Rais wa shilikisho la filam nchini'Bongo Movie' Simon Mwakifambo (wapili kushoto mwenye full Jins) akiwa nje ya kanisa na baadhi ya sanii wa filam nchini
Wasanii
Jasmini Emiry [kulia] Asha Boko[kati] na mke wa mzee Mjuto Rehema
Majutoa wakiwa kwenye ibada ya kumuombea marehemu Sherry iliyofanyika
jana jioni katika kanisani kuu la Mtakatifu Patriki Morogoro.
Bi,Flora
Msiba ambaye ni askali polisi kituo kikuu cha polisi Morogoro akiaga
kwa uchungu mwili wa mepndwa mtoto wake wa kwanza Sherry
Afande Flora akimpiga busu la mwisho mtoto wake huyo kipenzi
Mdogo huyo wa marehemu aliamua kurejea kwa mara ya pili kumuaga dada yake
Msanii Tausi akimuaga msanii mwenzake kwa uchungu
Tausi akizidi kumlilia Sherry
Tausi akisaidi kutoka kanisani baada ya kuaga
Msanii Tunu Mgoranzi akiangua kilio kwa uchungu
Msanii Tunu akitoka kanisani na pacha wake baada ya kuaga
Shosti mkubwa wa marehemu Sherry msanii Mahinda akiangua kilio baada ya kuaga mwili wa rafiki yake kipenzi
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie mkoani Morogoro wakishiriki kwenye ibada hiyo
Umati wawatu uliofulika kanisani hapo
Mwili wa marehemu Sherry ukitolewa kanisani baada ya lbada kumuombea kukamilika
Afande Flora akisaidiwa kutoka kanisani
Mwili wa Sherry ukipakiwa kwenye gari tayari kwa safari ya kueleka kwenye nyumba yake ya milele makabuli ya Kolla
Rais wa bongo Movie akiwaongoza waombolezaji kueleka makabuli ya Kola
Marehemu Sherry enzi za Uhai wake.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
MSIBA
wa msanii Sherry Choka,maarufu Sherry Magali umetawaliwa na vituko
kibao,baba mzazi mzee Salim Choka na baba wa hiyari mzee Charles Magali
waingia mitini mziba wa mtoto wao Mama mzazi Afande Flora Msiba awatosa
wazazi hao na kuamuakuandika jina la baba yake Mzee Msiba Edward kwenye
Msalaba wa mpendwa mtoto wake.
Kama
kawa baada ya vituko hivyo Mwandishi wa mtandao huu alimtafuta msemaji
wa familia hiyo Kulwa Choka ambapo alikiri kuwepo kwa vituko hivyo.
”
Nikweli baba yetu mzee Choka yuko Tunduma hakuweza kufika kwenye msiba
wa mwanae na kwamba amepiga simu nakumpa madalaka yote babu yetu mzee
Msafiri Ngedele ndio maana unaona msiba uko hapa Mji Mpya nyumbani kwa
mzee huyo, pia huyo mzee Magali ambaye watu wanadai ni baba yake Sherry
pia hakufika msibani"alisema Kulwa kwa Jazba na kuongeza kusema
"kuhusu
jina la kwenye msalaba tumekuwa na mvutano wa takribani masaa 4 kwenye
kikao mama wa marehemu alitushangaza kuacha jina la baba wa marehemu
mzee Choka na kung’ang’ania kuandika msalaba jina la baba yake mzee
Msiba Edward ambaye ni babu wa dada yangu sherry kwa upande wa mama
yake,tumeona tusiwape watu faida tumekubali lakini undani zaidi wa
matukio hayo tutakujuza baada ya kumaliza msiba huu”alisema Kubwa Choka
ambaye amechangia baba na marehemu Sherry.
Juhudi
za Mtandao huu za kutaka kuzungumza na Mama mzazi wa Sherry Afande
Flora Msiba zilikwama baada ya mama huyo muda wote kuangulia kilio kwa
kuondokewa na mpendwa mtoto wake juhuzi hizo zinaendele leo na kesho,Pia
juhuzi za Mwandishi wetu kumhoji mzee Choka kwa njia ya simu
zinaendele,
Pekuapekua
ya Mtandao huu imefanikiwakumbana mmoja wa wasanii nyota wa bongo Movie
kutoka Dar ambapo alipoulizwa kwa nini mzee Mgali hakufika kwenye msiba
wa Sherry alisema” Nikweli mzee magari hakufika kwenye msiba wa Sherry
yuko Mwanza kwenye shughuli za kisanii”alisema msanii huyo aliyeomba
hifadhi ya jina lake.
Picha na habair kwa hisani ya Shekidele Blog
No comments:
Post a Comment