TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Tuesday, 7 October 2014

ZANZIBAR,MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR OTHMAN MASOUD OTHMAN AFUTWA KAZI.

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman.
RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, leo amemfuta kazi Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman na nafasi yake kuchukuliwa na Said Hassan Said.
Rais Shein amefanya uteuzi huo wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 55 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984.
Mhe. Said Hassan Said ameteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na uteuzi huo umeaza rasmi leo 7, Oktoba 2014. Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu.
Uteuzi wa Mhe. Othman Masoud Othman umefutwa kwa mujibu wa Vifungu vya 53,54 (1) na 55 (3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kifungu 12 (3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.

Sunday, 5 October 2014

BABA,MAMA NA WATOTO WAPOTEZA MAISHA SABABU NI JENERETA

Mwili wa mama, na wa mmoja wa watoto unaonekana kwa mbali nyuma yakeMume, mke na watoto wao watatu wamefariki dunia baada ya kupumua hewa iliyojaa gesi ya “carbon monoxide” iliyokuwa ikitolewa na generator waliloliwasha ndani ya nyumba yao .
  

Katika dhahama hiyo iliyotokea Lagos, Nigeria, miili ya wahanga wote watano iligunduliwa na majirani zao. Majirani wameripoti kuwa baba wa familia hiyo alinunua generator siku mbili kabla ya kukutwa na umauti, na kuliweka chumbani kwake akihofia kuwa litaibwa akiliweka nje.
Siku iliyofuatia, majirani waligundua kuwa wanafamilia hao wote walikuwa kimya, na ndani ya nyumba yao siku nzima, hivyo mmoja wao akaamua kuangalia kujua kinachoendelea. Jirani huyo aliona miili ya marehemu, na kuwataarifu wenzake. Walipoingia ndani ya nyumba, walistushwa na janga walilokutana nalo.
Katika moshi unaotolewa na majenereta, kama wa mkaa, magari, pikipiki, na mashine nyingi, kuna gesi ya “carbon monoxide (CO)” ambayo, ni sumu inayokusababisha kuchoka, kupoteza fahamu, na hatimaye kufariki taratibu bila onyo, maumivu, wala kujijua. Utadhani unapata usingizi na kujilaza, kumbe ndio mauti yanakukuta. Uthithubutu kupika kwa kutumia mkaa ndani ya nyumba bila kufungua madirisha, au kuwasha jenereta ndani ya nyumba, au kuwasha gari katika “garage” wakati madilisha na milango imefungwa; maana hiyo ni sawa na kucheza na kifo. Gesi ya carbon monoxide ni tofauti na carbon dioxide (CO2) inayopumuliwa na wanyama, ambayo si sumu na inatumiwa na mimea katika photosynthesis.
Miili ya watoto watatu wa familia hiyo

Saturday, 4 October 2014

DODOMA,RAIS KIKWETE ATEMBELEA CHUO CHA SAYANSI YA AFYA UDOM.

 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunga rasmi Kikao cha kazi cha viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri nchini katuika ukumbi wa Chimwaga katika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dodoma.
 Mhe. Baraka Konisaga, ambaye ni Mjumbe wa Kikao cha kazi cha viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri nchini akitoa rais binafsi muda mfupi kabla Rais Jakaya Mrisho Kikwete hajafunga rasmi kikao hicho cha siku tatu kilichojumuisha wajumbe zaidi ya 900 kuzungumzia sekta ya elimu ili  kupanga mikakati na kutatua changamoto zinazoikabili, katuika ukumbi wa Chimwaga katika Cho Kikuu cha Dodoma mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Shaaban Mlacha na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (tai nyekundu) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Sayansi ya  Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitovo hicho kianzi kazi rasmi hivi karibuni.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa sehemu mbalimbali na  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dododma Profesa Shaaban Mlacha (mbele) na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (kulia) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitovo hicho kianzi kazi rasmi hivi karibuni.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maelekezo kwa  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Shaaban Mlacha na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (tai nyekundu) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitovo hicho kianzi kazi rasmi hivi karibuni.
Jengo kuu la  Chuo  cha Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha Chuo Kikuu cha Dodoma  mjini Dodoma 
 Sehemu ya majengo ya Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu ya UDOM
 Sehemu ya barabara ya lami ya kutoka na kuelekea vyuo mbalimbali vya UDOM

