TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Thursday, 31 October 2013

BAADA YA WIKI MBILI TANZANIA KUTOA UAMUZI KUHUSU HATIMA YAKE EAC.

Picture
Akijibu maswali ya Wabunge katika kikao cha Bunge tarehe 30 Oktoba 2013, Waziri anayeiwakilisha Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Samuel Sitta amesema tayari barua imeshaandikwa na kutumwa kwenye Jumuiya na majibu yanatarajiwa kupatikana ndani ya wiki mbili kutoka sasa, hivyo akawataka Watanzania kuvuta subira ili kujua uamuzi utakaochokuliwa kulingana na majibu watakayopatiwa.

Wakati huo huo, Waziri Sitta ameliezeleza Bunge kuwa Mamlaka Kuu ya Tanzania imemzuia Waziri wa Mambo ya Nchi za
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe kuhudhuria mkutano wa Mawaziri wanachama wa Jumuiya hiyo unaofanyika jijini Nairobi nchini Kenya kutokana na baadhi ya nchi kuwa tayari zilishafanya utaratibu wa kuunda shirikisho nje ya utaratibu, jambo alilolifananisha na mchezo wa kuigiza wa kushiriki kwenye vikao vya mambo ambayo tayari baadhi ya nchi wanachama wameshayawekea msimamo na kuafikiana.

Waziri Sitta pia aligusia uwezekano wa kuunda mbadala na nchi nyingine kama vile Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, "Kiuchumi sisi ni majirani zaidi na DRC... Rwanda inaangalia barabara tunayoshirikiana kuijenga kufika Burundi, ila ujenzi wa reli ya Uvinza-Msongati itaokoa wenzetu wa Burundi, kwani wakitumia bandari ya Mombasa kwenda Bujumbura, kwao ni mbali kwa zaidi ya kilometa 900, tofauti na Dar es Salaam kwenda Bujumbura," alifafanua Sitta.

Makosa 11 wayafanyayo wanaume waliooa

Picture
(picha: apartmenttherapy.com)
Laiti wanaume waliooa wangejua na kurekebisha makosa haya wayafanyayo kama yalivyochapishwa na Fuledi:-
  • Kutumia nguo nzuri au taulo la mwilini kufutia gari.
  • Kuingia ndani na viatu vya matope wakati kumeshadekiwa.
  • Kuvuruga nguo au vitu wakati wa kutafuta kitu kabla ya kuuliza kilipo.
  • Kuacha magazeti yanazagaa baada ya kuyasoma.
  • Kumleta rafiki yake kuja kula bila kutoa taarifa.
  • Kumsifia rafiki au ndugu wa mke wa kike kuwa anavutia bila hofu.
  • Kukosoa muonekano wa mke bila kujali atajisikiaje.
  • Kutosema chochote mke akipendeza mpaka aulize.
  • Kujifutia taulo na kuliacha ovyo bila kulianika.
  • Kutotandika bed mke asafiripo na kugeuza bed kama kiota cha ndege.
  • Kutofua boxer na socks zake hadi wife awepo na kama kasafiri zitasubiri arudi.

Wednesday, 30 October 2013

UAMUZI WA MAPITIO YAHUKUMU YA BABU SEYA

 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza 'Papii' wakiwa na nyuso za furaha wakati wakitoka katika Mahakama ya Rufaa baada ya majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kusikiliza maombi yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia hukumu iliyoitoa mwaka 2010.
 Nyuso za matumaini.......
 Johnson  Nguza 'Papii' akibusu mkono wake baada ya kuibusu ardhi mara baada ya kutoka mahakamani.
 Papii akinyoosha mkono juu kama ishara ya kumshukuru mungu.
 Waandishi wa habari wakiwa chini wakati wa harakani za kuchukua matukio mahakamani hapo.
 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza wakati wakitoka mahakamani.
 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza au Papii wakiwa  katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania kabla ya kuanza kwa  kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu  iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo.  
 Watu waliohudhuria mahakama hapo wakifuatilia kesi hiyo.
 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza au Papii wakiwa  katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania kabla ya kuanza kwa  kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu  iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo.  
 Mahakamani.
Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza wakiteta jambo na wakili wao, Mabere Marando.
Picha Kwa Hisani ya Michuzi Blog

watuhumiwa 7 waliokamatwa na kiganja cha mkono wa Binadamu Mwanza wafikishwa polisi. (Onyo: picha zinatisha )




