TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Sunday, 5 October 2014

BABA,MAMA NA WATOTO WAPOTEZA MAISHA SABABU NI JENERETA

Mwili wa mama, na wa mmoja wa watoto unaonekana kwa mbali nyuma yakeMume, mke na watoto wao watatu wamefariki dunia baada ya kupumua hewa iliyojaa gesi ya “carbon monoxide” iliyokuwa ikitolewa na generator waliloliwasha ndani ya nyumba yao .
  

Katika dhahama hiyo iliyotokea Lagos, Nigeria, miili ya wahanga wote watano iligunduliwa na majirani zao. Majirani wameripoti kuwa baba wa familia hiyo alinunua generator siku mbili kabla ya kukutwa na umauti, na kuliweka chumbani kwake akihofia kuwa litaibwa akiliweka nje.
Siku iliyofuatia, majirani waligundua kuwa wanafamilia hao wote walikuwa kimya, na ndani ya nyumba yao siku nzima, hivyo mmoja wao akaamua kuangalia kujua kinachoendelea. Jirani huyo aliona miili ya marehemu, na kuwataarifu wenzake. Walipoingia ndani ya nyumba, walistushwa na janga walilokutana nalo.
Katika moshi unaotolewa na majenereta, kama wa mkaa, magari, pikipiki, na mashine nyingi, kuna gesi ya “carbon monoxide (CO)” ambayo, ni sumu inayokusababisha kuchoka, kupoteza fahamu, na hatimaye kufariki taratibu bila onyo, maumivu, wala kujijua. Utadhani unapata usingizi na kujilaza, kumbe ndio mauti yanakukuta. Uthithubutu kupika kwa kutumia mkaa ndani ya nyumba bila kufungua madirisha, au kuwasha jenereta ndani ya nyumba, au kuwasha gari katika “garage” wakati madilisha na milango imefungwa; maana hiyo ni sawa na kucheza na kifo. Gesi ya carbon monoxide ni tofauti na carbon dioxide (CO2) inayopumuliwa na wanyama, ambayo si sumu na inatumiwa na mimea katika photosynthesis.
Miili ya watoto watatu wa familia hiyo

No comments:

Post a Comment