Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rashid Makwiro 'Chid Benz'.
MSANII
wa muziki wa kizazi kipya, Rashid Makwiro 'Chid Benz' amekamatwa na
madawa ya kulevya aina ya heroine na bangi akiwa kwenye Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo.
Akizungumza Kamanda wa Kuzuia na Kupambana
na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP, Alfred Nzowa, amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kusema kuwa msanii huyo alikuwa njiani kuelekea
mkoani Mbeya kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki.
Kamanda Nzowa amesema kuwa Chid
amekutwa na madawa hayo baada ya upekuzi wa kawaida uliokuwa ukiendelea
uwanjani hapo, ambapo jeshi la polisi linamshikilia kwa mahojiano na
uchunguzi zaidi.
Mara baada ya kupata taarifa hizo,mtandao huu uliwasiliana na Kamanda Nzoa ambaye alifunguka kama ifuatavyo:
“Ni kweli tumemkamanda Rashid Makwiro
maarufu kwa jina la Chid Benz akiwa na kete kumi na nne za madawa ya
kulevya aina ya heroine pamoja na misokoto miwili ya bangi.
“Msanii huyo alikuwa njiani kuelekea
mkoani Mbeya kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki, na sasa amewekwa
katika sehemu maalum ambayo hatuwezi kusema ni wapi, kwa sababu za
kiusalama, uchunguzi wa tukio unaendelea.”
Taarifa zilizokuwepo awali zilisema
kuwa Chid alikuwa njiani kwenda Mbeya kwa ajili ya kushiriki kwenye shoo
ya Instagram Party ambayo inatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi.
Chid ni kiongozi wa kundi la muziki la la Famila lenye makao makuu Ilala jijini Dar es Salaam.
(HABARI NA NA HARUN SANCHAWA/GPL)
No comments:
Post a Comment