TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Tuesday, 28 October 2014

Mambo yazidi kuiva Karibu Music Festival

Px 1
WASANII kutoka ndani na nje wanatarajiwa kupamba tamasha la Muziki la Kimataifa la ‘Karibu Music Festival’ litakalofanyika kwa siku tatu kwenye mji wa Kihistoria wa Bagamoyo, Novemba 7 hadi 9 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mapema Oktoba 27, Msemaji wa tamasha hilo Muslim Nassor ‘Jazzphaa’ alisema maandalizi yamekamilika na tayari wasanii wa awali waliopatikana wapo hadharani wanaendelea na matayarisho huku akiwaomba watanzania na wadau wa burudani kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo.
Jazzphaa aliwataka baadhi ya wasanii wa nje na ndani na nchi zao katika mabano ni Panda (Japan), Maria Kate (Ufaransa), IFE Pianki (Uganda), Masayo (Japan), Fantuzz (Marekani), Shiwe Musique (Comoro), Dwembede (Kenya) na Mbiye Ebrima (Guinea).
Kwa upande wa
viingilio, alisema kitakuwa ni sh 5,000 kwa kila Mtanzania huku kwa
atakayekata tiketi ya siku tatu, kwa pamoja, ni sh. 12,000.
“Tamasha
hili litakuwa likifanyika usiku na mchana. Wasanii wote watakaokuwepo
katika tamasha hili watalazimika kupiga muziki kwa kutumia ala za asili
za muziki ‘Live’ na siyo ‘Playback’” alisisitiza Jazzphaa.
Kwa
upande wake, Meneja wa tamasha hilo, Richard Lupia alisema tamasha
hilo mbali ya burudani, wasanii pia watapata nafasi ya kujifunza jinsi
ya kuunadi muziki wao duniani kwa njia mbali mbali ambako kutakuwa na
warsha kutoka kwa wataalamu toka pembe zote za dunia.
Pia alisema katika tamasha hilo kutakuwa na sanaa za Michoro, mavazi na kuchonga zitakuwa zikioneshwa eneo la tamasha.
“Semina
na mijadala ya jinsi ya kuupeleka muziki wa Tanzania katika hatua
nyingine za kimaendeleo zitatolewa kwa wasanii mbalimbali. Mbinu za
kuuza kazi zao kwenye masoko ya kimataifa na kutafuta soko duniano kote
hii itakuwa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa hapa hapa nchini”
alisema Lupia.
 Makundi na
majina ya wasanii kutoka nyumbani ni pamoja na Afrikabisa Band,
Wahapahapa, Segere Original, Jahazi, The Spirit Band na Mama Africa.
Wengine
ni Cocodo Band, Hokororo Band, Swanu Gogo Vibes, Swahili Vibes, Fimbo
Band, Abeneko Music, Man Kifimbo, Saganda na Msafiri Zawose.
Wasanii
wengine ni Msafiri Zawose ‘Chibite Zawose’, Tongwa Ensemble, Leo
Manyika, Swahili Blues, Profesa Jay, Shilole, Juma Nature, Barnaba,
Vitalis Maembe na Jhikoman.
Aidha,
Jazzphaa aliongeza kuwa lengo la tamasha hilo ni kukuza na kurasimisha
tasnia ya muziki kwa umakini zaidi na kukuza uchumi wa eneo la
Bagamoyo ambalo ni la kihistoria.
PICHANI JUU:
Msemaji wa
tamasha la Karibu Music Festival, MAuslim Nassor ‘Jazzphaa’ (katikati)
akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho
huo.

No comments:

Post a Comment