6
WAGANGA wawili wa jadi akiwemo mfanyabiashara mmoja wamenaswa jijini Mwanza wakiwa na kiungo cha mkono wa kulia unaoamainika kuwa wa binaadamu ambapo walikamatwa kwenye eneo la ziwani na Uwanja wa Ndege wa Mwanza, kufatia taarifa za raia wema na kisha jeshi la polisi kuweka mtego kwa muda wa wiki nzima na kufanikiwa kuwakamata.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Joseph Konyo amethibitisha tukio hilo na kwamba mkono huo uliokuwa umewekwa kwenye begi ukiwa umefungwa kwenye mfuko mweusi wa plasitiki na kuviringishwa kwenye karatasi nyeupe ya nailoni, umekutwa ukiwa mbichi.
Konyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Mwanza (RCO), alieleza kuwa watuhumiwa hao (majina yanahifadhiwa) wenye umri wa miaka 36 na 43 (ni waganga wa jadi wawili) na mfanyabiashara ana miaka 48.
Taarifa zilizotolewa katika jeshi hilo na kuweka mtego huo kisha makubaliano ya kununua viungo hivyo kutoka kwa watuhumiwa hao (wauzaji), walimhakikishia mnunuzi (polisi) kuwa wanaweza kupata kichwa, mikono, miguu na sehemu za siri za binaadamu endapo mteja angehitaji.
2 
kwa mujibu wa makubaliano hayo wauzaji hao ambao ni Waganga walitaka kupewa shilingi milioni 100 kwa mkono huo mmoja lakini baada ya kufanya mazungumzo ya kibiashara na wao kuona kitita cha fedha, walilegeza bei na kujikuta wakitiwa mbaroni baada ya kuonyesha kiungo hicho.
5
3
4
1
7Stori na picha vimetoka na gsengo.blogspot.com

Tuesday, 29 October 2013

PAPII KOCHA AANDIKA BARUA KWA RAIS JAKAYA KIKWETE



YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.

Husika na somo hilo hapo juu.

Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga. Kwa heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya kiMUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais. Nakuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais, kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maishagerezani,niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu. Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo, na ukweli kutoka moyoni sikufanya kosa hilo. Si mimi, baba yangu Nguza wala ndugu yangu yeyote aliyefanya kitendo kile. Lakini wenye mamlakawakatuona tuna hatia na kuamua kuteketeza kizazi chetu gerezani.

Natamani kiama ifike ili mwenyezi Mungu aweke wazi ukweli wote uliojificha nyuma ya pazia. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako
mitukufu Mh. Rais Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji
huruma yako wewe mzazi. Lakini pia sisi ni binadamu wenye nafsi na miili kama wengine. Waliotumia mamlaka yao kutuweka gerezani nao ni binadamu pia, wenye miili na nafsi. Ipo siku nafsi zetu zitapaswa kutoa hesabu ya tuliyoyafanya hapa duniani. wakati huo miili yetu tunayoitumia
kunyanyasa wanyonge itakuwa imeoza mavumbini.

Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu. Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.

Mungu akubariki.
Wako mtiifu
Mfungwa NO:836'04
JOHNSON
NGUZA (PAPII KOCHA

Posted by Link Live Tz

 

KITU KIPYAA CHA IRENE UWOYA


STAA kunako tasnia ya filamu,Irene Uwoya ameuanika mkoko wake mpya Range Rover.
Kupitia mtandao wa instagram Uwoya alipost picha za gari hilo huku akiandika… I don't care… Watasubiri sanaaaa…. My bby.
Huku watu wakicoment kwa kumpongeza kuwa huwa anaongea kwa vitendo na siyo…
STAA kunako tasnia ya filamu,Irene Uwoya ameuanika mkoko wake mpya Range Rover.
Kupitia mtandao wa instagram Uwoya alipost picha za gari 
 
hilo huku akiandika… I don't care… Watasubiri sanaaaa…. 

ALIYEPANGA KUMUUA MANDELA AHUKUMIWA MIAKA 35 JELA



 
Viongozi wawili wa kundi la wabaguzi wa Afrika Kusini lililojulikana naka "Boer Army" lililokula njama ya kumuua Rais wa Kwanza wa asili ya Afrika, Nelson Mandela na kisha kuwafuta kabisa watu weusi nchini humo, wamehukumiwa vifungo vya miaka 35 jela kila mmoja na mahakama kuu ya Pretoria nchini humo.

