Wanaume hawaoi sura tena bali uelewa…!
Siku
za nyuma, wanaume walijali zaidi uzuri wa sura na mwili wakati walipokuwa
wanatafuta mke. Lakini utafiti uliofanywa duniani kote unaonesha kwamba, wanaume
hivi sasa wamebadili mitazamo na kuanza kuangalia vitu vilivyo zaidi ya uzuri wa
sura na mwili.
Watafiti
kutoka Chuo Kikuu cha Grand Valley kilichopo jimboni Michigan nchini Marekani
walioendesha sehemu kubwa ya utafiti huo wamesema, wanaume hivi sasa wameanza
kujali uwezo wa wanawake katika kufikiri na kujua namna ya kujenga maisha kuliko
kujali sura zao na maumbile.
Tafiti
nyingi, ukiwemo huo wa karibuni wa Chuo cha Grand Valley, zinaonesha kwamba,
kwenye miaka hadi 1980, wanaume walikuwa wakioa wake ambao wanaume hao
wanawazidi kielimu na hata kimapato. Lakini kufikia mwaka 2002, wanaume wengi
walikuwa wameoa wanawake ambao wanawazidi kielimu, kimapato au
kukaribiana.
Lakini
pia imebainika kwamba, hadi kufikia miaka hiyo, wanaume na jamii nyingi zilikuwa
zikimtazama mwanamke anayefaa kuolewa kuwa ni yule mzuri sana kwa sura na umbo.
Lakini kufikia mwaka 2002, wanaume wengi na jamii walikuwa wanaamini kwamba,
mwanamke mwenye uwezo mkubwa wa kuelewa maisha ndiye anayefaa kuwa
mke.
Kwa
miaka ishirini hali imebadilika sana. Maisha yamezidi kuwa magumu na uhitaji wa
watu kusaidiana katika kuyakabili umeongezeka. Kwa hiyo mtu anapofikiria kuoa
huanza kujiuliza atakavyomudu maisha na mke. Kwa hofu za kushindwa, hujikuta
akijiuliza namna atakavyoweza kusaidiana na huyo anayetaka kumwoa katika kufanya
mambo yaende.
Siku
za nyuma, mwanamke mwenye kipato kizuri alikuwa katika ugumu wa kupata mume,
lakini siku hizi, bila kujali sura au sifa nyingine, uhakika wa mwanamke kuwa na
njia za kipato unampa, nafasi kubwa zaidi ya kuolewa. Kilichokuwa kinaogopwa
huko nyuma na wanaume kwa sasa ndicho kinachokimbiliwa.
Tafiti
hizo zinasisitiza kwamba, thamani ya mwanamke kwenye jicho la mwanaume inaanza
kuondoka kwenye uzuri wake wa sura na mwili na kuingia kwenye uwezo wake katika
kuyakabili maisha. Hii ikiwa na maana kwamba, kwa kadiri siku zinavyoenda,
wanawake ambao watakuwa na nafasi kubwa ya kuolewa watakuwa ni wale waliosoma au
wale wenye shughuli za kuzalisha.
Wataalamu
wengi wanasema, hivi sasa uzuri unaonekana kabisa kubadilishana nafasi na elimu
na uwezo wa ‘kutafuta maisha’ wa mwanamke. Kwa hiyo, sasa siyo suala la uzuri
tena, bali mwanamke anajua kitu gani na ana uwezo kiasi gani wa kufanya maisha
yawe bora sana.
Hii
pia ina maana kwamba, dhana ya zamani ya mwanamke mzuri kuolewa na mwanaume
msomi au mwenye fedha imeanza kukosa mashiko. Siku za nyuma mwanamke mzuri sana,
angeolewa na mwanaume mwenye fedha, kama zilivyo bidhaa nzuri kuangukia mikononi
mwa wenye uwezo kifedha.
Lakini
leo hii, wanaume wanachoweza kufanya ni kuwachezea kimapenzi wanawake wazuri na
siyo kuwaoa. Linapokuja suala la kuoa, kisomo na uwezo wa kuyajua maisha
huchukua nafasi. Uzuri wa sura hubaki nyuma kwanza.
BY Utambuzi na Kujitambua
BY Utambuzi na Kujitambua
No comments:
Post a Comment