Mahmoud Ahmad Arusha
Tanzania inatarajia kujenga kituo Kikubwa cha sekta ya nyuki ambacho kitatoa mafunzo juu ya namna bora ya kufuga nyuki kisasa
Mtendaji Mkuu wa baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi Dakta Anaclet Kashuliza ameeleza hayo wakati wa kongamano la kwanza la ufugaji nyuki barani Afrika.
Kituo hicho kinatarajiwa kujengwa MKoani Dodoma kwa msaada wa Kampuni moja kutoka Marekeni mbali na kituo hicho kuhusika na utoaji mafunzo pia kitahusika na uchakataji wa asali
Dakta Kashuliza amesema kuwa kituo hicho kitahusika na utunzani wa kumbukumbu ya vitu vya asali vya ufugaji nyuki hapa Tanzania na kinatarajia kuanza katika kipindi cha miezi minne ijaayo
Dakta Kashuliza aidha amesema mbali na kujengwa kwa kituo hicho kikubwa barani afrika pia Tanzania inatarajia kujenga viwanda vidogo vidogo, vya kati na viwanda vikubwa kwa ajili ya kusindika asali na nta
Viwanda hivyo vitatumika kwa ajili ya watalii kutoka nje watakaopata fursa ya kutembelea viwanda hivyo pamoja na kituo kikubwa cha Dodoma kujionea juu ya hali ya raslimali asali ilivyo.
Wakati huo huo Serikali Mkoa wa Singida imesema kuwa ipo tayari kuyaondoa makundi yote ya watu waliovamia maeneo ya wahadzabe wakiwemo wakulima na wafugaji na hivyo kuwawezesha kumiliki maeneo hayo kama zilivyo jamii nyingine nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo na mkuu wa mkoa wa Singida,Vicent Parseko Kone
Hatua hii inalenga kuwapa haki yao ya msingi ya kumiliki ardhi jamii hiyo ya wahadzabe kama jamii nyingine ya watanzania hapa nchini
Amewaambia washiriki wa kongamano la ufugaji nyuki barani afrika kuwa asilimia 77 ya eneo linalokaliwa na jamii ya wahadzabe tayari limevamiwa na wafugaji pamoja na wakulima jambo ambalo linatishia maisha ya jamii hiyo ya wahadzabe ambao maisha yao yote hutegemea sekta ya nyuki
Amesema katika mkakati huo wa kuwaondoa wavamizi wote pia Serikali imefanikiwa kupeleka huduma mbambali za kijamii zikiwemo za maji, miundo mbinu ya barabara, elimu na afya.
Mkuu huyo wa Mkoa pia amesema Serikali Mkoani humo imefanikiwa kuyapima maeneo yote wanamoishi wahadzabe ili kuwawezesha kupata hati miliki
Pia amesema Serikali imesambaza mizinga zaidi ya 150 katika jamii hiyo ili kuiwezesha kuendeleza zaidi ufugaji wa nyuki katika jamii hiyo pamoja na kuipatia mtama kwa ajili ya kuwawesha kuendelezaa kilimo katika vijiji vyao
Mkoa huo hivi sasa una watu wapatao 1,300 wa jamii ya wahadzabe ambapo 300 wanaishi katika wilaya ya Mkalama katika Kijiji cha Munguli
Wakizungumza katika kongamano hilo mmoja wa jamii hiyo ya wahadzabe amesema jamii hiyo inayo haki ya kumiliki ardhi kama jamii nyingine ya kitanzania
Aidha ameitaka serikali kukomesha vitendo vya baadhi ya jamii kuvamia maeneo yao kwa kutumia nguvu za kiuchumi walizonazo
Hivyo ameitaka serikali kuhakikisha jamii ya wafugaji na wakulima kufuata taratibu pale wanapoingia katika baadhi ya maeneo
Amekiri kuwa kwa asilimia kubwa jamii ya wahadzabe walikuwa hawajui haki haki zao pamoja na matumizi ya ardhi
Serikali Mkoa wa Singida imesema kuwa ipo tayari kuyaondoa makundi yote ya watu waliovamia maeneo ya wahadzabe wakiwemo wakulima na wafugaji na hivyo kuwawezesha kumiliki maeneo hayo kama zilivyo jamii nyingine nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo na mkuu wa mkoa wa Singida,Vicent Parseko Kone
Hatua hii inalenga kuwapa haki yao ya msingi ya kumiliki ardhi jamii hiyo ya wahadzabe kama jamii nyingine ya watanzania hapa nchini
Amewaambia washiriki wa kongamano la ufugaji nyuki barani afrika kuwa asilimia 77 ya eneo linalokaliwa na jamii ya wahadzabe tayari limevamiwa na wafugaji pamoja na wakulima jambo ambalo linatishia maisha ya jamii hiyo ya wahadzabe ambao maisha yao yote hutegemea sekta ya nyuki
Amesema katika mkakati huo wa kuwaondoa wavamizi wote pia Serikali imefanikiwa kupeleka huduma mbambali za kijamii zikiwemo za maji, miundo mbinu ya barabara, elimu na afya.
