Helkopta ya Ufufuo na Uzima ikitua uwanjani Kawe jijini Dar es salaam Leo.imeandaliwa na http://nkema.blogspot.com/
Waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima Wakiangalia Helkopta wakati inafika uwanjani hapo.
Mchungaji Josephat Gwajima (kushoto) akiwa na Mh.Waziri mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa na maaskofu wa makanisa mengine nchini Askofu Eliud Isanje (wa pili kulia) na Mchungaji Elifuraha Laswai (kulia).
Mch.Josephat Gwajima (kushoto) akiwa na MH.Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa (Kulia)
Muimbaji wa nyimbo za Injili Bon Mwaitege akitumbuiza katika Hafla hiyo Leo jijini Dar es Salaam.
Waimbaji wa kanisa la Ufufuo na Uzima wakiimba katika hafla hiyo kushoto ni Flora Mbasha.
Waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima Wakishangilia katika hafla hiyo.
Mch.Josephat Gwajima akitambulisha wageni waliofika katika uzinduzi huo leo mchana.
Maaskofu na wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini katika hafla hiyo.
Mch.Josephat Gwajima akimkaribisha Askofu Fernandes.
Askofu na mmiliki wa TV ya ATN Fernandes akihubiri.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa baraka zake kwa waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akijadili jambo na maaskofu waliofika katika hafla hiyo leo jijini Dar es salaam. Imeandaliwa na http://nkema.blogspot.com/
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiiingia ndani ya Helkopta hiyo kuashiria kuizindua rasmi kwa safari mbali mbali za injili na kijamii,itakayotumiwa na Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiondoka uwanjani hapo baada ya kumaliza Uzinduzi huo.
Mch. wa kanisa la Ufufuo na uzima Josephat Gwajima akielezea kuhusu kazi zitakazofanywa kupitia Helkopta hiyo leo jijini Dar es salaam katika viwanja vya Kawe, alisema pamoja na kueneza injili kuzunguka Tanzania nzima, Helkopta hiyo pia itasaidia katika dharura zitakazotokea katika jamii nzima ya Tanzania,ikiwemo ajali na majanga yanayohitaji msaada wa haraka.Pia kasema helkopta hiyo itasaidia jamii yote bila kuzingatia itikadi za kidini wala kisiasa. Mch.Kiongozi Josephat Gwajima kasema mwakani majira kama haya zinatarajiwa helkopta zingine tatu kufika Kanisani hapo Ufufuo na Uzima. Na http://nkema.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment