TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Wednesday, 8 October 2014

FASHION LEO










NSSF kuwezesha mradi wa daraja la kigamboni na ujenzi wa nyumza za gharama nafuu,Rais Kikwete asifu juhudi hizo

Waziri wa ujenzi, Dk. John Magufuli akielezea jinsi wizara yake ilivyojipanga kuhakikisha kuwa malengo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni unaofadhiliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), inafikiwa na kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam. Rais Kikwete alitembelea mradi huo pamoja na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa nyumba za garama nafuu zilizopo Kijichi Dar es Salaam.

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dk. Ramadhan Dau (wa pili kulia) akimweleza jambo Rais Jakaya Kikwete wakati wa ziara ya rais kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni ambayo inafadhiliwa na NSSF, pamoja na kuweka jiwe la msingi katika  mradi wa nyumba za garama nafuu zilizopo Kijichi Dar es Salaam.
 Rais Jakaya Kikwete akiongea na wahusika wa ujenzi wa daraja la Kigamboni inayofadhiliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
  Waziri wa ujenzi, Dk. John Magufuli akielezea jinsi wizara yake ilivyojipanga kuhakikisha kuwa malengo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni unaofadhiliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), inafikiwa na kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam. Rais Kikwete alitembelea mradi huo pamoja na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa nyumba za gharama nafuu zilizopo Kijichi Dar es Salaam.

Rais Jakaya Kikwete ametembelea daraja la Kigamboni, Dar es Salaam, jana, ambapo ameagiza changamoto zilizoanishwa zitatuliwe haraka kabla mradi haujamalizika. Akizungumza wakati wa kupokea taarifa ya ujenzi huo, Rais Kikwete alisema utekelezaji wa mradi unapaswa kwenda sambamba na utatuzi wa changamoto hizo.

Mapema wakati akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Makamu Mwenyekiti wa Mradi huo, John Msemo, alisema zipo changamoto chache ambazo zinapaswa kutatuliwa kwa ushirikiano na serikali.
Alizitaja changamoto hizo kuwa pamoja na zile za wembamba wa baadhi ya barabara pamoja na msongamano wa magari. Alitoa mfano wa barabara za Vijibweni-Mjimwema, Bendera Tatu-Kamata na Gerezani- Ohio kuwa ni nyembamba.

Pia aliutaja msongamano wa magari katika makutano ya barabara ya Kilwa- Mandela, Chang'ombe-Mandela na Nyerere (Tazara) kuwa unapaswa kushughulikiwa. Akizungumzia suala hilo, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alisema tayari serikali imeanza kushughulikia changamoto hizo, ambapo imeongea na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) pamoja na kutenga fedha katika bajeti kwa ajili ya upanuzi wa barabara hizo.

Dk. Magufuli alisema katika bajeti ya mwaka huu, fedha zimetengwa kulipa fidia kwa ajili ya barabara ya Vijibweni-Mjimwema ili iongezwe upana na kwamba, ile ya Ohio-Gerezani mazungumzo yanaendelea na ADB.

Daraja la Kigamboni linalojengwa kwa ushirikiano wa serikali na wadau na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambapo linatarajiwa kukamilika Juni, mwakani na kuzinduliwa na Rais Kikwete. Baada ya kutembelea mradi huo, Rais alikagua ujenzi wa nyumba 1,120 zilizojengwa na NSSF katika eneo la Mtoni Kijichi, Kigamboni, ambapo aliupongeza uongozi wa shirika hilo kwa kukamilisha mradi huo wa nyumba za watu wa kipato cha kati na chini.

Rais alizindua mradi huo na kuiagiza Manispaa ya Temeke kuangalia uwezekano wa kuijenga vizuri barabara inayokwenda mahali nyumba hizo zilipo pamoja na kutengeneza miundombinu nyingine muhimu ikiwemo maji. Mapema wakati wa ziara hiyo, Rais ambaye alisherehekea siku yake ya kualiwa jana, alikabidhiwa kadi maalumu ya kumtakia maisha marefu na Mkurugenzi Mkuu wa Nssf, Dk. Ramadhan Dau.

