Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal (wa pili kushoto) akikamkabidhi Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom kombe la mujairi bora wa mwaka 2013 ililoshinda Vodacom kutoka Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE).Vodacom ilitangazwa mwajiri bora wa mwaka 2013 wakati wa hafla ya usiku wa waajiri iliyoandaliwa na ATE mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Vodacom.Mbali na kutangazwa mwajiri bora wa mwaka, kampuni hiyo ilishinda pia vikombe vitano katika Nyanja tofauti zinazohusu ajira, usimamizi wa rasilimali watu na masilahi ya wafanyakazi.
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeshinda tuzo ya mwajiri bora wa mwaka 2013 inayotolewa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) baada ya kuyashinda makampuni mbalimbali yaliyoshindanishwa kuwania tuzo hizo.
Mbali na kuibuka mshindi wa jumla katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandiliwa na ATE jijini Dar es salaam na kuongozwa na Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Biala , Vodacom pia imeshinda katika maeneo mengine matano tofauti yanayohusiana na masuala ya uajiri, ajira na usimazi wa rasilimali watu kazini.
“Hakika ni furaha kubwa kwa wateja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000 ni mara ya kwanza kwa kampuni yetu kuweza kutambuliwa kwa kiwango kikubwa kiasi hiki” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza.
Pamoja na kuibuka na Tuzo ya Mwajiri bora wa Mwaka 2013, kampuni hiyo pia imeshinda Tuzo nyingiine tano ambazo ni pamoja na: Best Large Enterprise, Leadership and Governance, Human Resource and Management, Workforce Focus na Best Performance Management Systems.Tuzo hizo zinatambulika na Shirika la Kazi la Kimataifa la Umoja wa Mataifa – ILO ambalo kwenye hafla hiyo liliwakilishwa na Mkurugenzi wake Mkuu Guy Ryder.
Meza aliongeza kwa kusema kuwa, ni heshima na fahari kubwa kwa kampuni yake kuona inaendelea kutambulika siku hadi siku, huku akitanabaisha kuwa tuzo hizo ni chachu kwa kampuni yake kuendelea kupanua huduma na uwekezaji wake nchini, na kuwaendeleza zaidi wafanyakazi ili waendelee kutoa huduma sahihi kwa wateja wa mtandao huo na Watanzania kwa ujumla.
“Tuzo hizi ni kama chachu kwetu kuendeleza, Uwekezaji kwa wafayakazi wetu, wateja wetu, miundombinu katika mtandao wetu, na kwa jamii inayotuzunguka. Tumefanikiwa kufanya mabadiliko makubwa kwa Watanzania kupitia simu, sasa hawaishii tu kupiga na kupokea simu na pia tumewawezesha kutumia simu zao katika huduma mbalimbali za kifedha na kufanya mengine mengi kupitia mtandao wetu,” alisema Meza na Kuongeza.
“Wateja na wafanyakazi wetu ndio nguzo yetu, tutaendelea kuwathamini na kuwaendeleza ili kufikia mafanikio makubwa zaidi ya haya tuliyoyapata leo” alihitimisha Meza
Kutajwa kwa Vodacom kuwa ni mwajirio bora w amwaka 2013 kunakuja siku chache baada ya kampuni hiyo hivi karibuni kutangazwa kuwa ni kampuni ya tatu katika miongoni mwa walipaji kodi wakuu hapa nchini, tuzo iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA Wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mlipa kodi iliyoadhimishwa mwezi uliopita .
No comments:
Post a Comment