Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsifia Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Lukuvi kwa uchapakazi wake mzuri wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Magozi, Kata ya Ilolo Mpya, Iringa Vijini leo. Kinana alimjia juu Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu kwa kushindwa kutafutia ufumbuzi migogoro ya wananchi.Pia aliwataka wananchi kuacha kukwepa majukumu yao ya kuwatumikia Wananchi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye akihutubia katika mkutano huo
Kinana akisalimiana na wananchi alipowasili kushiriki ujenzi wa jengo la CCM tawi la Luganga Kata ya Ilolo Mpya.
Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana na Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Lukuvi wakishiriki kufyatua tofali za ujenzi wa jengo la Ofisi ya CCM.
Kinana na Lukuvi wakisaidia kufyatua tofali za kujengea jengo hilo la CCM
Wanachama wa CCM Shina namba 6 katika Kijiji cha Magozi, Kata ya Ilolo Mpya wakicheza kwa furaha wakati Kinna alipofika kuzungumza nao
Kinana akizungumza na wananchama wa shina hilo. Kulia kwake ni Balozi wa shina hilo Chengula Mlula
Kinana na Lukuvi wakitoka kukagua ujenzi wa Zahanati ya Magozi Kata ya Ilolo Mpya, Isimani
Kinana na Lukuvi wakijadiliana jambo baada ya kukagua ujenzi huo
Wamasai wakiingia kwenye mkutano kutumbiza kwa ngoma ya asili
Wasanii wakicheza ngoma ya asili ya kabila la wasukuma
Lukuvi akimkabidhi kompyuta na mashine ya kudurufia Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Pawaga Charles Mgimwa kwa ajili ya matumizi ya shule
Mgimwa akifurahia msaada huo
Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, Amina Imbo (kushoto) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa UWT wa wilaya hiyo, Shakila Kiwanga wakati wa mkutano huo
Mbunge wa Jimbo la Isimani, ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi akielezea miradi inayyotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM jimboni humo.
Mmoja wa wananchi akiuliza swali kwa Katibu Mkuu Kinana kuhusu mgogoro wa ardhi wa wanakijiji na Jeshi la Magereza.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Dk. Beatrice Ishengoma akijibu swali hilo ambapo alisema kuwa kwa asilimia kubwa wamelitafutia ufumbuzi na kwamba kilichobaki ni wizara husika kwenda kupima na kuweka alama za mipaka.
No comments:
Post a Comment