KATIBU WA CCM,KINANA ATINGA JIMBO LA ISIMANI IRINGA NA KUWATAKA VIONGOZI KUWATUMIKIA WANANCHI IPASAVYO



 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsifia Mbunge wa Jimbo la Isimani,  William Lukuvi kwa uchapakazi wake mzuri wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Magozi, Kata ya Ilolo Mpya, Iringa Vijini leo. Kinana alimjia juu Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu kwa kushindwa kutafutia ufumbuzi migogoro ya wananchi.Pia aliwataka wananchi kuacha kukwepa majukumu yao ya kuwatumikia Wananchi. 


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa  CCM, Nape Nauye akihutubia katika mkutano huo


 Kinana akisalimiana na wananchi alipowasili kushiriki ujenzi wa jengo la CCM tawi la Luganga Kata ya Ilolo Mpya.

 Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana na Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Lukuvi wakishiriki kufyatua tofali za ujenzi wa jengo la Ofisi ya CCM.


 Kinana na Lukuvi wakisaidia kufyatua tofali za kujengea jengo hilo la CCM


 Wanachama wa CCM Shina namba 6 katika Kijiji cha Magozi, Kata ya Ilolo Mpya wakicheza kwa furaha wakati Kinna alipofika kuzungumza nao


 Kinana akizungumza na wananchama wa shina hilo. Kulia kwake ni Balozi wa shina hilo Chengula Mlula


 Kinana na Lukuvi wakitoka kukagua ujenzi wa Zahanati ya Magozi Kata ya Ilolo Mpya, Isimani


 Kinana na Lukuvi wakijadiliana jambo baada ya kukagua ujenzi huo

 Wamasai wakiingia kwenye mkutano kutumbiza kwa ngoma ya asili

 Wasanii wakicheza ngoma ya asili ya kabila la wasukuma


 Lukuvi akimkabidhi kompyuta na mashine ya kudurufia Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Pawaga Charles Mgimwa kwa ajili ya matumizi ya shule

         Mgimwa akifurahia msaada huo

 Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, Amina Imbo (kushoto) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa UWT wa wilaya hiyo, Shakila Kiwanga wakati wa mkutano huo

 Mbunge wa Jimbo la Isimani, ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi akielezea miradi inayyotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM jimboni humo.


 Mmoja wa wananchi akiuliza swali kwa Katibu Mkuu Kinana kuhusu mgogoro wa ardhi  wa wanakijiji na Jeshi la Magereza.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Dk. Beatrice  Ishengoma akijibu swali hilo ambapo alisema kuwa kwa asilimia kubwa wamelitafutia ufumbuzi na kwamba kilichobaki ni wizara husika kwenda kupima na kuweka alama za mipaka.

HALIMA MDEE ,MBUNGE WA KAWE NA WENZAKE WALIVYOPELEKWA GEREZA LA SEGEREA BAADA YA KUNYIMWA DHAMANA

 Mbunge wa Kawe Halima Mdee (kulia), akionesha alama ya mbili inayotumiwa na Chadema wakati akisindikizwa na polisi kwenda kupanda gari kuelekea gereza la Segerea Dar es Salaam jana baada ya kunyimwa dhamana na wenzake kutokana na kesi inayomkabili ya kufanya maandamano yaliyozuiliwa na jeshi la polisi.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee, akipanda gari la Polisi Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam jana, wakati akipelekwa Gereza la Segerea.
 Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiimalisha ulinzi katika Mahakama ya Kisutu.
 Hapa Halima akisindikizwa kupanda gari.
 Baadhi ya wanachama wa Chadema, waliokuwa na Halima wakiwa ndani ya gari la polisi kabla ya kupelekwa segerea.
 Baadhi ya wanachama wa Chadema, waliokuwa na Halima wakiwa ndani ya gari la polisi kabla ya kupelekwa segerea wakionesha alama ya mbili inayotumiwa na chama hicho.
 Gari lililombeba Halima na wenzake 
likiondoka Mahakama ya Kisutu.
Wanachama wa Chadema wakishangilia nje ya 
Mahakama ya Kisutu.


