TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Wednesday 23 October 2013

KINAMAMA KUNYANYASA WATOTO!!

 

 

 
Picture
Huyu ni mtoto aliyeajiriwa kama mfanyakazi wa ndani na mtoto aliyembeba ni moja ya kazi zake.
Picture
Huyu ndiye mama mwenye nyumba aliyemuajiri huyo mtoto, na kama vile haitoshi huwa anampiga.
 Huko Ubungo-Maziwa jijini Dar es Saalam, kuna ukatili wa kijinsia unaoendelea.

Huwa kuna imani kuwa vitendo vingi vya ukatili vinafanywa na wanaume, ila la hasha hata wanawake nao ni balaa. Sababu
kubwa ya kuamini hivyo ni ile hali ya kuchukulia unaujua uchungu wa kuzaa, unajua hata wewe hutapenda mwanao afanyiwe vitendo ambavyo sio vizuri.

Nimekutana na mama huko Ubungo maziwa akiwa amemuajiri mtoto mdogo wa miaka 8 kama house girl na mbaya zaidi anampiga na kumkatakata. Mtoto ana makovu ya vipigo.
 
 
Kwa undani zaidi kuhusu habari hii, fuatilia kipindi cha Joyce Kiria Wanawake Live ndani ya EATV.

No comments:

Post a Comment