Friday, 3 October 2014

MKURUGENZI WA GLOBAL PUBLISHER ERIC SHIGONGO AZINDUA VITABU VYAKE VIPYA MAREKANI



Vitabu viwili vya Eric Shigongo alivyozindua nchini Marekani juzi.
 Eric Shigongo akihojiwa na Shaka Ssali (kulia) katika kipindi cha Straight Talk Africa kabla ya uzinduzi huo. 
MKURUGENZI Mtendaji wa Global Publishers, Eric James Shigongo amezindua vitabu vyake viwili vipya…
Vitabu viwili vya Eric Shigongo alivyozindua nchini Marekani juzi.
 Eric Shigongo akihojiwa na Shaka Ssali (kulia) katika kipindi cha Straight Talk Africa kabla ya uzinduzi huo. 
MKURUGENZI Mtendaji wa Global Publishers, Eric James Shigongo amezindua vitabu vyake viwili vipya vya namna ya kuondokana umaskini vyenye majina ya 10 Laws-How to Move From Poverty to Prosperity na 26 Secrets- How to Defeat From Enemies and Make Millions of Dollars.
10 Laws-How to Move From Poverty to Prosperity.
Shigongo alizindua vitabu hivyo vya ujasiriamali alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Runinga cha Voice of America (Voa) kwenye Kipindi cha Straight Talk of Africa nchini Marekani juzi.
26 Secrets- How to Defeat From Enemies and Make Millions of Dollars.
Kwa mujibu wa Shigongo vitabu hivyo vitakuwa vikiuzwa duniani kote ili kuikomboa jamii kwenye wimbi la umaskini.(Habari na picha kwa hisani ya Global Publisher)

JESHI LA POLISI WAKAMATA SAMAKI WENYE SUMU BAHARI YA HINDI NA KUWATEKETEZA

Askari polisi na JWTZ wakiangalia samaki hao. 
Askari wa Jeshi la Wananchi Tanazania (JWTZ) , Kikosi cha Wanamaji (Navy), wakiandaa samaki waliowakamata baada ya kuvuliwa kwa kutumia baruti katika Bahari ya Hindi Dar es Salaam Oktoba 2-2014.


Samkai hao wakiandaliwa tayuari kwa kuteketezwa kwa moto.

 Samaki hao wenye sumu ya baruti.


Askari wa JWTZ wakiwa wamewabeba samaki hao wakiwapeleka kuwateketeza.


 Askari wa JWTZ akiweka majani makavu tayari kwa kuwateketeza samaki hao.

Samaki hao wakiteketezwa kwa moto.

Thursday, 2 October 2014

UMOJA WA VYUO VYA USAFIRI WA ANGA BARANI AFRIKA(AATO)TANZANIA YAWA MWENYEJI MKUTANO MKUU WA KWANZA


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi , Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Mbwana . J. Mbwana akisalimiana na Rais wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika(AATO) Tchagbele Sadamba  wakati wa  mkutano mkuu wa kwanza wa AATO  unaofanyika Zanzibar   kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha  mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi  Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) 
04Baadhi ya wataalamu wa sekta ya  Usafiri wa Anga toka nchi ya Senegal  wakifuatilia kwa karibu mkutano  mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika( AATO) unaofanyika mjini  Zanzibar  kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha  mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Mbwana.  J. Mbwana (katikati)   akiwasikilza  wajumbe wa mkutano  wa AATO , baada ya kufungua mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika( AATO) unaofanyika mjini  Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha  mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika. Wengine  kutoka kushoto ni  mjumbe wa Bodi TCAA,  Yussuf . M. Ali, Mkurugenzi  Idara Udhibiti  Uchumi , TCAA, Dkt. James Diu , Rais wa AATO Tchagbele Sadamba  na   Mjumbe wa Bodi TCAA. Hanif.  M. Malik06Mkurugenzi  Idara ya Udhibiti Uchumi(TCAA) Dkt. James Diu , akitoa hotuba kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo Vya Usafiri wa Anga Barani Afrika(AATO)  unaofanyika mjini  Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.07 Mgeni  rasmi  wa mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika, Mbwana J. Mbwana (watano kutoka Kulia) akiwa  kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa baraza  la  Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika( AATO) unaofanyika mjini  Zanzibar  kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha  mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.08Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,  Dkt.  Shabaan Mwinjaka(Kushoto) akifuatilia  moja ya mada zilizokuwa zikitolewa kwenye  mkutano  mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika( AATO)  unaofanyika mjini  Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha  mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.