MBUNGE wa  Jimbo la Kawe Halima Mdee (35) amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za  
kutotii amri halali ya Jeshi la Jolisi na kufanya mkusanyiko usio halali.  
Wakili wa Serikali Mkuu Bernard kongola akisaidiana na Salum Mohamed na Hellen Mushi 
alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi  Janeth Kaluyenda wa Mahakama ya Hakimu Mkazi 
Kisutu, Dar es Salaam kuwa Mdee anakabiliwa na mashtaka mawil
Kongola alidai mbali na Mdee washtakiwa wengine ni Rose Moshi (45), Renina Peter Anna Linjewile(48), Mwanne KAssim (32), Sophia Fangel (28), Edward Julius (25), Martha 
Mtiko (27) na Beatu Mmari (35) wote wa kazi wa Dar es Salaam.
Ilidaiwa kuwa Oktoba 4 mwaka huu washtakiwa wakiwa mtaa wa Ufipa, bila kuwa na 
uhalali walikiuka amri halali ya kutawanyika iliyotolewa na Mrakibu wa Polisi (SP) Emmanuel 
Tillf kwa niaba ya Jeshi la Polisi.
Kongola alidai washtakiwa hao walifanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 124 cha Sheria ya 
Kanuni ya Adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Alidai katika shtaka la pili washtakiwa hao wakiwa eneo hilo hilo, walifanya mkusanyiko usio 
halali kwa lengo moja la kutembea kwenda kwenye Ofisi ya Rais huku wakijua ni kinyume 
cha sheria.
Wakili  huyo alidai kuwa kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 74 na 75 cha Sheria ya Kanuni 
ya Adhabu, sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Baada ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka yao walikana kuhusika na tuhuma hizo. 
Upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika hivyo waliiomba 
mahakama kupanga tarehe ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH).
Hakimu Kaluyenda alisema ili washtakiwa wawe nje kwa dhamana wanatakiwa kila mmoja 
asaini bondi ya sh. milioni 1  kuwa na wadhamini wawili ambapo mmoja kati yao awe 
anafanyakazi katika taasisi inayotambulika kisheria.Mdhamini huyo awasilishe barua kutoka 
kwa muajiri wake na kitambulisho cha kazi.
Upande wa Mashitaka umeiomba mahakama kuwapa nafasi ya kwenda kukagua nyaraka za 
dhamana zilizowasilishwa na wadhamini wa washtakiwa hao.
Hakimu ameiahirisha kesi hadi Oktoba 21, 2014 itakapokuja kwaajili ya washtakiwa hao 
kusomewa maelezo ya awali.

ORIFLEM YATOA MSAADA KATIKA SHULE YA MSINGI ALIYOSOMA BALOZI WA KAMPUNI HIYO " LADYJAYDEE" BUGOYI ILIYOPO MKOANI SHINYANGA


Meneja Mkazi wa Oriflame Tanzania, Fortunata Nkya akifungua sherehe hiyo.

 
Wanachama wakiwemo wageni wakisikiliza kwa mkini jinsi Oriflem ilivyojipanga katika kusaidia jamii ikiwemo wanachama wake.

MD wa Oriflem Tanzania, Klas Kronass akizungumza na wageni pamoja na wanachama, alisema kuwa Oriflem Tanzania imefanya vizuri sana mwaka huu katika kazi zake na pia kuwapongeza wanachama kwa kufikia hatua ya pili Africa,


Balozi wa Oriflem Tanzania LadyJaydee akikabidhiwa maua na kisura wa Oriflem Africa ambaye pia ni kiongozi  Jesca Nisege kwa kazi nzuri anayoifanya.

MD Klas Kronass akikabidhi hundi kwa Mwl wa fya wa Shule ya msingi Bugoyi "Mwl Stephani Nitaudimra" iliyopo Mkoani Shinyanga, 

Balozi wa Oriflem Tanzania Lady jaydee akitoa shukurani kwa viongozi na wanachama. 

Mwl Stephania Nitaudimara akitoa shukurani za dhati kwa Oriflem, lisema "Nawashukuru sana Oriflem kwa msaada huu mkubwa kwani tumekuwa na shida kubwa ya vyoo shuleni Bugoyi" Picha na matukio (www.nkema.blogspot.com)



Tuesday, 7 October 2014

MSHIRIKI BBA TANZANIA HUYU HAPA

Mrembo huyu ambaye ameshawahi kuingia 10 bora ya shindano la Miss Tanzania mwaka 2012, baada ya kutwaa taji la Miss Lindi 2012,…

















Irene Neema Vedastous ‘La Veda’, Mshiriki wa Big Brother Hotshots kutoka Tanzania.
IRENE NEEMA VEDASTOUS ni msichana mrembo wa Kitanzania, mwenye umri wa miaka 23 anayeiwakilisha Tanzania katika shindano la BIG BROTHER 2014 ‘HOTSHOTS’ nchini Afrika Kusini.
