Shirika la habari la Afrika Kusini, SABC limesema hukumu hiyo imetolewa leo baada ya kuendeshwa kwa miaka 10.

Mahakama iliyotoa hukumu hiyo ilimkuta kiongozi Mike du Toit, aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu na hatia katika kosa hilo wakati yeye akiongoza mipango ya kuipindua Serikali mwaka 2002 kwa madhumuni ya kukiangusha na kukifutilia mbali kabisa chama cha ukombozi cha ANC.

Viongozi wengine takriban 20 walihukumiwa vifungo vya chini ya miaka 35.

HII IMEKAA VIZURI


KATOONI HII IMETOLEWA KWENU KWA IDHINI YA MDAU WETU MARCO TIBASIMA
 

HATIMAYE JAMII PRODUCTION YAZINDULIWA RASMI


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara alipokuwa akisisitiza jambo wakati wa mahojiano mafupi aliyofanya na Jamii Production kabla ya KUZINDUA RASMI shughuli za kutayarisha na kusambaza matangazo ya Radio na Video.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiwa na waanzilishi wa Jamii Production, Mubelwa Bandio (kulia) na Abou Shatry (kushoto)

Naam....
Kwa baraka za Mhe. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt
Fenella Mukangara, JAMII RASMI IMEZINDULIWA RASMI Oktoba 26, 2013, alipotutembelea kuangalia utendaji wetu na kuizindua rasmi hapa ofisini
kwetu Washington DC.
Hii ilikuwa ni ZAIDI YA TUKIO.
Ilikuwa ni BARAKA KWETU na tunamshukuru kila aliyewezesha hili.
NA SASA.....
Kazi ya kutekeleza yale yaliyousiwa na Mhe Waziri, yaliyo yaliyo msingi
wa kituo chetu, yale yaliyo MAHITAJI ya walaji (hadhira yetu) NA WAJIBU
WA FANI YETU ndio imeanza.
Na......
Hakuna litajalokuwa na maana kama hatutajua namna ambavyo utendaji wetu unaathiri maisha yako kwa namna CHANYA na HASI
Wewe (msikilizaji, mtazamaji na msomaji wetu) ni mdau mkubwa wa kufanikisha hili. Tuzidi kushirikiana TWAWAPENDA
Msimamizi wa vipindi na mpigapicha mkuu wa Jamii Production Abou Shatry akisisitiza jambo kabla ya kuwasili kwa mgeni rasmi
Mtayarishaji na Mtangazaji wa kipindi cha FAMILIA Georgina Lema akiwa "kitini"

Mmoja wa wawezeshaji wakuu wa Jamii Production Bwn Isidory Lyamuya wa Prestige Health Services akijaribu vitendea kazi vya kituo.
Mhe. Waziri Mukangara akipokea maelezo ya utendaji wa kituo. Kushoto ni Afisa Ubalozi Mindi Kasiga

 Mhe. Waziri akisikiliza RISALA ya Jamii Production
 Mhe. Waziri Mukangara akijibu risala ya Jamii Production
Bwn Isidory Lyamuya akipata akipata picha ya pamoja na Mhe. Waziri kwa msaada anaotoa kufanikisha kazi za Jamii Production
Bwn Isidory Lyamuya akipata mkono wa pongezi toka kwa Mhe. Waziri kwa msaada anaotoa kufanikisha kazi za Jamii Production
Abou Shatry akipongezwa na Mhe Waziri Mukangara
 "Mwanamama" Georgina Lema wa kipindi cha FAMILIA akipata kumbukumbu na Mhe. Waziri
  Mkurugenzi wa Mambo Jambo Radio Bwn Julius Makiri ambaye aliungana nasi katika uzinduzi huu rasmi akipata kumbukumbu na Mhe. Waziri
 Mhe. Waziri Dkt Fenella Mukangara na Afisa Habari katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mindi Kasiga pamoja na wanaJAMII
 
Hakuna ZAWADI kubwa sawa na kilichofanyika. Na zawadi pekee tuliyonayo ni UPENDO. Ambao hauonyesheki wala haupimiki.

