TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Monday 30 September 2013

MWANAMKE HUSIKA NA USAFI WA NYUMBA YAKO



 Wanawake wengi tunapenda kuonekana nadhifu(smart) tutokapo nje ya nyumba zetu, na kuacha mende wakicheza disco ndani mwetu. Kina mama tujipange tusafishe nyumba zetu ili tuwe na hamu ya kuzitumia,usafi wa kila siku unahitajika sehemu zote.
Kwa wanaokosa muda kabisa, angalau usafi kwa wiki mara moja na uwe usafi wa kuridhisha.



                                            ZINGATIA YAFUATAYO                                                               

1. Funika vitu na vyombo vyote vinavyohusiana na chakula, Funga milango na madirisha yote kisha puliza dawa nyumba nzima
Dawa zinatofautiana kutokana na sehemu na maduka yaliyopo karibu ya maeneo tunayoishi, ila nunua dawa ya kuua wadudu Acha muda upite kama masaa 2, kabla hujarudi ndani ya nyumba.Kisha fungua milango na madirisha yote hewa na harufu vitoke nje, ukiridhika kuwa hali imekuwa shwari unaweza kuanza usafi wa sakafu, madirisha, milango na sehemu zingine zilizojificha zinazo hifadhi uchafu.






2. Wakati unapiga deki either kwa tambara au kwa mop, Yale maji ya kupigia deki hakikisha umeyawekea dawa ya kuua wadudu, unaweza kutumia Dettol au dawa nyingine yoyote ya maji inayopatikana au uliowahi kuitumia ukaona inafaa
Hakikisha maji yamefika sehemu zote muhimu.



3. Usisahau kufuta sehemu zozote ambazo chakula kimemwagika, mezani na kwingineko
Hakikisha matakataka yote unayatupa sehemu sitahili.

ZINGATIA: Usipende kuacha chakula wazi, au kuacha mabaki ya chakula au uchafu wowote uliodondoka bila kuusafisha kila unapomaliza kula
Na taka taka zote zitupwe mbali na nyumba kila siku kabla ya kulala, kwani mende hujitokeza nyakati za usiku.




4.Baada ya kuwa umeridhika na usafi wa nyumba unaweza kuweka manukato ya kufanya nyumba inukie vizuri , Airfreshner zipo za aina nyingi na bei tofauti
Chagua inayokupendezea kwa harufu, tundika au pulizia.



     
Ukifanya hivyo mara kwa mara itapunguza kwa kiasi kikubwa, mende kuitembelea himaya yako.
Jitahidi usiache chakula wala vinywaji vinazagaa bila kufunikwa na vyombo vyote vioshwe kabla ya kulala.

Mungu awabariki.

No comments:

Post a Comment