Viongozi wawili wa kundi la wabaguzi wa Afrika Kusini lililojulikana naka "Boer Army" lililokula njama ya kumuua Rais wa Kwanza wa asili ya Afrika, Nelson Mandela na kisha kuwafuta kabisa watu weusi nchini humo, wamehukumiwa vifungo vya miaka 35 jela kila mmoja na mahakama kuu ya Pretoria nchini humo.
Shirika la habari la Afrika Kusini, SABC limesema hukumu hiyo imetolewa leo baada ya kuendeshwa kwa miaka 10. Mahakama iliyotoa hukumu hiyo ilimkuta kiongozi Mike du Toit, aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu na hatia katika kosa hilo wakati yeye akiongoza mipango ya kuipindua Serikali mwaka 2002 kwa madhumuni ya kukiangusha na kukifutilia mbali kabisa chama cha ukombozi cha ANC. Viongozi wengine takriban 20 walihukumiwa vifungo vya chini ya miaka 35. |
tangaza hapa
TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA
Tuesday, 29 October 2013
ALIYEPANGA KUMUUA MANDELA AHUKUMIWA MIAKA 35 JELA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment