TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Monday, 17 November 2014

MISA YA SHUKRANI YA KUTIMIZA MIAKA SABA YA MAMA AURELIA KOBULUNGO MUGANDA TANGU ALIPOITWA NA MWENYEZI MUNGU ILIYOFANYIKA NYUMBANI KWA MTOTO WAKE FR.JAMES RUGEMALIRA MAKONGO JUU JIJINI DAR ES SALAAM


Mama Aurelia Kobulungo Muganda enzi za uhai wake
 Kaburi la Mama Aurelia linavyoonekana
 Altare iliyoandaliwa kwa ajili ya misa takatifu ya shukrani kwa ajili ya Mama Aurelia
Fr Mukandara akibariki maji yaliyochanganywa na chumvi ambayo yalitumika kubariki kaburi. (Imeandaliwa na www.habari za jamii.com)
Padri Mukandara akibariki kaburi
Ni wakati wa kuanza ibada takatifu ya misa ya shukrani. Wanafamilia wakielekea kwenye ukumbi maalumu. 
Bwana na Bibi Fr. James Rugemalira wakiwaongoza mapadre kuelekea kwenye misa takatifu
Paroko wa Kanisa Katoliki Makongo Juu Joseph Masenge akisisitiza jambo wakati wa misa hiyo
Jopo la mapadre walioshiriki katika misa hiyo takatifu
Wanakwaya kutoka kanisa la Makongo Juu wakitumbuiza katika misa hiyo
Wanafamilia kutoka kushoto Everine Rugemalira, Joe Mgaya na Jerome Rugemalira wakifuatilia kwa karibu ibaada ya misa hiyo
Wageni mbalimbali wakitafakari matendo makuu ya Mungu kwenye ibadaa hiyo
Waalikwa mbalimbali wakiwa kwenye ibaada hiyo





Wanafamilia wakiwa kwenye ibaada hiyo

Mmm ni upendo ulioje unapoona kusanyiko kubwa kama hili


Mdau Joyce (katikati) hakupenda kukosa ibaada hiyo takatifu 
Paroko Masenge akipokea vipaji mbalimbali kutoka kwa watukuu wa Bibi Aurelia.

MAUAJI YAZIDI KUTIKISA KITETO....WALIOPOTEZA UHAI WAFIKA 7

Mapigano baina ya wakulima na wafugaji Wilayani Kiteto mkoani Manyara, yameendelea tena, ambapo watu wengine wawili wamefariki dunia jana na kufanya idadi ya waliouawa kuwa saba.
Awali, Novemba 11, mkulima Hassan Kondeja mkazi wa Kitongoji cha Bwawani Kijiji cha Matui aliuawa kwa kukatwa shingo na wafugaji na ndipo yakatokea mauaji ya wakulima wawili na wafugaji wawili.
Akizungumza na mwandishi wetu, Kamanda wa polisi wa Mkoa Manyara, SACP Deusdedit Nsimeki alisema wakulima wawili wameuawa jana kwa kukatwa na mapanga na watu wanaodaiwa kuwa ni wafugaji wa jamii ya Kimasai.
Kamanda Nsimeki aliwataja wakulima hao waliouawa ni Juma Omary (65) na Nyanya Ngoroka (70) wote wakazi wa Kijiji cha Cheka Nao, kata ya Kiperesa iliyopo mpakani na wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
“Chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi uliotokea kati ya wafugaji kuingiza mifugo yao kwenye shamba la wakulima hao na walipowakataza wakatumia silaha za moto na kuwakata mapanga wakafa papo hapo,” alisema Kamanda Nsimeki.
Alisema vifo hivyo vinatokana na kulipiza kisasi kati ya wafugaji na wakulima ambao chanzo chake ni migogoro ya ardhi ya muda mrefu.
Naye, mkuu wa mkoa huo, Elaston Mbwilo alisema wapo baadhi ya viongozi wamekuwa wazembe hawawajibiki katika nafasi zao na kuwa sehemu ya baadhi ya migogoro inayoendelea Kiteto.

