TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Sunday, 3 November 2013

SIFURI HAIJAFUTWA ASEMA -ASEMA MULUNGO

Siku mbili baada ya Wizara kutangaza mfumo mpya na kuufuta mfumo wa zamani wa viwango vya upangaji wa alama za ufaulu kwa kidato cha nne na sita, na kueleza kuwa kwa sasa hakutakuwa na Daraja la Sifuri badala yake limewekwa Daraja la Tano -- mabadiliko ambayo watu mbalimbali walitoa maoni yao na kusema ikiwa kweli Serikali ina nia thabiti ya kuinua kiwango cha elimu nchini, basi inapaswa kiufumua mfumo mzima wa elimu badala ya kugusa vitu vidogovidogo tu -- leo katika gazeti la HabariLeo imechapishwa habari isemayo:


Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo ameeleza kuwa katika kubadili mfumo wa upangaji alama za ufaulu wa mitihani ya sekondari, Daraja Sifuri litaendelea kuwepo. Mulugo alisema hayo jana wakati wa mahafali ya 

Chuo Kikuu cha Tumaini Kampasi ya Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Karimjee.

Alisema dhana ya kuwepo kwa Daraja la Tano katika mfumo mpya, haikueleweka kwa wadau wengi na hivyo wataendelea kuelimisha umma juu ya mfumo huo mpya.

“Msiniulize mantiki hii ya divisheni 5 na Sifuri, kwa sababu ufafanuzi utatolewa. Kufaulu ni kufaulu tu na kufeli ni kufeli tu, hiyo divisheni 5 ni kufeli tu,” alisema Mulugo katika mahafali hayo, ambayo waandishi watatu wa gazeti hili, Oscar Mbuza, Betram Lengama na Anastazia Anyimike walitunukiwa Shahada ya Kwanza katika Mawasiliano ya Umma.
 
 

No comments:

Post a Comment