Waziri wa ujenzi, Dk. John Magufuli akielezea jinsi wizara yake ilivyojipanga kuhakikisha kuwa malengo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni unaofadhiliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), inafikiwa na kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam. Rais Kikwete alitembelea mradi huo pamoja na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa nyumba za garama nafuu zilizopo Kijichi Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dk. Ramadhan Dau (wa pili kulia) akimweleza jambo Rais Jakaya Kikwete wakati wa ziara ya rais kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni ambayo inafadhiliwa na NSSF, pamoja na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa nyumba za garama nafuu zilizopo Kijichi Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete akiongea na wahusika wa ujenzi wa daraja la Kigamboni inayofadhiliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Waziri wa ujenzi, Dk. John Magufuli akielezea jinsi wizara yake ilivyojipanga kuhakikisha kuwa malengo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni unaofadhiliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), inafikiwa na kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam. Rais Kikwete alitembelea mradi huo pamoja na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa nyumba za gharama nafuu zilizopo Kijichi Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete ametembelea daraja la Kigamboni, Dar es Salaam, jana, ambapo ameagiza changamoto zilizoanishwa zitatuliwe haraka kabla mradi haujamalizika. Akizungumza wakati wa kupokea taarifa ya ujenzi huo, Rais Kikwete alisema utekelezaji wa mradi unapaswa kwenda sambamba na utatuzi wa changamoto hizo.
Mapema wakati akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Makamu Mwenyekiti wa Mradi huo, John Msemo, alisema zipo changamoto chache ambazo zinapaswa kutatuliwa kwa ushirikiano na serikali.
Alizitaja changamoto hizo kuwa pamoja na zile za wembamba wa baadhi ya barabara pamoja na msongamano wa magari. Alitoa mfano wa barabara za Vijibweni-Mjimwema, Bendera Tatu-Kamata na Gerezani- Ohio kuwa ni nyembamba.
Pia aliutaja msongamano wa magari katika makutano ya barabara ya Kilwa- Mandela, Chang'ombe-Mandela na Nyerere (Tazara) kuwa unapaswa kushughulikiwa. Akizungumzia suala hilo, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alisema tayari serikali imeanza kushughulikia changamoto hizo, ambapo imeongea na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) pamoja na kutenga fedha katika bajeti kwa ajili ya upanuzi wa barabara hizo.
Dk. Magufuli alisema katika bajeti ya mwaka huu, fedha zimetengwa kulipa fidia kwa ajili ya barabara ya Vijibweni-Mjimwema ili iongezwe upana na kwamba, ile ya Ohio-Gerezani mazungumzo yanaendelea na ADB.
Daraja la Kigamboni linalojengwa kwa ushirikiano wa serikali na wadau na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambapo linatarajiwa kukamilika Juni, mwakani na kuzinduliwa na Rais Kikwete. Baada ya kutembelea mradi huo, Rais alikagua ujenzi wa nyumba 1,120 zilizojengwa na NSSF katika eneo la Mtoni Kijichi, Kigamboni, ambapo aliupongeza uongozi wa shirika hilo kwa kukamilisha mradi huo wa nyumba za watu wa kipato cha kati na chini.
Rais alizindua mradi huo na kuiagiza Manispaa ya Temeke kuangalia uwezekano wa kuijenga vizuri barabara inayokwenda mahali nyumba hizo zilipo pamoja na kutengeneza miundombinu nyingine muhimu ikiwemo maji. Mapema wakati wa ziara hiyo, Rais ambaye alisherehekea siku yake ya kualiwa jana, alikabidhiwa kadi maalumu ya kumtakia maisha marefu na Mkurugenzi Mkuu wa Nssf, Dk. Ramadhan Dau.
No comments:
Post a Comment