Aliyasema hayo mjini Kibaya akizungumza na wazee maarufu wa jamii ya wafugaji na wakulima, ili kujua kiini cha mauaji yaliyotokea Matui ambapo watu watano waliuawa kwa kukatwa mapanga.


Mbwilo alisema wapo baadhi ya viongozi kuanzia ngazi ya Kata,Vijiji na Mitaa wamebeba uongozi bila kujua dhamana zao.

EDWARD LOWASSA MMH...MASTAA KUMFANYIA BONGE LA PATI!

Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Wolper. Chanzo makini kilichopo ndani ya kamati ya wasanii hao wa Bongo Movies, kitendo cha Taasisi ya Twaweza kutangaza kuwa Lowassa anaongoza na kuwagaragaza makada wenzake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kwao ni ishara tosha ya ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao. 

SIKU chache baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kutangazwa kuwa anaongoza katika kinyang’anyiro cha urais 2015, mastaa mbalimbali wanaomuunga mkono wameandaa mkakati wa kumfanyia sherehe ya kumpongeza. 

“Mastaa wa Bongo Movies wanaomuunga mkono Lowassa wameandaa bonge la pati la kumpongeza Lowassa na siku hiyo watakula, watakunywa maana mipango yao tayari wanaona inakwenda vizuri na hakuna mtu ambaye anaweza kumuangusha katika chama hicho,” kilisema chanzo bila kutaja lini na wapi watakapofanyia sherehe hiyo

Sunday, 16 November 2014

SEKTA BINAFSI IHUSISHWE KUTOA HUDUMA ZA AFYA – PINDA

unnamed
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Afya (Annual Health Summit ) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 14, 2014. (Picha na Ofisi ya Wazri Mkuu) unnamed2 Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Afya (Annual Health Summit ) wakimsikiliza Waziri Mkuu,Mizengo Pinda wakati alipofungua mkutano wao kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Novemba14, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameitaka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ipanue wigo wa utoaji huduma za msingi kwa kuishirikisha zaidi sekta binafsi nchini.
 “Ninawasihi Waziri wa Afya na Naibu wake kwa vile ni wapya bado wabadili mtizamo wa wizara hii kwa kushirikisha zaidi wadau wa sekta binafsi kwenye utoaji wa huduma ili wasaidie kupunguza mzigo mkubwa ilionao Serikali,” alisema.
 Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Novemba 14, 2014) wakati akifungua Mkutano wa wa Kwanza wa Kitaifa wa Sekta ya Afya wa mwaka 2014 ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu ambaye amefungua mkutano huo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete aliyeko nje ya nchi kwa matibabu alisema: “Kuna tatizo la kukumbatia utoaji wa huduma … tunazo hospitali kubwa za wilaya zinazomilikiwa na taasisi za dini. Hivi ni kwa nini kama Wizara msiwasaidie kuwahudumia watumishi wao au kuwapa ruzuku kwenye dawa ili kuwawezesha kutoa huduma kwa ufanisi zaidi?,” alihoji Waziri Mkuu na kushangiliwa na washiriki wa mkutano huo.
 “Hata ukiangalia takwimu kwenye utoaji wa huduma za afya kupitia mifumo ya bima ya afya utabaini kuwa ni asilimia 18 tu wananchi wanatumia bima ya afya na kati ya hao, asilimia 15.3 ni mifuko ambayo imeanzishwa na Serikali. Ni kwa nini basi msiwasaidie wadau wa sekta binafsi ili wachangie huduma hii na idadi wa watumiaji wa mfumo huu iongezeke haraka?,” alihoji.
 Akizumgumzia kuhusu uwiano kati ya daktari na mgonjwa, Waziri Mkuu alisema uwiano uliopo ni mbaya na kwamba hakuna njia ya haraka ya kupunguza tatizo hilo isipokuwa kwa kuishirikisha sekta binafsi kwenye ujenzi wa vyuo vikuu vya elimu ya tiba na sayansi za jamii.
 “Uwiano wa sasa hapa nchini ni daktari mmoja kwa wagonjwa 75,000 wakati viwango vya kimataifa vinataka daktari mmoja awahudumie wagonjwa 7,000. Kwa wauguzi, hapa nchini muuguzi mmoja anahudumia wagonjwa 6,000 wakati viwango vya kimataifa vinataka muuguzi mmoja ahudumie wagonjwa 500,” alisema.
 “Kwa uwioano huu safari bado ni ndefu. Tunapaswa tuangalie tutafanyaje ili watu binafsi waje kuwekeza kwenye elimu ya juu ya sayansi na tiba, wajenge vyuo vya tiba, wajenge hospitali kubwa, na sisi pia kwa upande wa Serikali ni lazima tuseme tunawapa vivutio gani hawa wawekezaji hadi wakubali kuwekeza kwenye eneo hilo,” alisema.
 “Tunataka mkutano huo uje na mapendekezo ambayo mnataka Serikali iyafanyie kazi na hatimaye isaidie kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi,” alisema Waziri Mkuu.
 Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano huo, Waziri Mkuu alisema Serikali inaendelea kudhibiti ugonjwa wa ebola kwenye vituo vya mipakani na kwenye viwanja wa ndege.
 “Mpaka sasa hatujapata kesi ya ugonjwa wa ebola hapa nchini… changamoto kubwa ni ukubwa wa mipaka yetu. Si wageni wote wanaoingia nchini wanapita kwenye vituo rasmi, wapo wanaotumia njia za vichochoroni. Rai yangu ni kuwaomba Watanzania wawe waangalifu kutambua ni wageni gani wanaingia kwenye maeneo wanayoishi,” alisema.
Mkutano huo wa siku mbili unamalizika kesho (Jumamosi, Novemba 15, 2014).
Waziri Mkuu amerejea mjini Dodoma kuendelea na kikao cha Bunge.

