TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Monday, 14 October 2013

UFOO SARO WA ITV NA REDIO ONE, AJERUHIWA KWA RISASI, MAMA YAKE AFARIKI DUNIA




Habari zilizoufikia mtandao huu, zinasema kuwa, Mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha ITV na Redio One, Ufoo Saro pichani, amejeruhiwa kwa risasi na mtu anayedaiwa kuwa mchumba wake, ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, ambaye pia amejiua kwa kijipiga risasi baada ya kudhani kuwa tayari alikwisha muua mwandishi huyo.

Aidha habari zinasema kuwa katika tukio hilo, pia Mama yake mzazi na Ufoo Saro, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na Jamaa huyo, katika tukio hilo lililotokea jana nyumbani kwa mama mzazi wa Ufoo maeneo ya Kibamba.  Habari zinasema kuwa jamaa huyo aliwasili nchini juzi na  kufikia nyumbani kwa Mchumba wake huyo, 'Ufoo' na jana majira ya saa 11, waliondoka wawili hao na kwenda nyumbani kwa Mama mzazi wa Ufoo huko maeneo ya Kibamba, ambapo imeelezwa kuwa huenda wawili hao walifunga safari hiyo kwa kutafuta suluhisho la kutoelewana kwao.   Akizungumza na Radio one Kamanda wa Polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni kamanda Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana na kuongeza kuwa muuaji huyo amegundulika kuwa ni mfanyakazi katika Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) huko Sudani ila bado haijafahamika kwamba anafanyia kitengo gani.  
Imeelezwa kuwa hali ya mwandishi huyo inaendelea vizuri akiwa amelazwa ICU katika Hospitali ya Muhimbili, akiendelea kupatiwa matibabu.  Aidha imeelezwa kuwa Ufoo amejeruhiwa maeneo ya tumboni, ambapo inadaiwa ndipo alipopigwa risasi nyingi zaidi, begani na mguuni.

No comments:

Post a Comment