TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Monday, 27 October 2014

Montage, SOS Childrens Village Tanzania, wafikia lengo Chakula cha Usiku mjini Zanzibar

Bango la wadhamini kwa ajili ya kuchangia yatima wa SOS Childrens Village Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa SOS Childrens Village Tanzania, Anatori Rugaimukamu, akitowa maelezo wakati wa hafla hiyo ya chakula cha usiku kuchangia Watoto wa SOS na wenye mazingira magumu Tanzania, hafla hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na Kampuni ya Montage na SOS na kufanyika viwanja vya Hoteli ya Serena Inn mjini Zanzibar.


Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Tanzania, Bi. Teddy Mapunda akizungumza katika hafla hiyo na kutoa maelezo ya malengo ya chakula hicho, cha usiku kwa wafanyabiashara waliohudhuria hafla hiyo na kutoa malengo kiasi cha fedha zinazohitajika kutokana na michango hiyo, kuwa kiasi cha sh. milioni 200, kusaidia watoto yatima wa SOS na wanaoishi katika mazingira magumu.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya SOS Zanzibar, Bw. Mohammed Baloo, akizungumza katika hafla hiyo ya kuchangia fedha kwa ajili ya watoto wa SOS na walio katika mazingira magumu. 

Mtoto Tatu Haji Machano, shuhuda aliyelelewa katika Kijiji cha SOS Mombasa, mjini Zanzibar akitoa maelezo katika hafla ya chakula cha usiku ili kuwachangia watoto wa SOS, jinsi alivyopata malezi katika kijiji cha sos mombasa. hadi kupata elimu ya Juu. 

Mtoto Mgeni Ali Ameir, shuhuda aliyelelewa katika Kijiji cha SOS mombasa Zanzibar akitowa maelezo katika hafla ya chakula cha usiku ili kuwachangia watoto wa SOS, jinsi alivyopata maelezo hadi kupata elimu ya Juu katika vyuo vikuu ndani ya tanzania na nje ya nchi kwa sasa ni Ofisa katika jumuiya ya kijamii akitumia elimu yake. aliyoipata kupitia SOS. kwa sasa ni mama wa familia.


Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni Utalii na Michezo Mhe. Bihindi Hamad, akizungumza wakati wa hafla hiyo, ambapo pia alimkaribisha Makamu wa Rais wa Tanzania,  Dk. Mohamed Gharib Bilal kuzungumza.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya chakula cha usiku kilichoandiliwa na Kampuni ya Montage, kwa ajili ya kuchangia watoto yatima wa SOS Childrens Village Tanzania, kilichofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Serena Inn, mjini Zanzibar na kuwashirikisha wafanyabiashara na Makampuni ya Umma Tanzania.


Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Kijiji cha SOS Zanzibar, wakifuatilia hafla hiyo, maalum ilioandiliwa kwa ajili ya kuchangia watoto wa SOS na wenye mazingira magumu,  wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dk. Bilal alipokuwa akihutubia katika hafla hiyo.


Wafanyakazi wa SOS Childrens Village Tanzania wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa hafla ya chakula cha usiku kilichofanyika katika viwanja vya hoteli ya serena inn Zanzibar. 

Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Ghari Bilal akipokea mfano wa cheki kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Ultimate Security Tanzania Bi.Jacqui Bothma, ikiwa ni mchango wao kuwachangia Watoto SOS Childrens Village Tanzania, wakatika wa hafla ya chakula cha usiku kuchangia watoto hao.kilichofanyika katika viwanja vya hoteli ya serena inn Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Ghari Bilal akipokea mfano wa cheki kutoka kwa Meneja wa Hoteli ya Serena Inn Zanzibar ikiwa ni mchango wao kuwachangia Watoto SOS Childrens Village Tanzania, wakatika wa hafla ya chakula cha usiku kuchangia watoto hao.


Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akiungana na Wafanyabiashara katika hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa na Kampuni ya Montage na SOS kwa ajili ya kuchangia Watoto wa SOS na walioko katika mazingira magumu, hala hiyo imefanyika katika viwanja vya hoteli ya Serena Inn Zanzibar.


Maofisa wa ZSSF wakiwa katika hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa ajili ya kuchangia Kijiji cha SOS kwa Watoto walioko katika mazingira magumu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Tanzania, Bi.Teddy Mapunda, akipeana mkono na Makamu wa Rais, Dk. Bilal, alipokuwa akiinadi picha yake, wakati wa chakula hicho.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Tanzania, Bi. Teddy Mapunda, akiinadi picha ya Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Tanzania, Bi. Teddy Mapunda (katikati), akiinadi picha ya Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Bi. Teddy Mapunda akinadisha picha ya Makamu wa Rais Tanzania, Dk. Gharib Bilal (wapili kulia), iliochorwa na watoto wa SOS, katika wa hafla ya kuchangia iliofanyika viwanja vya Hoteli ya Serena Inn Zanzibar. Picha hiyo iliuzwa kwa sh. 200, katika mnada huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi wa kijiji cha kulelea watoto yatima cha SOS Zanzibar wakati wa ghafla ya kuchangisha mfuko wa kuendeleza watoto yatima wa kijiji cha SOS Zanzibar  iliyofanyija jana usiku Octoba 24-2014 katika ukumbi wa Serena Hotel, Jumla ya shilingi milioni 201 zilizokuwa zikihitajika zilichangishwa.




Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal akimkabidhi picha ya kuchora ya sura yake, iliyochorwa na Watoto wa SOS, baada ya kuinunua Mkurugenzi wa Kampuni za Turky, Tofik Salim Turky kwa thamani ya sh. milioni 2, wakati wa hafla ya chakula cha usiku kuchangia watoto wa Kijiji cha SOS. 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage, Bi. Teddy Mapunda akiinadi picha ya Rais wa Zanzibar, Dk. Shein, iliochorwa na Watoto wa SOS Children Village, wakatika wa hafla ya kuchangia iliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Serena Inn mjini Zanzibar. Picha hiyo iliuzwa kwa sh. milioni moja na laki tatu.


Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mahomed Gharib Bilal akimkabidhi picha ya kuchora ya Rais wa Zanzibar Dk. Shein, iliochorwa na Watoto wa SOS, Baada ya kununuliwa na PBZ kwa thamani ya shilingi milioni moja na laki tatu kwa Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa PBZ, Seif Suleiman.


Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal akimkabidhi cheti Ofisa wa Bank Kuu ya Tanzania (BOT), Tawi la Zanzibar Ndg. Nicodemis Mboje, kwa ajili ya kuchangia watoto wa SOS Childrens Villages Tanzania. Katika hafla hiyo zaidi ya Sh. milioni 200.9, zilipatikana.


Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akimkabidhi cheti 
Meneja Masoko wa Precision Air, Azda Amani ikiwa ni shukrani kwa kuwa moja ya kampuni zilizodhamini hafla hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na Kampuni ya Montage na SOS Children Village, Hoteli ya Serena mjini Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi wa kijiji cha kulelea watoto yatima cha SOS Zanzibar pamoja na waliochangia kwa namna moja ama nyingine, wakati wa ghafla ya kuchangisha mfuko wa kuendeleza watoto yatima wa kijiji cha SOS Zanzibar  iliyofanyija jana usiku Octoba 24-2014 katika ukumbi wa Serena Hotel, Jumla ya shilingi milioni 201 zilizokuwa zikihitajika zilichangishwa. (Picha zote kwa hisani ya Othman Maulid wa ZanziNews)

No comments:

Post a Comment