ORIFLAME YATOA AJIRA 60,000,PIA YAZINDUA BIDHAA MPYA JANA TAREHE 01 OCT2014

Mkurugenzi Mwandamizi wa Kampuni hiyo, Japhet Naftal (kulia), akifungua mkutno kwa makofi maalumu ya Oriflame katika hafla hiyo ya kutangaza bidhaa mpya za Kampuni hiyo iliyofanyika katika ofisi zao Dar es Salaam jana jioni zilizopo Posta Mpya ghorofa la Benjamin William Mkapa Towers Mezzanine Floor..

 Meneja Mkazi wa Oriflame Tanzania, Fortunata Nkya (kulia), akizungumza na wanachama wa kampuni hiyo kuhusu bidhaa mpya na mipango ya miezi mitatu ya kampuni hiyo. Moja ya bidhaa mpya iliyonadiwa na kutangazwa ni The One Make -Up sanjari na kuzindua kitabu chenye bidhaa mbalimbali za urembo kiitwacho Your Dreams-Our Inspiration kitakacho kuwa sokoni kuanzia jana  Oktoba 1 hadi Desemba 31-2014.

Viongozi wa Kampuni hiyo wakitambulishwa kwa wanachama. Kutoka kushoto ni Jesca Nisege, Meshack Wayanje, Julieth Msofe, Clara Wekwe, Christina Basil, James Mwangamba na Nasra Mohamed.

Wanachama wa Oriflame Tanzania wakimsikiliza kwa makini Meneja Mkazi, Fortunata Nkya wakati akielezea mambo mbalimbali ya kampuni hiyo.

Warembo wa Oriflame wakiwa katika sura ng'avu baada ya kutumia vipodozi vinavyosambazwa na kampuni hiyo hakika wanapendeza,  wakina mama nunueni vipodozi vya Oriflame ili mpendeze kama akina dada hawa. Kutoka kushoto ni mrembo Monica Mhando, Zainabu Ali na Suhaila Abdallah.
Ofisa Mwandamizi wa Oriflame Tanzania, James Mwangamba akihojiwa na wanahabari hapo anaelezea mafanikio makubwa yaliyofikiwa na kampuni hiyo.


KAMPUNI ya Oriflame Tanzania inayouza vipodozi asilia imetoa ajira kwa vijana 60,000 wa kitanzania kwa kusambaza na kuuza bidhaa zake.Hayo yalibainishwa na Meneja Mkazi wa Oriflame Tanzania, Fortunata Nkya wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana katika hafla ya kutangaza bidhaa mpya na uzinduzi wa kitabu chenye bidhaa mbalimbali za urembo kiitwacho Your Dreams-Our Inspiration kitakacho kuwa sokoni kuanzia  Oktoba 1 hadi Desemba 31-2014.
"Tangu tuanzishe kampuni hii mwaka 2011 tumefanikiwa kutoa ajira kwa vijana 60,000 jambo ambalo tunajivunia ukizingatia changamoto kubwa ya uhaba wa ajira" alisema Nkya.Alisema vijana hao wamekuwa wakijipatia zaidi ya sh. milioni 10 kwa mwezi kutokana na kufanya biashara ya bidhaa zetu kwa mfumo wa moja kwa moja.Nkya alisema kampuni yenye makao yake makuu nchini Sweden  kila baada ya miezi mitatu  inaingiza bidhaa mpya sokoni ili kutoa fursa kwa wateja wao kuzipata kwa urahisi na kuzisambaza kila kona kupitia mtandao wa vijana waliopo katika makundi.Aliongeza kuwa bidhaa nyingi ni vipodozi asilia vinavyotumika kwa wanaume na vingi zaidi ni kwa ajili ya wanawake.Nkya alitumia nadfasi hiyo kuwahamasisha wanawake kote nchini kununua vipodozi kutoka Oriflame Tanzania kwani havina kemikali yoyote ni bora na salama kwa mtumiaji kwa wakati wote.

Meneja huyo mkazi alisema kama atahijai ufafanuzi kuhusu namna ya kuzipata bidhaa zao anaweza kufika katika ofisi ya Oriflame iliyopo ghorofa la Benjamin William Mkapa Towers Mezzanine Floor.Imeandaliwa na mtandao wa (www.nkema.blogspot.com) na Getrude Edwrd.


x