Waziri
wa Afya Mh. Seif Rashid akiongea na Wauguzi wa Hospitali teule ya Mkoa
wa Temeke, Wafanyakazi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm pamoja na wadau
mbalimbali wakati wa uzinduzi Rasmi wa Radio hiyo, ambayo lengo lake ni
kuwakomboa vijana wa Mtaani pamoja na vipindi vingine vya kuelimisha
Jamii na Burudani, Pia amewashukuru kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali
ambavyo vitasaidia katika Hospitali hiyo leo Tarehe 1.11.2014
Mkurugenzi
wa Sibuka George Ndagali akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Ghetto Radio ya Sibuka Fm iliyo fanyika katika katika Hosipitali Teule
ya Mkoa wa Temeke Ambapo Ghetto Radio Imeweza kufunguliwa Rasmi Katika
Mkoa huo nakuweza kutoa Msaada Vifaa Mbalimbali pamoja na Madawa Ambavyo
Vyote kwa ujumla vimegharimu kiasi Cha Shilingi Milioni sita na Laki
sita.
Mkurugenzi
wa Ghetto Radio Matt Brouwer akizungumza neno wakati wa uzinduzi wa
Ghetto Radio ya Sibuka Fm Ambapo Bw.Brouwer Alisema kuwa Ghetto Radio
ilianzishwa nchini Kenya Miaka Sita iliyopita nakuweza kuwasaidia vijana
mbalimbali Hivyo wameweza kuingia Nchini Tanzania Ilikuendeleza kuwapa
vijana Fursa Na elimu INayo Tolewa na Kituo Hicho Kwa Hapa Nchini
Mganga
Mkuu wa Hospitali teule ya Mkoa wa Temeke Amaani K. Malima akitoa neno
la Shukurani kwa Timu nzima ya Ghetto Radio ya Sibuka Fm kwa kufanya
uzinduzi wa Radio yao katika Hospitali hiyo pia kutoa Msaada wa vitu
mbalimbali vitakavyo saidia katika eneo hilo.
Meneja
wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm Edward Lukaka akitoa maelezo machache
ya malengo ya Radio hiyo pia kueleza mikakati ya kuendelea kutoa msaada
wa vifaa mbalimbali vya tiba katika Vituo zaidi vya Afya.
Mkurugenzi
wa kituo cha afya cha Iran Nchini Tanzania Dkt. Farhad Arjomandi
akiwashukuru Ghetto Radio ya Sibuka FM kwa kuanzisha Kituo hicho pia na
wao wametoa vifaa vya matibabu kwa ajili ya kushiriki uzinduzi huo wa
Radio
Mwenyekiti wa Red Cross Mkoa wa Dar es salaam Leonard Masonu akitoa neno la Shukurani
Hivi
ni Baadhi ya vitu ambavyo vimetolewa na Ghetto Radio ya Sibuka Fm
katika Hospitali teule ya Mkoa wa Temeke wakati wa uzinduzi Rasmi wa
Radio hiyo
Waziri
wa Afya Mh. Seif Rashid akikabidhiwa Rasmi msaada wa Vifaa na Vitu
mbalimbali vitakavyo tumika katika Hospitali teule ya Mkoa wa Temeke
kutoka kwa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
Waziri wa Afya Mh. Seif Rashid kushoto Akishukuru kwa vifaa hivyo.
Baadhi ya Wadau mbalimbali walioshiriki katika Sherehe hiyo ya Uzinduzi Rasmi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
Baadhi ya Wauguzi wakiwa katika uzinduzi huo Rasmi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
Wafanyakazi
wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm pamoja na wadau mbalimbali wakijiandaa
kuelekea kutoa Msaada wa vitu mbalimbali katika vyumba vya wagonjwa
Wakiwa wanaelekea Wodini
Kulia
ni Mkurugenzi wa Sibuka George Ndagali akiwa katika Wodi ya watoto
kukabidhi zawadi za watoto na mama zao, katikati ni Mwanamuziki Mkongwe
wa Bongo Flava Juma Nature ambaye ni Balozi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
Balozi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm Juma
Nature akiwa anatandika Shuka moja wapo katika Wodi ya watoto kuashiria
kukabidhi mashuka hayo.
Baadhi ya Timu ya wafanyakazi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
No comments:
Post a Comment