Aneth Kushaba AK47 na Mary Lucos wakitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya uwanja wao wa nyumbani Thai Village Masaki.
Mashabiki wa Skylight Band wakionekana kukunwa na burudani ya Band hiyo.
Sam Mapenzi akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Sam Mapenzi akimpagawisha shabiki wake.
Hapo sasa twende kazi wewe ni balaaaa….
Aneth Kushaba AK47 akifanya yake jukwaani.
Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa Bongo naye hakubaki nyuma huku akipewa sapoti na Digna pamoja na Mary Lucos.
Shabiki wa Skylight Band aliyeshindwa kujizuia na kuamua kuvua shati na kupanda jukwaani kulisakata Sebene na waimbaji wa Skylight Band.
Wewe usipime burudani Mwanzo mwisho na mashabiki wa ukweli ndani ya Thai Village huku Joniko Flower akiwasebenesha wadau.
Yachuma chuma….mi nataka mukanda Yachuma chuma……mashabiki wa Skylight Band wakicheza Style mpya ya Skylight Band. Njoo wewe na yule ucheze leo usiku pale Thai Village.
Mbali na yote kama kawaida mduara ulichezeka huku Mary Lucos na Joniko Flower wakiongoza burudani hiyo.
Mdau Maurus na best yake walibambwa na camera yetu wakijinioma Kuku choma inayopatikana pale Thai Village ni balaa.
Aneth Kushaba AK 47 na Mdau Maurus wakishow love.
Ben Kinyaiya naye ndani ya nyumba, akishow love na Aneth Kushaba AK 47 aliyeamua kupunguza njaa baada ya kutikisika sana Jukwaani.
Lubeya wa Skylight Band akishow love na msanii Barnaba aliyeambatana na marafiki zake.
Wadau wakipata Ukodak.
Hapa ngumi jiwe tu sogea uoneee….Wadau wakishow love.
Mdau kwenye ofisi kubwa hapa mujini akishow love na Blogger King Kif.
Mpiga solo wa Skylight Band Allen Kisso, Digna na MaryLucos wakipooza koo Back stage.
Na Ijumaa yetu ya wiki iliyopita iliishia hapo kwa kupata hewa safi baada ya kusebeneka na Skylight Band tukutane leo tena kiwanja kile kile.
(Picha na Zainul Mzige)POWERD BY sundayshomari.com
No comments:
Post a Comment