Friday, 14 November 2014

WANAODAIWA KUWA NI WAVUVI HARAMU WAPOTEZA MIKONO, MACHO BAADA YA KULIPUKIWA NA MABOMU YAO WAKATI WAKIVUA

Baadhi ya majeruhi waliolipukiwa na baruti jana wakati wakivua samaki kwa kutumia baruti katika Kisiwa cha Karange tarafa ya Pongwe wakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo huku wakiwa wamepoteza baadhi ya viungo vikiwemo macho na mikono. (Picha na Elizabeth Kilindi)
 Baadhi ya majeruhi waliolipukiwa na baruti jana wakati wakivua samaki kwa kutumia baruti katika Kisiwa cha Karange tarafa ya Pongwe wakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo huku wakiwa wamepoteza baadhi ya viungo vikiwemo macho na mikono. 
 Baadhi ya majeruhi waliolipukiwa na barutiwakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo huku wakiwa wamepoteza baadhi ya viungo vikiwemo macho na mikono.
  Mmoja wa majeruhi waliolipukiwa na baruti wakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo huku wakiwa wamepoteza baadhi ya viungo vikiwemo macho na mikono. 

Elizabeth Kilindi, Tanga

Wakazi wawili wa kata ya Tangasisi tarafa ya Pongwe wilayani Tanga wamejeruhiwa vibaya viungo mbalimbali vya mwili  kwa kulipukiwa na baruti wakati wakivua kwa kutumia dhana za uvuvi haramu kwenye kisiwa cha Karange.

Tukio hilo limetokea mnamo Novemba 12 mwaka huu majira ya saa nane mchana katika kisiwa  ambapo majeruhi hao wakiwa kwenye ngalawa yenye namab za usajili TTA 315 wakati wakijianda kutegesha baruti hizo ndipo zilipowalipukia.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Freisse Kashai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja majeruhi hao kuwa ni Hamis Omari ambaye amekatika mkono wa kulia na ameumia jicho la kulia, huku majeruhi mwingine Adamu Selemani amekatika mikoni yote miwili, pamoja na kupoteza macho yote mawili.

