Mtoto Brilliant David (2yrs) akipaka rangi kwa furaha siku hiyo ndani ya Nkema Reading Club.
Mkurugenzi Mtendaji wa Nkema Reading Club Bi Getrude Kilyabusebu akiwasomea watoto hadithi iitwayo 'MTO WA AJABU'
Mmoja kati ya waalimu wa Nkema Reading Club akimuelekeza mtoto Briliant namana ya kupaka rangi.
Baadhi ya wanachama wakichora ndani ya Nkema Reading Club.
wako bize sana wanachora nini njoo tembelea Nkema Reading Club.
Mwanachama Kemmy Linus Kinyondo (kulia) akiwasomea na kuchambua hadithi ya 'GODORO LA AJABU' wanachama wenzie (kushoto) wakimsikiliza kwa makini
Mmoja kati ya waalimu wa Nkema Reading Club Glorito (kati) akiwafundisha wanachama wa Club hiyo Careen Elly (kushoto) na Kemmy Kinyondo (kulia) wakimsikiliza kwa makini.
Hili ni darasa la Computer lililoandaliwa kwa ajiri ya kufundishia program za computer kwa watoto watakao andikishwa kuanzia mwezi wa tatu mwaka huu
Hivi ni baadhi ya vitabu ambavyo vimesomwa na watoto ndani ya Nkema Reading Club.
Na Getrude Edward
Nkema Reading Club ni kituo cha kusomea watoto kuanzia umri wa
miaka miwili hadi miaka kumi na nne,ambapo mtoto atajifunza mambo mengi ikiwemo
kupenda kusoma vitabu ili kuongeza maarifa,vitabu vitasomwa kwa lugha mbili
ikiwemo English na Kiswahili, hapo mtoto atasomewa na kusoma kisha wote kwa
pamoja watachambua kitabu ili kupata uelewa na kufahamu maudhui ya hadith
waliyo soma. Kwa watoto wenye uwezo wa kutunga hadithi zitapokelewa na kusomwa ndani ya Club hiyo, pia zitahaririwa.
Nkema Reading Club ina lengo kuu la kutengeneza kizazi cha wasomi
wenye kupenda kusoma kwani inaamini maarifa mengi hupatikana katika usomaji
vitabu, pia ina lengo la kujenga ujasiri kwa watoto wa kitanzania, ambapo Nkema
Reading Club ilifanya utafiti na kugundua kuwa ujasiri kwa Mtanzania ni tatizo,
Nkema Reading Club inatoa mafunzo ya Computer (program za watoto) kwa watoto
watakaoandikishwa kwa ajiri ya program hizo.
Nkema Reading Club ni
suruhisho la Jamii ya Tanzania.
Mwandikishe mwanao kwa gharama ya Tsh.50,000 kwa mwezi, kila jmosi
kuanzia saa nne hadi saa saba mchana. Usafiri upo mtoto atafuatwa na
kurudishwa, pia course za Computer ni Tsh.50,000 kwa kila program,ambapo
program moja inamalizika kwa week moja. Tunao waalimu wazuri waliobobea juu ya
ufundishaji na ukufunzi.
Nkema Reading Club ipo maeneo ya Kinondoni karibu na kituo cha daladala cha Vijana.
KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA NAMBA. 0754032589/0655032589
NAFASI ZIPO