TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Thursday 10 October 2013

ZIJUE FAIDA ZA MATUNDA HAYA ILI KUBORESHA AFYA YAKO

 

Kuna faida nyingi za kula matunda licha ya kupenda ladha tamu za  matunda tunayokula. Matunda yana virutubisho vingi ikiwa vitamin A na C hupatikana kwenye matunda mengi ukilinganisha na virutubisho vingine vilivyopo kwenye matunda mengine.
Matunda husaidia kupunguza matatizo ya moyo( heart diseases ), stroke ( kiharusi ), shinikizo la damu ( blood pressure ), cholesterol, aina mbalimbali za saratani (cancer ), matatizo ya uwezo wa macho kuona na mengine mengi.
Matunda yote yana manufaa kwa miili yetu lakini napenda ujue haya machache kuhusu faida za apple, parachichi, ndizi, zabibu, embe, chungwa, papai na nanasi. Matunda haya niliyoyataja huwa tumezoea kuyala lakini naamini wengi wetu hatujui sana kuhusu ni vitu gani tunanufaika kutokana na kula matunda haya.
Zijue faida za matunda.....

APPLE.

-Hupunguza uwezekano wa kupata kisukari ( diabetes ) na pumu (asthma )

-Husaidia kinywa kutokuwa na harufu mbaya ( natural mouth fresher )  vilevile apple husafisha meno kila unapotafuna.

Je Unajua? Harufu nzuri ya apple hupatikana kwenye maganda/ngozi yake, hivyo ni vyema ukalitafuna pasipo kulimenya kwani vitamin nyingi pia hupatikana kwenye maganda/ngozi ya juu.

PARACHICHI.

-Ni chanzo cha vitamin E.

-Hupunguza kiwango cha cholesterol mwilini.

-Kwa afya njema ya moyo wako, kwenye sandwich au mkate tumia parachichi badala ya siagi.

Je Unajua? Watoto hupenda sana kula parachichi kwasababu ni laini na pia mafuta ya parachichi husaidia katika kukuwa kwa mtoto na kuwa mwenye afya bora.

NDIZI.

-Ni chanzo cha vitamin B6 na madini ya potassium.

-Licha ya kuwa na ladha nzuri, ndizi zina madini mengi ya potassium ukilinganisha na matunda mengine ambayo husaidia kupunguza ongezeko la shinikizo la damu ( blood pressure ).

Je Unajua? Watu wenye aleji na material ya mpira( rubber latex ) wanaweza pia kuathirika kwa aleji ya ndizi kwakuwa mpira na ndizi vyote zina aina moja ya protini.

ZABIBU.

-Ni chanzo cha madini ya manganese.

-Hupunguza uwezekano wa kupata maradhi ya moyo kwa kusaidia kushusha kiwango cha shinikizo la damu ( blood pressure )

-Huepusha magonjwa ya aina mbalimbali za saratani kwa kuzuia usambaaji wa seli za saratani ya titi ( breast cancer ), tumbo ( stomach cancer ) na utumbo ( colon cancer ).

Je Unajua? Unaweza gandisha zabibu za kijani na nyekundu na ukazitumia kama barafu ( ice cubes ) kwenye kinywaji chako upendacho.

EMBE.

-Ni chanzo cha vitamin A na E.

-Vitamin A  iliyopo kwenye embe husaidia kuboresha macho yako kwa kukuwezesha uweze kuona vizuri. Pia husaidia kupunguza uwezekano wa upofu kwa wazee kwa kuimarisha macho yao.

Je Unajua? Embe ni tamu sana likiwa limeiva lakini pia likiwa bichi unaweza kutumia embe kutengenezea kachumbari, achali, chutney na salad.

CHUNGWA.

-Ni chanzo cha vitamin C na madini ya potassium.

-Chungwa lina vitamin inayojulikana kama ‘’folate’’ ( B-Group Vitamin ) ambayo husaidia katika kujengeka kwa ubongo wa mtoto kwa mama mjamzito.

-Chungwa lina kemikali zinazojulikana kama ‘’hesperidin’’ ambazo hupunguza kiwango cha cholesterol kwenye damu.

Je Unajua? Sehemu nyeupe ya chungwa ( gome lililo ndani ya chungwa ) lina thamani ya vitamin karibia sawa na nyama ya chungwa hivyo ni vyema kula chungwa lote baada ya kumenya maganda yake.

PAPAI.

-Ni chanzo cha vitamin A na C.

-Papai lina enzyme ijulikanayo kama ‘’papain’’ ambayo husaidia katika kusaga au mmeng’enyeko wa chakula.

-Pia vitamin A iliyopo kwanye papai husaidia husaidia kuboresha afya ya ngozi yako.

Je Unajua? Mbegu nyeusi za papai zinaweza kuliwa japo kuwa ni chungu lakini unaweza kuzisaga na salad kwa kutumia blender badala ya pili.

NANASI.

-Nanasi lina enzyme asilia ijulikanayo kama ‘’bromelain’’ ambayo husaidia kuvunjavunja  protini hivyo husaidia katika mmeng’enyeko wa chakula.

-Vilevile enzyme ya bromelain husaidia kupunguza ukuaji wa seli za saratani na kuchochea uponaji wa vidonda kwa haraka.

Kwa hayo machache hapo juu unaona ni jinsi gani matunda yalivyo muhimu kwa kujenga afya zetu na kutumika kama dama kwa miili yetu. Napendekeza upende kula angalau tunda moja kwa siku kwa uboreshaji wa afya yako.

No comments:

Post a Comment