TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Wednesday 23 October 2013

WACHINA WAPORWA NA MAJAMBAZI ML. 135/= WANANCHI KWA KUSHIRIKIANA NA POLISI WAOKOA ML.80

Picture   
 
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP, Athumani Mungi akiwaonyesha raia wa China maburungutu ya fedha zilizonusurika kutoka kwa majambazi waliowateka na kuwapora raia wa China. (picha: Oliver Motto blog)
Mjini Iringa, majambazi waliwateka raia wanne wa China wa kampuni ya SIETCO, inayojenga barabara ya Iringa- Dodoma, wakawapora fedha zaidi ya shilingi milioni 135/-,  fedha za Kichina (yuan), pamoja na vifaa mbalimbali zikiwemo simu tano katika mlima wa Nyang'oro.

Wachina hao walikuwa wemetoka kuchukua fedha katika benki ya CRDB tawi la Iringa kwa ajili ya malipo na mishahara ya
wafanyakazi na vibarua. Walipokuwa njiani kurudi kwenye kambi yao iliyopo Mtera, gari lao aina ya Toyota yenye namba za usajili T. 335 CMX liliwekewa kizuizi na lori kubwa walipofika katika mlima wa Nyang'oro, kisha watu watano wenye silaha wakapora mfuko uliokuwa na fedha.

Polisi na wananchi waliendesha msako wa na baada ya majibizano ya risasi, majambazi yalitupa begi moja lililokutwa na shilingi milioni 80, jingine likiwa na biskuti na vitu vingine vya Kichina. Polisi walimkamata mmoja wa majambazi hayo.

wamefanikiwa kumkatata jambazi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuhofia kuharibu upelelezi  wa kuwasaka majambazi wengine wanne waliofanikiwa kutoroka. 

No comments:

Post a Comment