumaji, uhunzi, usindikaji na ufungashaji wa bidhaa mbalimbali.

Aidha, wanawake 6,662 wamepatiwa elimu ya ujasiriamali. Uhamasishaji wanawake kujiunga katika ushirika wa kuweka na kukopa (SACCOS). .Jumla ya mitandao 3 na SACCOS 5 za wanawake zimeanzishwa. Aidha vikundi 134 vya kiuchumi vya wanawake vinashiriki katika maonyesho ya kimataifa ya biashara tangu 2005 hadi sasa. Wajasiriamaliwakiuza bidhaa sokoni
Moja ya Soko maarufu la bidhaa Mkoani Dar es Salaam
Wito wangu kwa  mikoa mingine  hasa kina mama jamani tuamke ili tuondokane na shida ndogo ndogo.
 
 
posted by Nkema.

No comments:

Post a Comment