TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Monday, 30 September 2013

MWANAMKE HUSIKA NA USAFI WA NYUMBA YAKO



 Wanawake wengi tunapenda kuonekana nadhifu(smart) tutokapo nje ya nyumba zetu, na kuacha mende wakicheza disco ndani mwetu. Kina mama tujipange tusafishe nyumba zetu ili tuwe na hamu ya kuzitumia,usafi wa kila siku unahitajika sehemu zote.
Kwa wanaokosa muda kabisa, angalau usafi kwa wiki mara moja na uwe usafi wa kuridhisha.



                                            ZINGATIA YAFUATAYO                                                               

1. Funika vitu na vyombo vyote vinavyohusiana na chakula, Funga milango na madirisha yote kisha puliza dawa nyumba nzima
Dawa zinatofautiana kutokana na sehemu na maduka yaliyopo karibu ya maeneo tunayoishi, ila nunua dawa ya kuua wadudu Acha muda upite kama masaa 2, kabla hujarudi ndani ya nyumba.Kisha fungua milango na madirisha yote hewa na harufu vitoke nje, ukiridhika kuwa hali imekuwa shwari unaweza kuanza usafi wa sakafu, madirisha, milango na sehemu zingine zilizojificha zinazo hifadhi uchafu.






2. Wakati unapiga deki either kwa tambara au kwa mop, Yale maji ya kupigia deki hakikisha umeyawekea dawa ya kuua wadudu, unaweza kutumia Dettol au dawa nyingine yoyote ya maji inayopatikana au uliowahi kuitumia ukaona inafaa
Hakikisha maji yamefika sehemu zote muhimu.



3. Usisahau kufuta sehemu zozote ambazo chakula kimemwagika, mezani na kwingineko
Hakikisha matakataka yote unayatupa sehemu sitahili.

ZINGATIA: Usipende kuacha chakula wazi, au kuacha mabaki ya chakula au uchafu wowote uliodondoka bila kuusafisha kila unapomaliza kula
Na taka taka zote zitupwe mbali na nyumba kila siku kabla ya kulala, kwani mende hujitokeza nyakati za usiku.




4.Baada ya kuwa umeridhika na usafi wa nyumba unaweza kuweka manukato ya kufanya nyumba inukie vizuri , Airfreshner zipo za aina nyingi na bei tofauti
Chagua inayokupendezea kwa harufu, tundika au pulizia.



     
Ukifanya hivyo mara kwa mara itapunguza kwa kiasi kikubwa, mende kuitembelea himaya yako.
Jitahidi usiache chakula wala vinywaji vinazagaa bila kufunikwa na vyombo vyote vioshwe kabla ya kulala.

Mungu awabariki.

Sunday, 29 September 2013

DON'T LYING IN BED GO WASH YOUR FACE, THEN COME BACK READ THIS

 1. You have so many things to focus on besides some guy’s neuroses. The more brain space you devote to this bullshit, the less you have left for useful knowledge like basic geometry or getting a raise at work or how to make an awesome grilled cheese-and-avocado sandwich.


2. The single life isn’t as bad as you think. An emotional palate-cleanser between relationships — like spending an hour or two browsing Anthropologie without your ex sitting in a pretty chair at one of the designated Boyfriend Stations and whining about wanting to leave — is fun and essential.

BE CAREFUL WITH THINGS THAT CAN ACTUALLY KILL YOU


Vitamins
Just shoot us now, why don't you. Vitamins, yes vitamins of all things, can destroy your health: A and E in particular have been linked in numerous studies to increased mortality (from cancer, heart failure, etc.). The reason? Their high levels of antioxidants—which, WTF, have always been hailed as the holy grail of health—weakens your immune system.  
Yoga
Torn tendons and cartila

MAPISHI YA SAMAKI KATIKA OVEN KWA KUTUMIA FOIL

NI RAHISI, NAFUU NA HARAKA SANA KUANDAA AINA HII YA MAPISHI YA SAMAKI KWA KUTUMIA FOIL NA KUOKA KATIKA OVEN LAKINI SAMAKI ATATOKA KAMA AMECHEMSHWA NA AKIWA NA LADHA SAFI SANA BILA YA KUPOTEZA VIRUTUBISHO VYOTE MUHIMU.
MAHITAJI
1pc kitunguu maji kikubwa
1 pc limao kubwa
5 gram binzali
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
1 pc pili pili hoho kubwa
50 gram tomato pest ( nyanya ya kopo)
kipande cha foil kutokana na ukubwa wa samaki
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Huu ni muonekano wa samaki akiwa mbichi tayari umeshamsafisha vizuri kwa maji baridi na mapishi haya unaweza tumia kwa samaki aina ya sato, sangara, kibua, change, jodari au kole kole na akaiva na ladha safi kabisa.


Katika picha unaona mchanganyiko wa vitunguu, pilipili hoho, maji ya limao, binzali, chumvi, pili pili manga na nyanya ya kopo baada ya kuchanganya pamoja kasha mpakae samaki pande zote mbili ulizompasua ili mchanganyiko huu uingie vizuri katika nyama kasha mabaki ya huo mchanganyiko mjazie tumboni kisha mfunike vizuri na foil muweke katika oven tayari ikiwa na moto.

Jana mchana niliporudi nyumbani niliandalia samaki aina ya sato pamoja na maharage ya Nazi na ugali wa mahindi nipo ulaya lakini na kula chakula nilichokizoea nyumbani Tanzania na kwa ladha na ubora ule ule.



