TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Thursday, 30 October 2014

MAISHA NI MAPAMBANO,KILA SIKU NI MAPAMBANO.

Kila siku za maisha yetu tunapitia mapambano mbali mbali na changamoto mbali mbali.
Likiisha hili unahisi utakaa kwa raha lakini baadae litakuja lingine.Changamoto kwenye kazi kawaida huwa tunaita matatizo mie natumia neno changamoto.Kama sio kwenye kazi basi kwenye,biashara,nyumbani,kwenye mahusiano yako,kwa majirani,marafiki,watoto,pesa,jamiii yaani likiisha hili baada ya muda linakuja hili.

Usitarajie utakaa kwa starehe mwenyewe ndio maana kila jambo lina kinyume chake.Raha karaha,tabasamu kinyume chake huzuni,kicheko kinyume chake kilio n.k

Napenda ni kwambie vyovyote iwavyo lazima maisha yaendelee.Maisha hayatakiwi kusimama.Tatizo linapojitokeza usipaparike ukatapatapa TULIA.Tuliza akili tafakari na uweze kuona vyema namna utakavyojitoa kwenye tatizo husika.Ukipaparika utashindwa kuona vyema na badala ya kutatua tatizo ukaongeza tatizo.

Pia kubwa angalia CHANZO cha tatizo husika ni nini ili usolve ukijua unasolve nini?tatizo la aina gani
Kwa sababu ya wahaka na roho kuwa juu na maumivu ya tatizo husika unakuta unakuwa na huzuni,hasira,uchungu, ambao unaweza kuzidisha na kuzalisha tatizo jipya hata ukija kutaka kutatua tatizo chanzo hukioni kwa sababu tayari umejijazia matatizo.

Hakuna hali ya kudumu kuwa na imani,kuwa mvumilivu na mwenye subira.Usikae chini ukasema yaani jamani kila siku mimi tu mimi tu matatizo yananiandama kila mtu ana mapambano yake na anapambana nayo kivyake.Usikae chini ukajihurumia simama.

Wakati mwingine matatizo na changamoto ukiyatazama vizuri yanaweza kuwa fursa.Sio yote inategemea ni tatizo gani.

Litambue tatizo,usipaparike stay calm,acha mawazo na akili yako yawe chanya ili uweze kuona vyema na kutafakari vyema.Kuwa kwenye control sio tatizo ndio likucontrol wewe.

*Haya ni mawazo yangu kama mdau unaweza kujazilizia mtazamo wako pindi tunapopitia changamoto mbali mbali za kimaisha tufanyeje?*

*wewe hufanyaje nyakazi za matatizo na changamoto?*

*Hapo siongelei Msiba au kifo.

Na Dina Marios.

No comments:

Post a Comment