“Hali ya majeruhi wote wawili ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo ni mbaya hii inaonyesha ni kwa kiasi gani uvuvi haramu ulivyo na madhara makubwa kwa jamii pamoja na viumbe wa baharini “alisema Kamanda Kashai.

Kamanda Kashai alitumia fursa hiyo kuwa taka wakazi
wanaoishi maeneo ya bahari kutoa taarifa ya watu wanaojihusisha na uvuvi haramu ili kuweza kuwachukulia hatua mapema kabla ya kutokea kwa madhara zaidi.

WADAU WA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA WAKUTANA KUJADILI MAENDELEO YA SEKTA HIYO NCHINI.

1
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA)Charles M.  Chacha (Kushoto), akiteta jambo na mmiliki wa kampuni ya Tran World ya nchini Dubai  Mr. Adil Jadid kulia) wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya usafiri wa anga Tanzania. Mkutano huo unatoa   fursa za kujadili maendeleo ya sekta hiyo nchini .  Mkutano ulifanyika makao makuu ya Mamlaka ya usafiri wa Anga jijini Dar es Salaam.  Katikati ni Mjumbe wa Bodi wa TCAA Yussuf Mohammed Aly. 2
Baadhi ya wadau wa sekta ya usafiri wa anga Tanzania wakifuatilia mada wakati  wa mkutano wa wadau wa sekta hiyo uliotoa   fursa za kujadili maendeleo ya sekta hiyo nchini ulifanyika makao makuu ya Mamlaka ya usafiri wa Anga jijini Dar es Salaam leo.34
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti masuala ya Ki- Uchumi, Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA), Dkt. James Diu  (wapilia kutoka kulia) akitoa mada wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya usafiri wa anga Tanzania. Mkutano huo unatoa   fursa za kujadili maendeleo ya sekta hiyo nchini, ulifanyika makao makuu ya Mamlaka ya usafiri wa Anga jijini Dar es Salaam .Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Udhibiti masuala ya ki-usalama TCAA, Bw. Jude Mkai. 5
Baadhi ya wadau wa sekta ya usafiri wa anga Tanzania wakifuatilia mada wakati  wa mkutano wa wadau wa sekta hiyo uliotoa   fursa za kujadili maendeleo ya sekta hiyo nchini ulifanyika makao makuu ya Mamlaka ya usafiri wa Anga jijini Dar es Salaam leo.6
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka yaUsafiri wa Anga(TCAA), Bw. Charles M. Chacha(aliyeshika maiki), akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya usafiri wa anga Tanzania. Mkutano huo unatoa   fursa za kujadili maendeleo ya sekta hiyo nchini Ulifanyika makao makuu ya Mamlaka ya usafiri wa Anga jijini Dar es Salaam

TANZANIA KUJENGA KITUO KIKUBWA CHA SEKTA YA NYUKI DODOMA

index
Mahmoud Ahmad Arusha
Tanzania  inatarajia kujenga kituo Kikubwa   cha sekta ya nyuki ambacho kitatoa mafunzo  juu  ya namna bora ya kufuga nyuki kisasa
 
Mtendaji Mkuu wa baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi Dakta  Anaclet Kashuliza  ameeleza hayo  wakati wa kongamano la kwanza  la ufugaji nyuki barani Afrika.
 