Unaweza kumpika katika oven kwa dakika 30 kwenye moto wa degree 200 hadi 250 pia kwa mtindo huu unaweza kumchoma katika jiko la mkaa akiwa hivi hivi katika foil na akaiva safi kabisa



Baada ya nusu saa samaki wako atakua ameiva na atakua na muonekano kama huu na ladha safi sana



Hapa sasa ndio nilikua namfunua vizuri tayari kwa chakula cha mchana


Hata kama samaki amekaa kwenye friza kwa muda mrefu mchanganyiko huu wa mboga majani limao na viuongo vinasaidia sana kuamsha ladha ya samaki wako pika familia ifurahie.


By ISSA KIPANDE

Saturday, 28 September 2013

KINYANG'ANYIRO CHA UREMBO WA DUNIA




HATIMAE MREMBO KUTOKA PHILIPPINES Megan Young ATWAA TAJI LA UREMBO WA DUNIA LEO HII JUMAMOSI 28,09,2013, AKIWAPIGA CHINI MREMBO WA  FRANCE ALIYESHIKA NAFASI YA PILI NA GHANA AMBAE AMESHIKA NAFASI YA TATU

Monday, 23 September 2013

PICHA ZAIDI ZA WATOTO WALIVYOJIACHIA NA DADA DINA CARES WEEKEND HII.

 Snura wa majanga alikuja na mtoto wake,katikati msikilizaji wa clouds fm Ummy Kitwana na Shilole na wanawe.
 Shilole na mtoto wa Snura
 Binti wa Michuzi Jr mzee wa jiachie blog
 Queen Darleen na Mwasiti
 Mwasiti,Shadee na mama wawili
 Regina Mwalekwa na Janet Sosteness wakiwa na watoto
 Shamim Mwasha na Abdul wa sherehe yetu blog nilikochukua baadhi ya picha
 Michuzi jr na Abraham
 Mtoto wa Tunda Man kafanana na baba yake akiwa na mtoto wa Snura katika pozi matata sana
 Tulifungiwa mziki wa nguvu na respect dj
 Respect Dj akiwarusha watoto
 Kila mmoja na style yake heheheeh
 Hapana chezea dada..yupo na mzuka wa hatari
 Washindi walikuwa wakipata zawadi
Kutoka Bongo Movies Dr.Cheni na watoto
 
Picha zitaendelea...

Friday, 20 September 2013

TUZO ZA WANAWAKE WENYE MAFANIKIO TANZANIA 2013 ZAZINDULIWA RASMI!

images 
Achievement (TWAA) leo imezindua Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania msimu wa 2013 zilizopangwa kufanyika katika siku ya wanawake duniani tarehe 8 Mwezi Machi mwaka huu.
Tuzo hizi ambazo hufanyika kila baada ya miaka miwili zilizinduliwa mwaka 2009 kwa heshima ya wanawake katika sekta mbalimbali nchini kote ambao kupitia kazi zao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kuleta maendeleo ya jamii zao kwa njia moja au nyingine.

“TWAA inataka kutambua wanawake, waishio Tanzania ambao kupitia kazi zao wameweza kupata mafanikio makubwa sit u kibinasi bali wametumia nafasi zao kuleta maendeleo na mabadiliko ya kimsingi kwenye jamii zinazowazunguka.” Alisema Mkurugenzi mkuu wa TWA Bi. Irene Kiwia. “Tuzo hizi mbazo sasa ziko katika msimu wake wa 3 zinatoa fursa nzuri ya kutambua na kupongeza wanawake ambao wamechangia sana kwenye kubadilisha na kuboresha sura ya Tanzania. Kwa wanawake wengi hii itakuwa mara ya kwanza mafanikio na michango yao imetunukiwa na hili ni jambo la kufajiri na kuridhisha sana.”
Vipengele vya tuzo za mwaka huu ni Sanaa na Utamaduni, Biashara na Ujasiriamali, Habari na Mawasiliano, Michezo, Professional (Kazi), Elimu, Afya, Ustawi wa Jamii, Sayansi na Teknolojia, Sekta ya Umma, Kilimo na Mshiriko Mdogo.
Bi Sadaka Gandi, mwenyekiti wa kamati ya TWAA alitoa wito kuwa “tunawasihi mashirika, vyama, wanawake na wanaume kote Tanzania kuteua wanawake wenye mafanikio katika makundi haya na kuonyesha mchango wao katika uwezeshaji wa wanawake. Kuna maelfu ya wanawake  wastahili wa tuzo hizi huko nje ambao ni mawakala wa mabadiliko katika jamii zao. Tunataka kuimba mapambio ya mashujaa hawa na kuhamasisha mamilioni ya wanawake wengine wa Tanzania kuiga mifano na kupata msukumo wa kuleta mabadiliko. Kamati ilipokea fomu za nyingi sana za washiriki miaka ya nyuma na hivyo basi tunategemea ushiriki mzuri zaidi mwaka huu. “

Kamati ya TWAA inawajumuisha Bi Mary Rusimbi – Mwanaharakati na Mwanzilishi wa Programu ya Mtandao wa Jinsia Tanzania, Jaji Joaquine De Mello – Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Dk Marcelina Chijoriga- Mkurugenzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bi. Ludovicka Tarimo – Mtaalamu wa Jinsia kutoka USAID, Bwana. Innocent Mungy-Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Sadaka Gandi – Mwanasaikolojia na mfanyakazi za Jamii, Irene Kiwia – Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya mahusiano ya jamii Frontline Porter Novelli.
Huko nyuma tuzo hizi zilidhaminiwa na Baileys, Delloite, NBC, Home Shopping Center, TCRA, Songas, Watu wa Marekani, DTP, UN DPG Gender Group, UNFPA, UNESCO, TBL, Multichoice, African Life Assurance, Barrick, Twiga Cement, Vodacom, Farm Equip, RBP, Clouds FM na Frontline Porter Novelli.