Lakini....tunapenda POPOTE UWAPO, UKUMBUKE SIKU YA LEO.
Na hivyo..twaomba KIKOMBE hiki kiwe kumbukumbu ya tukio hili kubwa kwetu
Abou Shatry akiwa mahala anapopatawala zaidi...

Monday, 28 October 2013

FILAMU YA "FIGO" KUTOKA PROIN PROMOTIONS KUINGIA SOKONI MUDA WOWOTE KUANZIA SASA

 

 
Kampuni ya utengenezaji,uuzaji na usambazaji wa filamu za kitanzania ya Proin Promotions Limited inatarajia kuingiza movie yake nyingine sokoni mapema wiki hii. Filamu ya "FIGO" ni filamu ya kitanzania ambayo imechezwa na waigizaji wakongwe katika tasnia ya filamu nchini na Ni filamu ambayo inasimimua,kufundisha na kuelemisha, Filamu ya Figo ni moja kati ya filamu ya Kitanzania ambayo imechezwa kwa ustadi wa hali ya juu na kutengenezwa kwa hali ya juu na kampuni Mahiri ya Utengenezaji na Uuzaji wa Filamu Tanzania ya Proin Promotions Limited 

Proin Promotions ni moja ya kampuni kubwa ya utengenezaji,uuzaji na usambazaji wa filamu Tanzania ambayo tayari ishaingiza Sokoni Filamu Mbili ambazo zinafanya Vizuri kama vile Foolish Age, Long Time na sasa inakuletea Filamu ya FIGO ambayo imechezwa na Jennifer Kyaka ambaye anafahamika kama Odama, Irene Uwoya, Rachel Haule, Stanley Msungu na wengineo wengi.

Filamu ya "FIGO" inatarajia kuingia sokoni muda wowote kuanzia sasa ambapo itapatikana katika maduka yote ya Uuzaji wa filamu na Kwa mawakala Wao Nchini Nzima, Vilevile Unaweza kununua filamu hiyo ya figo kupitia Ukurasa wa facebook wa Proin Promotions Limited Kupitia https://www.facebook.com/proinpromotions na kupitia pia tovuti yao ya http://www.proinpromotions.com

Sunday, 27 October 2013

KINACHOENDELEA MSIBANI KWA BABA’KE WEMA MAREHEMU BALOZI SEPETU

Mama mzazi wa Wema akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mumewe mzee Sepetu.

Wema Sepetu akiwa katika hali ya majonzi baada ya kufiwa na baba yake mzazi.
Kajala Masanja (kushoto), Wema Sepetu (katikati) na Zamaradi Mketema (kulia) wakiwa katika hali ya majonzi nyumbani kwao Wema Sepetu, Sinza - Mori jijini Dar.
Kajala Masanja (kushoto) na Wema Sepetu (katikati) wakiangua vilio. Kulia Zamaradi akijaribu kumtuliza Wema.
Ndugu wa karibu wa marehemu akiwa na simanzi nzito.
Wema Sepetu akibubujikwa na machozi baada ya kuondokewa na baba yake mzazi.
STAA wa sinema za Kibongo na Miss Tanzania 2006 Wema Isaac Sepetu, bado yuko kwenye wakati mgumu baada ya leo asubuhi kupatwa na msiba mkubwa wa kuondokewa na baba yake mzazi Balozi Isaac Abraham Sepetu aliyefariki asubuhi ya leo.
Kwa sasa kuna watu wengi wamefika kumjulia hali maeneo ya Sinza, Mori jijini Dar, rafiki yake wa karibu Kajala Masanja na Zamaradi Mketema wapo bega kwa bega kuwa naye karibu na vilio vimetawala kila kona ya familia ya marehemu Balozi Sepetu.
Bado haijafahamika mazishi yanafanyika lini maana wanasubuliwa watoto wa Marehemu Tunnu Sepetu na Sunna Sepetu ambao wanaishi nchini Marekani, lakini kuna tetesi kuwa huenda mazishi hayo yakafanyika siku ya Ijumaa.
Mama mzazi wa Wema bado yuko kwenye hali ya huzuni baada ya kufiwa na mume wake ambaye amedumu nae kwa miaka mingi kabla ya kupatwa na mauti asubuhi ya leo katika hospitali ya TMJ jijini Dar. Mpaka mauti yanamfika, marehemu alikuwa akisumbuliwa na kisukari pamoja na kiharusi.

habari na Global publisher