Wiki moja iliyopita nilisema ntakuwa nashare namna mbalimbali ya kuandaa ratiba ya mlo wa asubuhi,mchana na usiku.Tulianza na mlo wa asubuhi na nikapata maoni ya wale wanaotaka kupunguza uzito je wanaweza kuwa na ratiba ipi?Ifuatayo ni ratiba ya mlo wa asubuhi kwa mtu anaetaka kupunguza mwili/uzito.
JUMATATU
Mkate wa brauni slesi 1 +siagi ya karanga
Yai 1 la kuchemsha
Kinywaji cha soya
Chungwa 1
JUMANNE
Mhogo/kiazi/gimbi kipande 1
Kachumbari-nyanya na kitunguu na tango
Maziwa kikombe 1
Papai
JUMATANO
Sandwich (mkate brauni slesi 2,yai la kukaanga moja,nyanya kitunguu,hoho,tango)
Chai ya maziwa yenye viungo
Tikiti maji
ALHAMISI
Chapati 1 ya unga wa atta (roti-iliyochomwa bila mafuta)
Sausage 1
Kinywaji cha Soya
Parachichi
IJUMAA
Uji wa dona na maziwa/oats na maziwa/all bran na maziwa(kula kimojawapo)
Tikitimaji
JUMAMOSI
Supu ya kuku/samaki/nyama
Chapati 1 ya unga wa atta (roti-iliyochomwa bila mafuta)
Saladi ya matunda
JUMAPILI
Skonzi za atta +cheese/asali/siagi ya karanga
Salad ya mboga mboga(nyanya,tango,kitunguu)
Maziwa kikombe 1
Nanasi
NOTE
· Maziwa yatakayotumika yawe yaliyoenguliwa mafuta yaani skimmed milk,unaweza chemsha na kuondoa mafuta yatakayobaki juu au ukatumia maziwa ya Cowbell.
· Matunda na mboga mboga zitumike za kwenye msimu, mboga na matunda yanayoshauriwa zaidi kwa kupunguza uzito ni spinach, sukuma wiki, lettuce,tango,nyanya,zabibu,chungwa,limao,parachichi,papai,apple,tikitimaji,cauliflower,broccoli,bilinganya,nyanyachungu,bamia,uyoga,zukini na maharage mabichi.
· Tumia unga wa nafaka zisizokobolewa, dona-inga wa mahindi mazima, atta-unga wa ngazo isiyokobolewa
· Roti jina la aina ya chapatti ya Kihindi inayochomwa kwenye kikaango bila mafuta.
· Usile mayai kila siku, yana lehemu, mayai matatu kwa wiki yanatosha.
BY DINA MARIOS
No comments:
Post a Comment