Achievement (TWAA) leo imezindua Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio
Tanzania msimu wa 2013 zilizopangwa kufanyika katika siku ya wanawake
duniani tarehe 8 Mwezi Machi mwaka huu.
Tuzo hizi ambazo hufanyika kila
baada ya miaka miwili zilizinduliwa mwaka 2009 kwa heshima ya wanawake
katika sekta mbalimbali nchini kote ambao kupitia kazi zao wamechangia
kwa kiasi kikubwa sana kuleta maendeleo ya jamii zao kwa njia moja au
nyingine.
“TWAA inataka kutambua wanawake,
waishio Tanzania ambao kupitia kazi zao wameweza kupata mafanikio
makubwa sit u kibinasi bali wametumia nafasi zao kuleta maendeleo na
mabadiliko ya kimsingi kwenye jamii zinazowazunguka.” Alisema Mkurugenzi
mkuu wa TWA Bi. Irene Kiwia. “Tuzo hizi mbazo sasa ziko katika msimu
wake wa 3 zinatoa fursa nzuri ya kutambua na kupongeza wanawake ambao
wamechangia sana kwenye kubadilisha na kuboresha sura ya Tanzania. Kwa
wanawake wengi hii itakuwa mara ya kwanza mafanikio na michango yao
imetunukiwa na hili ni jambo la kufajiri na kuridhisha sana.”
Vipengele vya tuzo za mwaka huu ni
Sanaa na Utamaduni, Biashara na Ujasiriamali, Habari na Mawasiliano,
Michezo, Professional (Kazi), Elimu, Afya, Ustawi wa Jamii, Sayansi na
Teknolojia, Sekta ya Umma, Kilimo na Mshiriko Mdogo.
Bi Sadaka Gandi, mwenyekiti wa
kamati ya TWAA alitoa wito kuwa “tunawasihi mashirika, vyama, wanawake
na wanaume kote Tanzania kuteua wanawake wenye mafanikio katika makundi
haya na kuonyesha mchango wao katika uwezeshaji wa wanawake. Kuna maelfu
ya wanawake wastahili wa tuzo hizi huko nje ambao ni mawakala wa
mabadiliko katika jamii zao. Tunataka kuimba mapambio ya mashujaa hawa
na kuhamasisha mamilioni ya wanawake wengine wa Tanzania kuiga mifano na
kupata msukumo wa kuleta mabadiliko. Kamati ilipokea fomu za nyingi
sana za washiriki miaka ya nyuma na hivyo basi tunategemea ushiriki
mzuri zaidi mwaka huu. “
Kamati ya TWAA inawajumuisha Bi
Mary Rusimbi – Mwanaharakati na Mwanzilishi wa Programu ya Mtandao wa
Jinsia Tanzania, Jaji Joaquine De Mello – Kamishna wa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora, Dk Marcelina Chijoriga- Mkurugenzi kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, Bi. Ludovicka Tarimo – Mtaalamu wa Jinsia
kutoka USAID, Bwana. Innocent Mungy-Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka
Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Sadaka Gandi –
Mwanasaikolojia na mfanyakazi za Jamii, Irene Kiwia – Mwanzilishi na
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya mahusiano ya jamii Frontline Porter
Novelli.
Huko nyuma tuzo hizi zilidhaminiwa
na Baileys, Delloite, NBC, Home Shopping Center, TCRA, Songas, Watu wa
Marekani, DTP, UN DPG Gender Group, UNFPA, UNESCO, TBL, Multichoice,
African Life Assurance, Barrick, Twiga Cement, Vodacom, Farm Equip, RBP,
Clouds FM na Frontline Porter Novelli.
No comments:
Post a Comment