Mkuu huyo wa Mkoa pia amesema Serikali Mkoani humo imefanikiwa kuyapima maeneo yote wanamoishi wahadzabe ili kuwawezesha kupata hati miliki
Pia amesema Serikali imesambaza mizinga zaidi ya 150 katika jamii hiyo ili kuiwezesha kuendeleza zaidi ufugaji wa nyuki katika jamii hiyo pamoja na kuipatia mtama kwa ajili ya kuwawesha kuendelezaa kilimo katika vijiji vyao
Mkoa huo hivi sasa una watu wapatao 1,300 wa jamii ya wahadzabe ambapo 300 wanaishi katika wilaya ya Mkalama katika Kijiji cha Munguli
Wakizungumza katika kongamano hilo mmoja wa jamii hiyo ya wahadzabe amesema jamii hiyo inayo haki ya kumiliki ardhi kama jamii nyingine ya kitanzania
Aidha ameitaka serikali kukomesha vitendo vya baadhi ya jamii kuvamia maeneo yao kwa kutumia nguvu za kiuchumi walizonazo
Hivyo ameitaka serikali kuhakikisha jamii ya wafugaji na wakulima kufuata taratibu pale wanapoingia katika baadhi ya maeneo
Amekiri kuwa kwa asilimia kubwa jamii ya wahadzabe walikuwa hawajui haki haki zao pamoja na matumizi ya ardhi
Hatua hii itachangia kuvutia zaidi masoko ya nje kutokana na watalii hao kutembelea viwanda hivyo
Aidha Dakta Kashuliza amesisitiza kuwa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi limejipanga kuimarisha elimu kwa wazalishaji na wafugaji wa nyuki ili waweze kuzingatia uzalishaji wa asali katika viwango vyenye ubora kimataifa
Elimu hiyo itatolewa na baraza hilo kwa ushirikino na TBS ili kuwezesha asali ya Tanzania kupata masoko ya uhakika nje ya nchi.amesisitiza Katibu Mtendaji huyo wa baraza hilo
Mbali na hatua hiyo Dakta Kashuliza amesema Baraza limeanzisha Programu ya majaribio katika miko 10 ya Tanzania bara kuhisiana na ufugaji nyuki ili wafugaji hao waweze kufuga kiisasa zaidi na kibiashara katika viwango vyenye ubora kimataifa
Dakta Kashuliza ameitaja mikoa inayotekeleza Programu hiyo ya majaribio kuwa ni Mkoa wa Pwani,Dodoma,Morogoro,Tanga,Manyara, Iringa, Singida, Tabora Katavi na Kigoma
Amesema baraza hivi sasa linasimamia kwa nguvu zote suala la wafugaji kutumia teknolojia bora zaidi katika ufugaji wa nyuki kwa kutumia mizinga bora
Mbali na hatua hii Baraza pia limeingia mikataba na wadau mbalimbali wa nje ya nchi ili kuwaunganisha wazalishaji wa asali nan je kuweza kupata masoko ya uhakika ya mazao ya nyuki kutoka Tanzania.Amesisitiza Dakta Kashuliza
No comments:
Post a Comment