La Veda katika pozi na baadhi ya mastaa.
Mrembo huyu ambaye ameshawahi kuingia 10 bora ya shindano la Miss Tanzania mwaka 2012, baada ya kutwaa taji la Miss Lindi 2012, anaingia rasmi leo tarehe 5 Oktoba 2014 kwenye shindano hilo lenye mashabiki
wengi duniani ambalo kuanzia saa 1 jioni litakua likirushwa live kupitia DSTV kwenye channel no. 198.
Irene Neema Vedastous aka Irene La Veda ni nani?
Irene La Veda, sio mrembo mpya kwenye jamii ya Watanzania kama wengi wanavyodhani, ni mrembo anayependa kujichanganya na watu mbalimbali. Hii hali imemuwezesha kufanya vitu mbalimbali na
vikubwa kwenye fani mbalimbali kama filamu, muziki, urembo, mitindo, nk.
FILAMU (BONGO MOVIES): Amecheza filamu mbalimbali ambazo nyingine zipo sokoni na nyingine bado hazijaingia mfano; KITENDAWILI, aliyofanya na msanii Rich Rich tayari ipo sokoni, LOVE IN A MESS
aliyocheza na Msungu. Mrembo huyo, pia amecheza filamu na magwiji kama King Majuto, Mzee Magali, Hashimu Kambi na Mzee Chilo ambapo filamu hizo walizocheza zitaingia sokoni hivi karibuni na zote
La Veda amecheza kama mhusika mkuu ‘Main Character’.



























La Veda akiwa kazini.
MUZIKI: Kwa upande wa muziki, La Veda ni mkali sana wa kucheza na tarumbeta. Hii ni nadra sana kukutana na mwanamuziki ambaye anauwezo wa kupiga kifaa japo kimoja cha muziki.
Mrembo La Veda sio tu mkali wa kupuliza tarumbeta bali ameshatoa vibao mbalimbali kama UTANIMISS, SIMPLE LOVE, LET IT GO, na kibao kikali kinachotamba kwenye mitandao mbalimbali, kibao
ambacho kinaitangaza Tanzania katika sekta ya utalii kiitwacho TWENDE TUKATALII , Video ya wimbo huu inapatikana You tube.

Video ya wimbo wa La Veda, Twende Tukatalii. UCHEZAJI DANSI: Mshiriki huyo ni dansa mzuri na umahiri wake tayari ameuonyesha katika video zake alizofanya pamoja na kazi nyingine za muziki alizofanya hapa Tanzania na nje ya nchi zikiwemo
Uswiss na Ufaransa.
MITINDO NA UREMBO: Licha ya kuwa Miss Lindi 2012, La Veda ni mwanamitindo ambaye tayari ameshafanya ‘events’ mbalimbali za mitindo mojawapo ikienda kwa jina LA VEDA SHOW.
Irene La Veda ambaye hasiti kusema ‘Role Model’ wake ni Mama yake Mzazi, moja ya mipango yake ni kuona anafika mbali kisanaa, hivyo aliamua kwenda kukaa darasani kwenye Chuo Cha Sanaa
Bagamoyo mwaka 2012 kuongeza ujuzi na utaalamu katika fani hiyo.



















La Veda (wa kwanza kulia) akiwa na baadhi ya washiriki wa Miss Tanzania 2012.
Mama Mzazi wa La Veda, Mecky Sebastian anasemaje kuhusu mwanaye kushiriki Big Brother Hotshots? msikie hapa;
“Naomba akina mama wenzangu, wasanii na Watanzania wote kwa ujumla mnisaidie katika kumuunga mkono La Veda ili aweze kuiletea heshima nchi yetu na yeyote popote alipo mwenye kuitakia mema
Tanzania na Afrika Mashariki tumpe ‘support’ ya kutosha ili aweze kuibuka mshindi. Nawatakia Watanzania kila la kheri kwenye shughuli zao za maendeleo”, alisema Mama Mzazi wa La Veda, Mecky Sebastian.