TAKUKURU inamshikilia Mkurugenzi na mmiliki wa kituo cha Makoye Education Centre kilichopo maeneo ya Nyasho Manispaa ya Musoma Mwalimu Joseph Makoye kwa tuhuma za kudai rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi aliyekuwa akifanya maandalizi ya mtihihani wa Taifa wa Kidato cha Nne 2013 unaoanza leo, katika kituo hicho.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkuu wa TAKUKURU mkoani Mara, Holle Makungu ilidai mwanafunzi huyo wa

kike (jina limehifadhiwa) alijiandikisha kufanya mtihani huo kupitia sanduku la posta 216 la kituo hicho ambapo barua yake ya mtihani kutoka Baraza la Mtihani ilipitia katika kituo hicho, lakini Mkurugenzi wa kituo hicho aliitumia kama chambo cha kutaka rushwa ya ngono ndipo aitoe barua hiyo.
TAKUKURU wakiwa katika mtego wao, alifika mtuhumiwa katika eneo husika na kumuita mwanafunzi na kumpandisha kwenye gari namba T 697 BNQ na kwenda naye katika nyumba ya kulala wageni ya Tedasi iliyopo eneo la Bweri nje kidogo ya mjini wa Musoma huku wakiwa na tahadhari ili mwanafunzi huyo asiweze kufanyiwa mabaya.
Hatimaye TAKUKURU walifanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo katika nyumba hiyo ya wageni kisha kwenda naye nyumbani kwake eneo la Mkendo Kati na kufanya upekuzi na kufanikiwa kuipata fomu hiyo kutoka Baraza la Mtihani la Taifa.

No comments:
Post a Comment