Kituo hicho kinatarajiwa kujengwa MKoani Dodoma kwa msaada wa Kampuni moja kutoka Marekeni mbali na kituo hicho kuhusika na utoaji  mafunzo pia kitahusika na  uchakataji  wa asali
 
Dakta Kashuliza amesema kuwa kituo hicho  kitahusika na utunzani wa  kumbukumbu  ya vitu vya  asali  vya ufugaji nyuki hapa Tanzania na kinatarajia kuanza katika kipindi cha miezi minne ijaayo
 
Dakta Kashuliza  aidha amesema mbali na kujengwa kwa kituo hicho kikubwa barani afrika pia  Tanzania inatarajia kujenga viwanda vidogo vidogo, vya kati na viwanda vikubwa kwa ajili ya kusindika asali na nta
 
Viwanda hivyo  vitatumika kwa ajili ya watalii kutoka nje  watakaopata fursa ya kutembelea viwanda hivyo pamoja na kituo kikubwa  cha  Dodoma kujionea  juu ya hali ya raslimali asali ilivyo.
 
Wakati huo huo Serikali Mkoa wa  Singida imesema kuwa ipo tayari  kuyaondoa  makundi yote  ya watu waliovamia maeneo ya wahadzabe wakiwemo wakulima na wafugaji na hivyo kuwawezesha kumiliki maeneo hayo kama zilivyo jamii nyingine nchini.
 
Kauli hiyo imetolewa leo na mkuu wa mkoa wa Singida,Vicent  Parseko  Kone
 
Hatua hii inalenga kuwapa haki yao  ya msingi ya kumiliki ardhi jamii hiyo ya wahadzabe kama  jamii nyingine ya watanzania hapa nchini
 
Amewaambia washiriki wa kongamano la ufugaji nyuki barani afrika kuwa   asilimia 77 ya eneo linalokaliwa na jamii ya wahadzabe tayari limevamiwa na wafugaji pamoja na wakulima  jambo ambalo linatishia maisha ya jamii hiyo ya wahadzabe ambao  maisha yao yote hutegemea sekta ya nyuki 
 
Amesema katika mkakati huo wa kuwaondoa wavamizi wote pia  Serikali imefanikiwa kupeleka huduma mbambali za kijamii zikiwemo za maji, miundo mbinu ya barabara, elimu na afya.
 
Mkuu huyo wa Mkoa pia amesema Serikali Mkoani humo imefanikiwa kuyapima maeneo yote wanamoishi wahadzabe ili kuwawezesha kupata hati miliki
 
Pia amesema Serikali imesambaza mizinga  zaidi ya 150 katika jamii hiyo ili kuiwezesha kuendeleza zaidi ufugaji wa nyuki katika jamii hiyo pamoja na kuipatia  mtama kwa ajili ya kuwawesha kuendelezaa kilimo katika vijiji vyao
 
Mkoa huo hivi sasa una  watu wapatao 1,300 wa jamii ya  wahadzabe ambapo  300 wanaishi katika wilaya ya Mkalama katika Kijiji cha Munguli
 
Wakizungumza katika kongamano hilo mmoja wa jamii hiyo ya wahadzabe amesema jamii hiyo inayo haki ya kumiliki  ardhi kama jamii nyingine ya kitanzania
 
Aidha ameitaka serikali kukomesha vitendo  vya  baadhi ya jamii kuvamia maeneo yao kwa  kutumia nguvu  za kiuchumi walizonazo
 
Hivyo ameitaka   serikali kuhakikisha  jamii   ya wafugaji na wakulima kufuata taratibu pale wanapoingia katika  baadhi ya maeneo
 
Amekiri kuwa  kwa asilimia kubwa jamii ya wahadzabe walikuwa  hawajui haki haki zao pamoja na matumizi ya ardhi

Serikali Mkoa wa  Singida imesema kuwa ipo tayari  kuyaondoa  makundi yote  ya watu waliovamia maeneo ya wahadzabe wakiwemo wakulima na wafugaji na hivyo kuwawezesha kumiliki maeneo hayo kama zilivyo jamii nyingine nchini.
 
