TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Friday, 31 October 2014

PAC yaahidi kuwalinda maafisa wa ofisi ya CAG waliotishiwa maisha na viongozi

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (Public Accounts Committee - PAC) imesema itawalinda na kuwatetea maafisa wa ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General - CAG).

Uamuzi huo unatokana na taarifa za maafisa hao kutishiwa maisha na baadhi ya Viongozi wanaotuhumiwa kuhusika na matumizi mabaya ya fedha za umma, zaidi ya shilingi bilioni 40.

Hatua hiyo ilielezwa katika mkutano uliofanyika mkoani Mwanza, wa majumuisho ya ziara ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali ambayo iliwataka viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhudhuria mkutano huo ili kutoa majibu ya tuhuma hizo. Hata hivyo viongozi hao walipuuza agizo la kamati, hivyo kumlazimu Mwenyekiti kuuvunja mkutano huo.

Mjumbe wa kamati hiyo, Kange Lugora alisema kamati hiyo iliishauri wizara husika kushirikiana nao pamoja tangu mwanzo wa ziara yao katika majumuisho ya kamati hiyo ili kubaini yanayotendeka katika miradi ya maendeleo.

“Kitendo cha wizara kutoshiriki katika majumuisho ya kamati hii ni kuendelea kuhalalisha ubadhirifu unaoendelea kwenye halmashauri, tunaonyeshwa miradi hewa na serikali ngazi ya wizara ilipaswa wajionee wenyewe,” alisema.

No comments:

Post a Comment