Kauli hiyo imetolewa leo na mkuu wa mkoa wa Singida,Vicent  Parseko  Kone
 
Hatua hii inalenga kuwapa haki yao  ya msingi ya kumiliki ardhi jamii hiyo ya wahadzabe kama  jamii nyingine ya watanzania hapa nchini
 
Amewaambia washiriki wa kongamano la ufugaji nyuki barani afrika kuwa   asilimia 77 ya eneo linalokaliwa na jamii ya wahadzabe tayari limevamiwa na wafugaji pamoja na wakulima  jambo ambalo linatishia maisha ya jamii hiyo ya wahadzabe ambao  maisha yao yote hutegemea sekta ya nyuki 
 
Amesema katika mkakati huo wa kuwaondoa wavamizi wote pia  Serikali imefanikiwa kupeleka huduma mbambali za kijamii zikiwemo za maji, miundo mbinu ya barabara, elimu na afya.
 
Mkuu huyo wa Mkoa pia amesema Serikali Mkoani humo imefanikiwa kuyapima maeneo yote wanamoishi wahadzabe ili kuwawezesha kupata hati miliki
 
Pia amesema Serikali imesambaza mizinga  zaidi ya 150 katika jamii hiyo ili kuiwezesha kuendeleza zaidi ufugaji wa nyuki katika jamii hiyo pamoja na kuipatia  mtama kwa ajili ya kuwawesha kuendelezaa kilimo katika vijiji vyao
 
Mkoa huo hivi sasa una  watu wapatao 1,300 wa jamii ya  wahadzabe ambapo  300 wanaishi katika wilaya ya Mkalama katika Kijiji cha Munguli
 
Wakizungumza katika kongamano hilo mmoja wa jamii hiyo ya wahadzabe amesema jamii hiyo inayo haki ya kumiliki  ardhi kama jamii nyingine ya kitanzania
 
Aidha ameitaka serikali kukomesha vitendo  vya  baadhi ya jamii kuvamia maeneo yao kwa  kutumia nguvu  za kiuchumi walizonazo
 
Hivyo ameitaka   serikali kuhakikisha  jamii   ya wafugaji na wakulima kufuata taratibu pale wanapoingia katika  baadhi ya maeneo
 
Amekiri kuwa  kwa asilimia kubwa jamii ya wahadzabe walikuwa  hawajui haki haki zao pamoja na matumizi ya ardhi
Hatua hii itachangia kuvutia zaidi masoko ya nje kutokana na watalii hao kutembelea viwanda hivyo
 
Aidha Dakta Kashuliza amesisitiza kuwa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi limejipanga  kuimarisha elimu kwa wazalishaji na  wafugaji wa nyuki ili waweze kuzingatia  uzalishaji wa  asali katika viwango vyenye ubora kimataifa
 
Elimu hiyo itatolewa na baraza hilo kwa ushirikino  na TBS ili kuwezesha asali ya Tanzania kupata masoko ya uhakika nje ya nchi.amesisitiza Katibu Mtendaji huyo  wa baraza hilo
 
Mbali na hatua hiyo Dakta Kashuliza amesema Baraza  limeanzisha Programu ya majaribio katika miko 10 ya Tanzania bara kuhisiana na ufugaji nyuki ili  wafugaji hao waweze kufuga kiisasa zaidi na kibiashara katika viwango vyenye ubora kimataifa
 
Dakta Kashuliza ameitaja mikoa inayotekeleza Programu hiyo ya majaribio kuwa ni Mkoa wa Pwani,Dodoma,Morogoro,Tanga,Manyara, Iringa, Singida, Tabora Katavi na Kigoma
 
Amesema baraza  hivi sasa linasimamia  kwa nguvu zote suala la wafugaji kutumia teknolojia  bora zaidi katika ufugaji wa nyuki kwa kutumia mizinga bora
 
Mbali na hatua hii Baraza pia limeingia mikataba na  wadau mbalimbali wa nje ya nchi ili kuwaunganisha wazalishaji wa asali nan je kuweza kupata masoko ya uhakika ya mazao ya nyuki kutoka Tanzania.Amesisitiza Dakta Kashuliza